HABARI KWA WAKATI KUTOKA HAPA

Tunakuhakikishia kupata habari zote zilizo muhimu kutoka ulimwenguni kote kwa wakati, unaweza kusubscribe mtandao wetu na ukawa unapokea habari zote katika email yako punde tu tuchapishapo machapisho yetu. Jiunge na mitandao yetu ya Facebook na Twitter kutupata kirahisi.

HABARI ZA MICHEZO

Sasa Fichuo tunakuhakikishia kupata taarifa zote za kimichezo kutoka viwanja mbalimbali duniani, lengo ni kuhakikisha hupitwi na lolote katika ulimwengu wa michezo.Jiunge na mitandao yetu ya Facebook na Twitter kutupata kirahisi.

TAARIFA ZA BURUDANI NA HABARI ZA WASANII

Unapenda masuala ya burudani? Ni jukumu letu kuhakikisha unazipata info zote za burudani na wasanii wanaokupa burudani, unapata video mpya, movie pamoja na muziki. Kaa karibu nasi.

KURASA ZA MAGAZETI KILA SIKU

Tunakupatia kila ambacho kinaandikwa katika magazeti ya Tanzania na nje ya Tanzania, usitie shaka ukishindwa kununua gazeti uipendalo, sogea karibu nasi na upate kila unachokihitaji.

MAHUSIANO

Fahamu mambo mengi katika ulimwengu wa mapenzi kwa kupitia dondoo, simulizi na visa mbalimbali kupitia Fichuo Online, Jiunge na mitandao yetu ya Facebook na Twitter kutupata kirahisi.

Jumanne, Septemba 30, 2014

NICKI MINAJ KUWA MC KATIKA MTV 2014

Mwanamuziki wa miondoko ya kufokafoka Nicki Minaj anaelekea kukamata mic maaruku kama mc katika tuzo za mwaka huu za MTV Europe Music Awards maarufu kama EMAs mjini Glasgow, nchini Scotland. Kama hiyo haitoshi mlimbwende huyo atatumbuiza kwenye tamasha hilo la ugawaji tuzo November 9.
Mpaka sasa mwanadada Katy Perry anaongoza kwa kuchaguliwa kuwania tuzo takriban saba ikiwemo ile ya best female, pop act, video na maonesho hai.
Katty anachuana na mwanadada mwingine Ariana Grande, ambaye anawania tuzo sita wakati huo huo 5 Seconds of Summer na Pharrell Williams wanawania tuzo tano kila mmoja wakiwatangulia One Direction.
Nicki Minaj alitumbuiza wimbo wake wa Anaconda katika tuzo za MTV VMA mjini California mwezi August mwaka huu anawania tuzo zingine nne katika tuzo za EMAs.

HII NDIO NCHI YENYE PANYA HATARI ZAIDI AFRIKA

Mji wa Johannesburg nchini Afrika Kusini ni mmoja wa miji inayokua kwa kasi barani Afrika, lakini mji huo unakabiliwa na tatizo la kuvamiwa na panya walionona ambao huwatafuna watoto wadogo majumbani na wengine kufariki dunia. Maafisa wa halmashauri ya jiji la Johannesburg sasa wamezidisha juhudi ya kupambana na tatizo hilo ambalo limekuwepo kwa muda mrefu.

HIVI ULIIPATA ISHU YA RAILA ODINGA KUTIWA BAKORA???

Hali ya taharuki iliibuka katika mkutano wa hadhara katika jimbo la Kwale nchini Kenya, baada ya mwanamume mmoja kwenda ukumbini na kuanza kutandika bakora kiongozi wa upinzani Raila Odinga pamoja na wanasiasa wengine.
Raila alikuwa amejiunga na kikundi cha wanawake waliokuwa wanacheza densi ya kitamaduni kuwatumbuiza wageni, pamoja na gavana wa jimbo la Kwale Pwani ya Kenya Salim Mvuruya katika mkutanmo wa kisiasa.
Walikuwa wameambatana na viongozi wengine, wakiwemo, Seneta Juma Boy, Hassan Omar, Agnes Zani, James Orengo, Johnstone Muthama na wengineo.
Mwanamume huyo alimshambulia Odinga ambaye ni waziri mkuu wa zamani na kumchapa mara mbili kabla ya kumgeukia gavana wa jimbo hilo na pia kumchapa mara mbili. Hata hivyo mwanamume huyo alishindwa nguvu na walinzi wa Raila Odinga.
Polisi walithibitisha kuwa walimkamata mwanamume huyo na kumwachilia baada ya kugundua kuwa alikuwa na matatizo ya kiakili.
Haijulikani kwa nini mwanammume huyo alimshambulia Raila ila baadhi wabnasema ni kwa sababu alighadhabishwa pale waziri mkuu alipocheza densi na mwanamke aliyesemekana kuwa mke wake ambaye alikuwa katika kikundi cha wanawake waliokuwa wanawatumbuiza wageni waheshimiwa.
Viongozi waliofika walilazimika kusitisha densi hiyo kabla ya mwanamume huyo kushindwa nguvu.

SASA TEGEMEA KUMUONA RIHANNA KATIKA MOVIE YA JAMES BOND KAMA BOND GIRL

Ripoti zilizotolewa na gazeti la Sunday Mirror zinaeleza kuwa waandaaji wa movie za Bond wamemuomba Rihanna kuigiza kama ‘Bond Girl’ kwenye filamu hizo.
Kwa mujibu wa chanzo cha Sunday Mirror, Rihanna anadaiwa kuifurahia sana offer hiyo kwa kuwa yeye pia ni shabiki mkubwa wa filamu za James Bond.
Rihanna ni shabiki mkubwa sana wa filamu za Bond na ameipenda sana aidea ya kuonekana kwenye moja kati ya filamu hizo. Hakutaka hata kufikiria kuhusu ombi la waandaaji hao, anajua anataka kufanya.
Kilieleza chanzo hicho.
Daniel Craig ambaye anacheza uhusika wa James Bond kwa sasa atakuwa ameshampitisha Rihanna kwa kuwa aliwahi kumpendekeza kama ‘dream Bond Girl’ wake alipoambiwa kupendekeza kati ya Beyonce na Rihanna.
Filamu ya James Bond ijayo iliyopewa jina la ‘Bond 24’ iliyoongozwa na Sam Mendes inatarajiwa kutoka November 2015.

HABARI ZA MATUKIO YA MAUAJI NA MADAWA YA KULEVYA IRINGA LEO

Mtu mmoja amefariki Mkoani Iringa kwa ajali ya barabarani huku jeshi la polisi likimshikilia mtu mmoja kwa tuhuma ya kukutwa na madawa ya kulevywa aina ya bhangi. Kamanda wa jeshi la polisi Mkoani Iringa ACP Ramadhani Mungi amesema Godfrey Nkini umri miaka 40 mkazi wa Dar es Saalam amefariki baada ya kutokea ajali ya kugongana kwa magari mawili ya mizigo maeneo ya Rungemba barabara kuu ya Iringa-Mbeya wilaya ya Mufindi Mkoa wa Iringa. Kamanda Mungi ameongeza kuwa ajali hiyo imehusisha gari lenye namba za usajili T.135 BTD likiwa na tera namba T.347 BAS aina Scania lililokuwa likiendeshwa na marehemu akitokea nchini Congo kuelekea Dar es Salaam na kugongana na gari namba T.538 APP lenye tera namba T.605 BFM Aina ya Scania likiendeshwa na Charles Paison umri miaka 40 mkazi wa Mbeya. Aidha amesema ajali hiyo imepelekea majeruhi kwa Charles Paison na Thabiti Saleh umri miaka 30 mkazi wa Dar es Salaam ambao wamelazwa hospitari ya Mafinga wilaya ya  Mufindi Mkoa wa Iringa kwa matibabu zaidi chanzo chake kikiwa ni mwendo kasi. Hata hivyo Kamanda Mungi amesema askari polisi wakiwa doria maeneo ya Makorongoni Manispaa na Mkoa wa Iringa wamemkamata Zarina Juma umri miaka 25 mkazi wa mawelewele Manispaa ya Iringa akiwa na bhangi kete 68 alizozihifadhi kwenye mfuko wa suruali chanzo kikiwa ni kujipatia kipato.

TAREHE YA LEO KATIKA HISTORIA

Tarehe 30 Septemba miaka 29 iliyopita alifariki dunia mvumbuzi wa kipimo kinachotumiwa kupimia nguvu ya mitetemeko ya ardhi Charles Richter. Charles Richter alishirikiana na mhakiki mwingine kusanifu nguvu ya mitetemeko kwa mujibu wa nishati inayotokana na mawimbi ya mitetemeko hiyo toka daraja moja hadi 9 na kusajili kipimo cha Rishta. Kabla ya hapo wataalamu walikuwa wakipima mitetemeko ya ardhi kwa mujibu wa athari zake, kipimo ambacho hakikuwa cha kuaminika.

Siku kama ya leo miaka 48 iliyopita nchi ya Botswana ilifanikiwa kupata uhuru kutoka kwa mkoloni Mwingereza. Mwaka 1885 Botswana iliwekwa katika himaya ya mkoloni Mwingereza. Tangu mwaka 1920 mapambano makali ya wapigania uhuru nchini humo yalishadidi na Botswana ikapata uhuru mwaka 1966 na kukaundwa serikali ya jamhuri. Botswana inapatikana kusini mwa bara la Afrika na inapakana na nchi za Afrika Kusini, Zimbabwe na Namibia.

ALICHOKIFANYA CHRIS BROWN ALIPOVAMIWA NA BINTI WAKATI YUKO NA KARRUECHE

Chris Brown ameingia tena matatizoni baada ya kumzingua shabiki wa kike anaedaiwa kumrukia na kujaribu kumkiss mbele ya mrembo wake Karrueche Tran katika Club moja ya usiku.
Kwa mujibu wa TMZ, mwimbaji huyo wa ‘Loyal’ aliyekuwa na onesho katika club hiyo huko Texas, badala ya kuwaacha walinzi wake wamshughulikie msichana huyo kwa hasira alimsukuma vibaya.
Vyanzo vimeieleza Hollywoodlife kuwa mama mzazi wa Chris Brown na mpenzi wake wamekuwa na hofu kubwa kufuatia matatizo mfululizo yanayomtokea mwimbaji huyo.
Chris Brown alishauriwa hivi karibuni kutojiingiza katika matatizo baada ya kutoka jela hivi karibuni alikotumikia kifungo cha siku 108 kwa kosa la kuvunja masharti ya kipindi cha matazamio.

'ELLO' MTANDAO WA KIJAMII UNAOKUJA KASI DUNIANI

Mtandao wa kijamii wa Ello unapokea maombi 31,000 ya watumiaji wanaotaka kujiunga kila saa moja hali ambayo inaibua ushindani mkubwa kwa mtandao wa Facebook.
Muanzilishi wa mtandao huo Paul Budnitz ameiambia BBC kuwa wakati mtandao huo unaazishwa ulilenga watu kuhudumia marafiki 90 tu.
Mtandao huu kwa mjibu wa muanzilishi umeanzishwa August mwaka huu ukiwa ambapo hauna gharama yoyote kwa mtumiaji iwe matangazo ama kulipia data.
Hata hivyo baadhi ya watumiaji wameubatiza kwa jina la Anti-Facebook mtandao huo, wakimaanisha kwamba ndiye mpinzani mkubwa wa Facebook.
Baadhi ya wataalam wa masuala ya kimitandao wamekosoa mfumo wa Ello kutotoza gharama yoyote wakidai kuwa katika siku za usoni huenda mtandao wa Ello utalazimika kutoza kiasi kidogo cha fedha kwa watumiaji wake.
Paul Budnitz mtengenezaji wa baiskel za kampuni ya Vermont ameiambia BBC kuwa wapo imara katika ushindani wa kimitandao na kujigamba kuwa ana wataalamu wa kutosha kukabiliana na makampuni pinzania.
Hata hivyo kuhusiana na baadhi ya watu kuuiita kwa jinala bandia la anti-Facebook mtandao huo yeye amesema wanajiendesha kama mtandao wenye mtazamo wake binafsi na si kutegemea mtazamo wa mtandao wa Facebook.

VYOMBO VYA HABARI VIMESHINDWA KUANDIKA KASHFA ZA RAIS WA ARGENTINA DHIDI YA MAREKANI

Vyombo vikuu vya habari duniani vimejizuia kurusha hewani matamshi ya Rais wa Argentina katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ambayo yalikosoa vikali siasa za Marekani kimataifa.
Katika hotuba yake kwenye mkutano wa 69 wa Baraza Kuu, Bi. Cristina Fernandez de Kirchner Rais wa Argentina ameelezea masuala mbalimbali kuanzia mabadiliko yanayotakiwa kwenye Mfuko wa Fedha wa Kimataifa hadi matatizo ya Wapalestina na vita dhidi ya ugaidi.
Ameihoji Marekani kwamba imekuwaje sasa inashambulia baadhi ya makundi kama lile la kigaidi la Daesh ambalo imekuwa ikiliunga mkono ili liangushe serikali ya Syria.
Rais hiyo amekosoa siasa za alizoziita za ‘kindumilakuwili’ za Marekani, na kuuliza kwamba
Daesh na Al Qaeda wanapata wapi silaha? Jana walikuwa makundi ya ukombozi na leo ni magaidi?
Katika hatua nyiningine, rais huyo wa Argentina ametupilia mbali madai yanayotolewa dhidi ya Iran tangu mwaka 1994 kuhusiana na shambulizi la bomu lililolenga kituo cha Mayahudi mjini Buenos Aires, na kusema kwamba uchunguzi uliofanywa na na nchi yake umethibitisha kwamba Iran haikuhusika katika shambulio hilo.
Wapiganaji wa kudni la Daesh ambalo sasa ni kundi la kigaidi, mwaka 2012 lilipewa mafunzo na maajeti wa shirika la kijesusi la Marekani (CIA) huko nchini Jordan kwa lengo la kuiondoa madarakani serikali ya Syria.

AADHIBIWA BAADA NA KUFUNGA GOLI NA KUMSHUKURU MUNGU

Mchezaji wa Kansas City Chiefs Husain Abdullah aliadhibiwa vikali na refarii baa da ya kupiga sijida baada ya kufunga bao katika mchezo wa soka ya Marekani Kansas walipoinyuka New England Patriots 41-14.
Refarii alimwadhibu papo hapo Abdullah alipoinuka baada ya kusheherekea kwa kupiga sijida.
Aliyekuwa refarii wa zamani wa NFL Mike Pereira alisema kuwa sio hatia mtu kupiga sijida.
Tukio hilo linawadia wakati ambapo ligi hiyo inapigwa msasa kufuatia utovu wa nidhamu mbali na tuhuma chungu nzima kuhusiana na wachezaji wa ligi hiyo.
Tayari wandani wa NFL wanadai kuwa kuna upendeleo kwani mchezaji mwengine nyota Tim Tebow hakuadhibiwa baada ya kuonesha ishara yake al maarufu “Tebowing” msimu wote wa mwaka wa 2011.
Abdullah amejitokeza kutetea dini yake ya Uislamu sawa na vile Tebow huonesha wazi kuwa ni Mkristo.
Aidha Abdula alihiji mwaka uliopita alipoambatana na kakake Hamza,kuenda kwa hajji huko Mecca.
Kwa mujibu wa washika dau wanaishauri NFL itangaze wazi msimamo wake kuhusiana na ishara za kidini ilikutoa utata unaoibuka .

MICHUANO YA UEFA INAYOPIGWA LEO

Michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya inaendelea tena hii leo kwa michezo ya mzunguuko wa pili ya hatua ya makundi ambapo makundi yatakayohusika ni kuanzia kundi la tano hadi la nane.

Kundi la Tano:

Arena Khimki, Khimki

CSKA Moscow v Bayern Munich

Etihad Stadium, Manchester

Manchester City England v Italy Roma


Kundi la sita:

Parc des Princes, Paris

Paris Saint-Germain v Barcelona

GSP Stadium, Nicosia (Cyprus)

APOEL v Ajax



Kundi la saba:

Estádio José Alvalade, Lisbon

Sporting Lisbon v Chelsea

Veltins-Arena, Gelsenkirchen

Schalke 04 v MK Maribor (Slovenia)


Kundi la nane:

Arena Lviv, Lviv

Shakhtar Donetsk v FC Porto

Borisov Arena, Barysaw (Belarus)

BATE Borisov v Athletic Bilbao

MWANAFUNZI AFA BAADA YA KUFUKIWA NA KIFUSI MBEYA

MWANAFUNZI WA DARASA LA SITA KATIKA SHULE YA MSINGI SANZYA WILAYA YA MOMBA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA VALIUD SIAME@KIMUNDE (13) MKAZI WA KIJIJI CHA KAONGA ALIFARIKI DUNIA BAADA YA KUANGUKIWA NA KIFUSI CHA MCHANGA.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 29.09.2014 MAJIRA YA SAA 13:00 MCHANA HUKO KATIKA KIJIJI CHA KAONGA, KATA YA CHILULUMO, TARAFA YA KAMSAMBA, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA, WAKATI TUKIO HILO LIKITOKEA MAREHEMU ALIKUWA NA WANAFUNZI WENZAKE WAKICHIMBA NA KUBEBA MCHANGA KWA AJILI YA UJENZI WA NYUMBA ZA KULALA WAALIMU SHULENI HAPO.
MWILI WA MAREHEMU UMEFANYIWA UCHUNGUZI WA KITABIBU NA KUKABIDHIWA NDUGU KWA MAZISHI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WAZAZI/WALEZI KUWA MAKINI KWA KUTOA UANGALIZI WAKUTOSHA IKIWA NI PAMOJA NA KUWASIMAMIA WATOTO KATIKA SHUGHULI WANAZOWATUMA KUFANYA ILI KUEPUKA MADHARA YANAYOWEZA KUEPUKIKA.

HABARI KAMILI KUHUSU KIKONGWE WA MIAKA 90 ALIYEUAWA MBEYA

KIKONGWE MWENYE UMRI WA MIAKA 90 ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA BAPONDO NGAO MKAZI WA KIJIJI CHA UKWILE WILAYANI MBOZI ALIUAWA KWA KUKATWA NA KITU CHENYE NCHA KALI SEHEMU ZA KICHWANI NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA.
MWILI WA MAREHEMU UMEKUTWA MNAMO TAREHE 29.09.2014 MAJIRA YA SAA 10:00 ASUBUHI HUKO KATIKA KIJIJI UKWILE, KATA YA ISANDULA, TARAFA YA VWAWA, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA, WATU HAO WALIMVIZIA MAREHEMU AKIWA AMELALA NDANI YA NYUMBA YAKE NA KISHA KUMVAMIA NA KUANZA KUMKATAKATA NA KUPELEKEA KIFO CHAKE.
CHANZO CHA MAUAJI HAYO BADO KUFAHAMIKA. MWILI WA MAREHEMU UMEKUTWA NA MAJERAHA MAKUBWA MAWILI YA KUKATWA NA KITU CHENYE NCHA KALI SEHEMU ZA KICHWANI. MAREHEMU ALIKUWA ANAISHI PEKE YAKE MAENEO YA MASHAMBANI UMBALI WA ZAIDI YA KILOMITA TANO [05] KUTOKA MAKAZI YA WATU.
HAKUNA MTU/WATU WALIOKAMATWA KUHUSIANA NA TUKIO HILI, MSAKO MKALI UNAENDELEA KUWATAFUTA WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MTU/WATU WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO ILI AZITOE MARA MOJA KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAHUSIKA WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.

Jumatatu, Septemba 29, 2014

MTOTO AMUUA BABA YAKE MBEYA

MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA RICHARD NELSON FWAMBO (50) MKAZI WA UTAMBALILA WILAYA YA MBARALI ALIUAWA KWA KUKATWA NA KITU CHENYE NCHA KALI SEHEMU ZA KICHWANI NA MTU ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA KHAMIS MGALA (32) MKAZI WA MLOWO – MBOZI AMBAYE NI MTOTO WAKE WA KAMBO.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 28.09.2014 MAJIRA YA SAA 01:00 USIKU HUKO KATIKA KITONGOJI CHA MAGAMBA, KIJIJI CHA UTAMBALILA, KATA YA NAMBIZO, TARAFA YA ITAKA, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA MTUHUMIWA KABLA YA KUTEKELEZA TUKIO HILO, ALIVUNJA MLANGO NA KUINGIA NDANI NA KUANZA KUMSHAMBULIA MAREHEMU AMBAYE ALIKUWA AMELALA NDANI YA NYUMBA YAKE AKIWA NA MKE WAKE AITWAYE YUSTINA KASHAPAMBA@NAKAMANGA (40) MKAZI WA UTAMBALILA AMBAYE NI MAMA MZAZI WA MTUHUMIWA.
CHANZO CHA TUKIO HILO, INADAIWA KUWA MTUHUMIWA ALIKUWA HATAKI/HAPENDI MAMA YAKE HUYO KUISHI NA MAREHEMU AMBAYE NI BABA YAKE WA KAMBO BAADA YA BABA YAKE MZAZI KUFARIKI. MWILI WA MAREHEMU UMEKUTWA NA MAJERAHA MANNE SEHEMU ZA KICHWANI.
AIDHA, INADAIWA KUWA MTUHUMIWA KWA MUDA MREFU HAKUONEKANA KIJIJINI HAPO LAKINI GHAFLA SIKU MOJA KABLA YA TUKIO HILO ALIONEKANA. TAARIFA ZA AWALI ZINADAI KUWA, MTUHUMIWA KIPINDI CHA NYUMA ALIWAHI KUMJERUHI MAMA YAKE PAMOJA NA MAREHEMU. MSAKO MKALI UNAENDELEA WA KUMTAFUTA MTUHUMIWA KWANI ALIKIMBIA NA KUTOKOMEA KUSIKOJULIKANA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.

MWINJILISTI AUAWA MBEYA


MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA AMBUMBULWISYE MWASOMOLA (35) MUINJILISTI NA MKAZI WA KIJIJI CHA LUKASI ALIUAWA KWA KUPIGWA NA MCHI WA KUTWANGIA SEHEMU ZA KICHWANI NA MTU ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA SWALAPO MWAISANILA (56) MKAZI WA KIJIJI CHA LWANGWA AMBAYE NI MGONJWA WA AKILI.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 27.09.2014 MAJIRA YA SAA 23:30 USIKU HUKO KATIKA KIJIJI CHA LUKASI, KATA YA LWANGWA, TARAFA YA BUSOKELO, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA TUKIO HILO NI BAADA YA MAREHEMU AMBAYE NI MUINJILISTI WA KANISA LA BAPTISTI KUTAKA KUMFANYIA MAOMBI MTUHUMIWA HUYO KUTOKANA NA UGONJWA WA AKILI ALIOKUWA NAO NA NDIPO MTUHUMIWA ALICHUKUA MCHI NA KUMPIGA NAO MAREHEMU KICHWANI NA KUPELEKEA KIFO CHAKE. MTUHUMIWA AMEKAMATWA.

ACHOMWA NA MIKUKI HADI KUFA MBEYA

MTU MMOJA ALIFAHAMIKA KWA JINA MOJA LA KABOTE (41) MKAZI WA MWANAVALA WILAYANI MBARALI ALIUAWA KWA KUCHOMWA MIKUKI SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA NYAMANIENGO KINANGA AMBAYE NI MMILIKI WA KLABU CHA POMBE ZA KIENYEJI.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 28.09.2014 MAJIRA YA SAA 23:00 USIKU HUKO KATIKA KLABU CHA POMBE ZA KIENYEJI, KIJIJI CHA MWANAVALA, KATA YA IMALILO SONGWE, TARAFA YA RUJEWA, WILAYA YA MBARALI, MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA, CHANZO CHA TUKIO HILO NI BAADA YA MAREHEMU KUSHINDWA KULIPA KIASI CHA TSHS. 500 ALIYOKUWA AKIDAIWA BAADA YA KUNYWA POMBE KLABUNI HAPO.
WATU 13 WANASHIKIRIWA KWA MAHOJIANO KUHUSIANA NA TUKIO HILI KWANI BAADA YA MAREHEMU KUSHINDWA KULIPA FEDHA HIYO, WATU HAO 13 WALIOKUWEPO ENEO HILO WALIANZA KUMKIMBIZA MAREHEMU HUKU WAKIPEGA KELELE. MSAKO MKALI UNAENDELEA KUWATAFUTA WATUHUMIWA WENGINE WA TUKIO HILI KWANI WANAFAHAMIKA NA WALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI AKIZUNGUMZA NA FICHUO TZ, AMETOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.

MWANAMUZIKI WA BONGO FLEVA AFARIKI DUNIA

Msanii wa Bongo Fleva aliyewahi kutamba na nyimbo kama 'Kua uone', 'Usimdharau usiyemjua', Said Salim 'Side Boy Mnyamwezi' amefariki dunia leo katika Hospitali ya Nyangao iliyopo Mkoani Lindi. Mtandao wa Fichuo Tz bado unafuatilia undani wa kifo chake na hata kile kilichosababisha mauti ya Side Boy Mnyamwezi. Tunatoa pole kwa familia na wote walioguswa na msiba huu. R.I.P Side Boy Mnyamwezi.

TAREHE YA LEO KATIKA HISTORIA

Siku kama ya leo miaka 22 iliyopita, ulifanyika uchaguzi huru wa kwanza nchini Angola. Katika uchaguzi huo chama cha MPLA kilichokuwa kikiongoza nchini humo tangu mwaka 1976 kilipata ushindi na kiongozi wake Jose Edward Dos Santos akachaguliwa tena kuingoza nchi hiyo. Ni vyema kuashiria hapa kwamba, Angola ilitumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe baada ya kupata uhuru kutoka kwa mkoloni Mreno hapo mwaka 1975. Vita vya ndani nchini humo vilihitimishwa rasmi mwaka 2002 baada ya kuuawa kiongozi wa chama cha upinzani cha UNITA Jonas Savimbi.
Siku kama ya leo miaka 33 iliyopita, muwafaka na tarehe 7 Mehr 1360 Hijria Shamsia, aliuawa shahidi Hujjatul Islam Sayyid Abdul Karim Hasheminejad mwanachuoni na mwanamapambano shupavu wa Iran katika mji wa Mashhad. Sayyid Hasheminejad aliuawa shahidi baada ya kupigwa risasi na mmoja wa wanachama wa kundi la Munafikiin. Mwanachuoni huyo alikuwa mstari wa mbele katika harakati za mapinduzi nchini Iran dhidi ya utawala wa Shah, na aliwahi kuteswa na kuwekwa gerezani mara kadhaa.
Siku kama ya leo miaka 113 iliyopita, alizaliwa mwanafizikia mashuhuri wa Italia Enrico Fermi katika mji wa Roma. Baada ya kukamilisha masomo ya chuo kikuu aliweza kuvumbua kanuni ya Mwendo wa Molekuli ya Gesi. Fermi alifanya uchunguzi kuhusu mabadiliko ya atomu na akafanikiwa kutengeneza betri ya atomu kwa kuipasua na kutoa nje nishati yake. Mwanafizikia huyo wa Italia alifariki dunia mwaka 1954.
Na miaka 96 iliyopita muwafa na leo, nchi ya Bulgaria ilisalimu amri baada ya kushindwa mara kadhaa katika Vita Vikuu vya Kwanza vya Dunia. Bulgaria ilikuwa pamoja na Ujerumani, utawala wa Othmania, Austria na Hungary na zilikuwa zikipigana dhidi ya Ufaransa, Russia, Uingereza na Italia. Baada ya Bulgaria kushindwa katika vita vya Macedonia, Desemba 15 mwaka 1918 ilitia saini Mkataba wa Salonica katika mji wenye jina hilo nchini Ugiriki ya leo.

KUBWA KUTOKA IRINGA LEO

Ili kuwa na maendeleo ya elimu wazazi na walezi Mkoani Iringa wametakiwa kuendelea na uchangiaji wa michango ya sekta hiyo na kutowaruhusu wanafunzi waliohitimu darasa la saba kwenda kutumikishwa kazi za ndani.
Akiwa katika mahafari ya darasa la saba shule ya msingi Ilambilole wilaya ya Iringa Vijijini Mwenyekiti wa jumuhiya ya wazazi Mkoa wa Iringa Bw.Ephrahim Mhekwa amesema nidhamu kwa wanafunzi na ushirikiano wa kutosha kati ya walimu na wazazi hupelekea ufaulu mzuri kwa wanafunzi.
Bw.Ephrahimu ameongeza kuwa wananchi wanatakiwa kufanya kazi kwa bidii wakizingatia uhifadhi wa mazingira pia kuwa makini na matamko yanayotolewa nabaadhi ya vyama vya pamoja kuelimishana wao kwa wao juu ya maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi.
Aidha wakisoma lisara mbele ya mgeni rasmi wahitimu wa shule hiyo wamewataka wadau mbalimbali kutoa misaada ya hali na mali ili kupambana na changamoto za uhaba wa majengo na samani.
Hata hivyo sherehe hizo zimeenda sambamba na harambee iliyoendeshwa na diwani wa kata ya Nduli-Kising'a wilaya ya Iringa Vijijini Mh.Ritha Mlagala ambapo zaidi ya milioni mbili imepatikana pia mabati 50,siment 50 na madawati 10 yametolewa na mgeni rasmi Bw.Ephrahim Mhekwa kwa ajili ya ukarabati wa majengo na ununuzi wa vifaa mbalimbali vya shule hiyo.

MESSI KAFUNGA MAGOLI ZAIDI YA 400

Mshambulizi wa Barcelona Lionel Messi amesema kuwa hakuwahi kufikiria kuwa atawahi kufunga mabao 400.
Mchezaji huyo aliyewahi kutwaa taji la mchezaji bora duniani mara nne aliwahi mabao mawili katika mechi yao dhidi ya Grenada vigogo hao wa ligi kuu ya Uhispania walipofunga mabao 6-0 .
Mshambulizi huyo wa Argentina alifunga mabao mawili ya 400- na 401.
Kocha wa Barcelona Luis Enrique alimsifu kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27 akisema kuwa ilikuwa ni mafanikio makubwa.
Tangu atue Uhispania Messi ameifungia Barcelona mabao 359 akaifungia Argentina mabao 42 katika jumla ya mechi 506 alizoshiriki.
Kiungo huyo machachari ameisaidia sana Barcelona kutwaa mataji 21,yanayuojumuisha 6 ya ligi kuu ya Uhispania La Liga na 3 ya kombe la mabingwa barani Ulaya katika muongo mmoja uliopita.
Kibinafsi Messi alishinda mataji manne ya Ballon d'Ors,ambayo hutuzwa mchezaji bora duniani kuanzia mwaka wa 2009 hadi 2012.
"nitajitahidi zaidi kunogesha talanta yangu''

BAADA YA KUPATA RED CARD, ROONEY AOMBA RADHI

Mshambuliaji kutoka nchini Uingereza na klabu ya Man Utd, Wayne Mark Rooney amewataka radhi wachezaji wenzake kufuatia adhabu ya kadi nyekundu iliyomuangukia mwishoni mwa juma wakati wa mchezo wa ligi dhidi ya West Ham Utd kwenye uwanja wa Old Trafford.
Rooney ambaye pia ni nahodha wa kikosi cha Man Utd, amesema hana budi kuwataka radhi wachezaji wenzake kutokana na kufahamu kwamba aliwapa wakati mgumu mara baada ya kuonyeshwa kadi nyekundi zikiwa zimesalia dakika 30 mchezo huo kumalizika.
Amesema kwa hakika muamuzi Lee Mason alikuwa sahihi kumuonyesha kadi nyekundu kutokana na kosa la kumchezea ndivyo sivyo kiungo wa West Ham Utd, Stewart Downing, hivyo hana budi kujutia na kukubali makosa aliyoyafanya.
Kuadhibiwa kwa mshambuliaji huyo kwa kuonyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja kunaashiria ataikosa michezo mitatu ya ligi kuu ya soka nchini Uingereza inayofuata ambayo itashuhudia Man Utd wakipambana dhidi ya Everton, West Bromwich Albion pamoja na Chelsea.
Rooney atarejea kwenye kikosi cha Man Utd wakati wa mchezo dhidi ya mabingwa watetezi Man city ambao pia ni mahasimu wakubwa wa Man Utd mchezoa mbao utachezwa mwishoni mwa mwezi ujao.
Kadi nyekundu aliyoonyeshwa Wayne Rooney mwishoni mwa juma ni ya kwanza tangu alivyokumbana na adhabu kama hiyo mwezi Machi mwaka 2009.

AMBER ROSE AMFUMANIA WIZ KHALIFA LIVEEEEE

Uamuzi wa Amber Rose kutaka kutalakiana na mumewe Wiz Khalifa ulizua maswali mengi huku ‘uchepukaji’ ukitajwa kuwa chanzo cha yote.
Lakini kwa mujibu wa TMZ, Amber Rose alichukua uamuzi huo baada ya kumfumania Wiz Khalifa akiwa na mwanamke mwingine nyumbani kwake majira ya saa nane usiku.
Taarifa hizo zimeunganishwa na tweet ya Amber Rose inayoeleza kuwa anaendelea kulikumbuka tukio hilo.
Hata hivyo chanzo cha karibu na Wiz Khalifa kiliieleza TMZ kuwa rapper huyo aliwaambia kuwa alifanya makusudi kwa kuwa hataki tena kuendelea kuwa mume wa Amber Rose.
“I just didn't want to be married to her anymore.” Chanzo hicho kimemkariri Wiz Khalifa.
Inaelezwa kuwa hii ni moja kati ya sababu zilizomfanya Wiz Khalifa kutopinga uamuzi wa Amber Rose kudai talaka yake.
Taarifa za awali zilieleza kuwa Amber Rose na Nick Cannon walianzisha uhusiano wa mapenzi na kuwala kisogo Wiz na Mariah Carey lakini wote walikanusha taarifa hizo.

Jumapili, Septemba 28, 2014

UGONJWA WA UTI WAWEZA KUKUPOTEZEA MAISHA YAKO

Maambukizi Katika Njia ya Mkojo (UTI) ni moja kati ya magonjwa ambayo hayapewi msisitizo wa kutosha katika jamii licha ya kuwa wengi huathirika kwa ugonjwa huu bila kujua chanzo, tiba na kinga yake.
Ugonjwa huu huanza kuathiri mirija inayopitisha mkojo, baadaye huenea katika kibofu na figo. Mgonjwa anaweza kupata ugonjwa sugu wa figo na kupoteza maisha kama ugonjwa huu hautatibiwa mapema.
Wataalamu wa afya wanasema UTI husababishwa na vimelea ambao huingia kupitia mirija inayosafirisha mkojo na kuutoa nje. Vimelea hawa wanashambulia kibofu na baadaye huendelea mpaka kwenye figo. Hii ndiyo hatua kubwa ya ugonjwa ambayo inaweza kusababisha kifo au tatizo la kudumu.
Hawa ni vimelea wa jamii ya bakteria walio wanajulikana kwa jina la escherichia coli (E.coli).
Bakteria hawa wanapatikana katika utumbo mpana lakini husafiri kupitia njia ya haja kubwa kwenda katika njia ya mkojo na kusababisha maambukizi katika kibofu na figo.

YALIYOMKUTA SOULJA BOY

Rapper Soulja Boy alikuwa na kila sababu ya kumshitukia mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 7 baada ya msichana aliyewahi kuwa mpenzi wake kudai kuwa alizaa nae mwaka 2007.
Mwama jana Mackey mwenye umri wa miaka 23 alisambaza picha inayomuonesha akiwa na Soulja Boy na kueleza kuwa ilichukuliwa mwaka ambao alipewa ujauzito na rapper huyo.
Kwa mujibu wa TMZ, matokeo yaliyopatikana baada ya kufanyiwa vipimo vya DNA yameonesha kuwa kwa 99.9% mtoto huyo sio wa Soulja Boy.
Kipande cha document ya majibu hayo ambacho TMZ imekipata kinasomeka;
The alleged father is excluded as biolocal father of the tested child.

Alhamisi, Septemba 25, 2014

GOOD NEWS: CHANJO YA EBOLA KUPATIKANA HIVI KARIBUNI

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema kuwa, chanjo ya ugonjwa wa Ebola inaweza kuwa tayari kwa kiasi kikubwa mwishoni mwa mwaka huu ili kusaidia kupambana na virusi vya ugonjwa huo katika nchi za magharibi mwa Afrika.
WHO aidha imesema, kiasi cha chanjo hiyo kitakuwa cha kutosha kuweza kusaidia kudhibiti ugonjwa wa Ebola kwenye eneo hilo. Tangaza hilo limetolewa kufuatia uchunguzi uliofanywa na taasisi hiyo ya Umoja wa Mataifa ulioonesha kuwa asilimia 70 ya watu walioambukizwa virusi vya ugonjwa huo huko magharibi mwa Afrika wamefariki dunia.
Itakumbukwa kuwa, kuanzia tarehe 19 Septemba mwaka huu, idadi ya walioambukizwa ugonjwa huo katika nchi za Guinea, Liberia na Sierra Leone imeongezeka mno na kufikia watu 5,843, huku watu wapatao 2,800 wakiwa wamefariki dunia kutokana na ugonjwa huo.

TAZAMA WATOTO WANAVYOTUMIKISHWA VITANI

Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa UNICEF umetangaza kuwa, makundi ya wanamgambo wanaobeba silaha yanawatumikisha maelfu ya watoto vitani nchini Sudan Kusini. 
Fatuma Ibrahim afisa mwandamizi wa UNICEF Sudan Kusini amesema kuwa, hivi sasa karibu watoto elfu kumi wako mstari wa mbele kwenye mapigano nchini humo. Fatuma Ibrahim ameongeza kuwa, makundi yanayobeba silaha yanawalazimisha kwa nguvu watoto kwenda vitani. 
Afisa huyo wa UNICEF amesema kuwa, makundi yanayobeba silaha nchini humo mwanzoni mwa mwaka huu yaliahidi kutowatumia watoto vitani, ahadi ambayo bado haijatekelezwa hadi sasa. Mwanzoni mwa mwaka huu, Umoja wa Mataifa pia ulizituhumu pande zote zinazopigana nchini Sudan Kusini kwa kuwatumia watoto wadogo vitani. 
Inafaa kuashiria hapa kuwa, kuanzia mwezi Disemba mwaka jana hadi sasa, Sudan Kusini inashuhudia mapigano makali kati ya wanajeshi watiifu kwa serikali ya Rais Salva Kiir dhidi ya wanamgambo waasi wanaoongozwa na Riek Machar makamu wa zamani wa rais wa nchi hiyo.

JAMAA AMBAKA MTOTO WA MIAKA 12 IRINGA

Maneno Ilave mwenye umri wa miaka 21 mkazi wa maeneo ya Mkwawa Manispaa na Mkoa wa Iringa anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kumbaka na kumsababishia maumivu makali ya mwili mtoto mwenye umri wa miaka 12.
Hata hivyo Kamanda wa jeshi la Polisi mkoani Iringa ACP Ramadhani Mungi amesema chanzo cha tukio hilo ni tamaa ya mapenzi pia ametoa wito kwa walezi na wazazi kuwa makini katika malezi ya watoto wao ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanacheza sehemu za wazi na kuwahi kurudi nyumbani.

MTOTO AGONGWA NA GARI NA KUFARIKI IRINGA

Mtu mmoja amefariki mkoani Iringa baada ya kugongwa na gari. Akithibitisha kutokea kwa matukio hayo kamanda wa jeshi la polisi Mkoani Iringa ACP Ramadhani Mungi amesema Kelsensia Bonifasi umri miaka 7 mwanafunzi wa dalasa la kwanza shule ya msingi Sun Academy iliyopo maeneo ya Isakalilo Manispaa na mkoa wa Iringa amefariki papo hapo baada ya kugongwa na gari lenye namba za usajili T.306 CRM aina ya toyota Hiace.
Kamanda Mungi ameongeza kuwa ajali hiyo imetokea katika barabara ya Iringa-Kalenga Manispaa na Mkoa wa Iringa, chanzo kikiwa ni mwendo kasi na dereva wa gari hilo Rajabu Adamu umri miaka 28 mkazi wa eneo la Kihesa Manaispaa ya Iringa anashikiliwa na jeshi la polisi kwa uchunguzi zaidi.

RAIS GOODLUCK JONATHAN: BADO TUNAWATAFUTA WATOTO WALIOTEKWA NA BOKO HARAM

Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria amesema katika Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwamba, maafisa wa nchi yake bado wanafanya jitihada za kuwakomboa wasichana wa shule karibu 200 waliotekwa nyara na kundi la kigaidi la Boko Haram mwezi Aprili. 
Rais Jonathan ameongeza kuwa, ingawa miezi zaidi ya mitatu imepita tangu wasichana hao wa shule watekwe nyara, lakini hawajaacha kufanya jitihada za kuwakomboa. Rais wa Nigeria anakosolewa ndani na nje ya nchi kwa kuchelewa kuchukua hatua za kuwakomboa wasichana hao waliotekewa nyara na Boko Haram na kushindwa kulitokomeza kundi  hilo.
Wakati huo huo, jeshi la Nigeria limetangaza kwamba, zaidi ya wapiganaji 135 wa kundi la Boko Haram wamejisalimisha kwa vikosi vya usalama vya serikali na kukabidhi silaha zao huko kaskazini mashariki mwa nchi. 

MWANAHISTORIA MPYA WA KARNE YA 21 TOKA RUVUMA

Wasomi mkoani Ruvuma,wamemtaja Abate mstaafu Lambert Doerr OSB wa Abasia ya Peramiho kuwa ni Mwanahistoria wa karne ya 21 kutokana na mchango wake mkubwa wa kuchangia shughuli mbalimbali za maendeleo hapa Nchini ikiwemo katika nyanja ya Elimu.
Matamko hayo yalitolewa na Wasomi hao kwa nyakati tofauti wakati walipokuwa wakitoa mada mbalimbali katika kongamano lililoandaliwa kwa ajili ya kuzungumzia juu ya maisha na kazi zilizofanywa na Abate huyo katika kipindi chake cha miaka 50 ya Umisionari hapa Nchini lililofanyika kwenye ukumbi wa Nyerere chuo kikuu cha Sauti tawi la Songea.
Akitoa mada katika kongamano hilo Padre Dr.Xsaver Komba,alisema kuwa moja ya mchango wa uliotolewa na Abate Lambert wakati akiwa Mwalimu bora na mwadilifu katika Seminari ndogo ya Likonde na Seminari kuu ya Peramiho alifundisha kwabidii kwa kufuata misingi ya ualimu iliyopelekea  kutoa wasomi wengi ambao miongoni mwao ni viongozi wakubwa wa Serikali na Dini.
Alisema kuwa michango mingine aliyoitoa ni pamoja kuwaunganisha Waafrika kuwa kitu kimoja na wazungu kwenye nyumba za kitawa, kuwasomesha baadhi ya wananchi wa kijiji cha Mbinga Mharule kwa kuwalipia ada ya shule,
kusogeza huduma ya maji safi na salama kwa kilometa saba,kujenga zahanati,ujenzi wa barabara ya Lambert yenye urefu wa kilometa tatu,kusaidia wazee wasiojiweza,watoto Yatima pamoja na kuimarisha mahusiano kati ya dini ya kikristu na waislamu.
Alisema kuwa maadhimisho hayo ya Jubilei ya miaka 50 ya Umisionari Nchini yatakwenda sambamba na na uanzishwaji wa chuo cha ufundi cha Mtakatifu Lambert mjini hapa kitakachotoa fani ya kompyuta,ushonaji na uselemala kama sehemu ya kumuenzi.
Naye mmoja wa watoa mada na mwanafunzi  aliyefundishwa na Abate huyo,Dr.Damas Mbogoro ambaye amewahi kushika nyadhifa mbalimbali hapa Nchini alimwelezea Abate Lambert kuwa ni mtu  ambaye hakuwa mchoyo wa elimu na kudai kwamba alikuwa karibu na watu katika kusikiliza shida na matatizo yao.
Kwa upande wake mgeni rasmi katika kongamano hilo,Padre Dastan Mbano ambaye alimwakilisha Askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Songea Damian Dallu,alisema kuwa Abate Lambert ni hazina kubwa sio kwa upande wa kanisa peke yake bali ni kwa jamii nzima.
Mbano alisema kuwa kazi nzuri na kumbukumbu za Abate huyo zinapaswa kutangazwa,kuenziwa na kuhifadhiwa kwa ajili ya faida ya vizazi vijavyo huku mwakilishi wa Baraza la mila kasian
Shauritanga,alisema kuwa wamisionari Wabenediktini wa Abasia ya Peramiho watakumbukwa kwa mchango wao wa kusaidia kutunza kumbukumbu za mila na desturi za wangoni katika makumbusho ya vita ya majimaji na kuupatia mkoa na taifa kwa ujumla sifa pekee ya utunzaji.

ASAMOAH GIAN AKANUSHA KUMTOA KAFARA RAFIKI YAKE MWANAMUZIKI

Nahodha na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ghana, Asamoah Gyan, amekanusha madai kuwa alimtoa kafara yake ambaye pia alikuwa mwanamuziki mashuhuri nchini Ghana Castro. Gyan amesema tetesi hizo ni za kushangaza sana wala hazina msingi.
Mwanamuziki huyo aliyekuwa anaiimba nyimbo za mtindo wa Afrobeats, ambaye jina lake halisi ni Theophilus Tagoe, alitoweka pamoja na rafiki yake Janet Bandu, mnamo mwezi Julai.
Wawili hao walitoweka wakati walipokuwa wamekwenda likizo na Gyan ambaye alikuwa mchezaji wa zamani wa Sunderland, katika mji wa Ada.
Madai katika vyombo vya habari nchini Ghana yanasema kuwa kutoweka kwa rafiki ya Gyan kumezua wasiwasi baadhi wakidai kuwa huenda alimtoa kafara mwanamuziki huyo.
Castro na rafiki yake Bandu, walionekana kwa mara ya mwisho wakielekea baharini na baadaye iliarifiwa kuwa walizama.
Miili ya wawili hao haikuwahi kupatikana na madai yaliendelea kusambazwa mwezi huu wakati ambapo kakake Gyan, Baffour Gyan alidaiwa kuwa mmoja wa genge la vijana waliowashambulia wandishi wa habari waliohoji maswali kuhusu madai hayo.
Hata hivyo baadaye aliachiliwa na polisi waliokuwa wamemkata kwa lengo la kumfungulia mashitaka.
Tetesi hizo zilimfanya Gyan kuitisha mkutano na wandishi wa habari kuzungumzia madai hayo.
Wakili wake Kissi Agbyabeng alitoa taarifa akisema kuwa familia ya Gyan imeshangazwa sana na madai hayo na iliamua kutosema chochote ili polisi waendelee na uchunguzi wao.
Taarifa hiyo ilisema:
Tumekuwa kimya huku madai na tetesi zikienezwa kila upande katika vyombo vya habari. Tumekuwa kimya sio eti kwa sababu tunaficha ukweli, bali kwa sababu hatuoni umuhimu wa kusema kilichojiri mjini Ada. Tumekuwa kimya kwa sababu tunataka polisi wafanye kazi yao bila kuingiliwa.

UNAPENDA BIDHAA ZA APPLE KAMA iPHONE, iPAD NA iPOD? SASA MWANZILISHI WAKE ALIWAKATAZA WANAE KUZITUMIA

Bidhaa za kampuni ya Apple zina mashabiki na wateja wengi duniani, hii inathibitishwa na foleni kubwa ya watu waliojitokeza kwenye vituo mbalimbali duniani kununua toleo jipya la iPhone6.
Tumesikia watu wakiachana ama familia zikitengana kwa sababu tu baba ameshindwa kununua bidhaa za kielekroniki za kampuni ya Apple. Mwaka jana familia moja nchini China iliwauza watoto wao ili kupata pesa ya kununua iPhone5.
Kwa kuzingatia hayo, huenda ukadhani watoto wa mwanzilishi wa kampuni ya Apple na mgunduzi wa bidhaa hizo, Steve Jobs wanafaidi zaidi bidhaa hizo.
Na huenda ukadhani hata kuta za nyumba yao zingeweza kuwa za mfumo wa simu za kisasa za kupangusa ‘Screen Touch’ na mawasiliano ya hali ya juu ndani ya nyumba hiyo kwa mfumo huo.
Lakini ukweli ni kwamba, marehemu Steve Jobs hakuwaruhusu hata kidogo watoto wake kutumia iPhones, iPods wala iPads nyumbani kwake.
Katika article iliyoandikwa na New York Times wiki hii, mwandishi wa habari Nick Bilton ameeleza jinsi ambavyo alishangaa majibu ya Steve Jobs alipomuuliza jinsi ambavyo watoto wake wanapenda bidhaa za kampuni hiyo.
Hawajawahi kutumia kabisa. Tunadhibiti kiasi ambacho watoto wetu wanatumia teknolojia nyumbani.
Alijibu Steve Jobs.
Nae mwandishi maalum wa Steve Jobs, Walter Isaacson ambaye alikuwa akitumia muda mwingi nyumbani kwa boss wake huyo alithibitisha kuwa maoengezi ya uso kwa uso yalitawala katika nyumba hiyo.
Kila jioni Steve alikuwa akipata chakula cha usiku na familia yake kwenye meza kubwa jikoni, wakijadili vitabu na historia na vitu vingine vingi. Hakuna mtu aliyekuwa na iPad au computer. Watoto hawakuonekana kuwa addicted hata kidogo na vifaa hivyo.
Alieleza Isaacson.
Inaelezwa kuwa hata Steve Jobs hakuwa na tabia ya kutumia vifaa hivyo kwa muda mrefu.
Hata hivyo, Steve Jobs aliyefariki mwaka 2011 sio mtu maarufu pekee aliyeamini katika kuweka sheria kali kwa watoto wake kutumia vifaa hivyo, Chris Anderson, mhariri wa zamani wa Wired pia alieleza kuwa yeye na mkewe wamewazuia watoto wao kiasi kwamba watoto hao huwalalamikia sana wakilinganisha na uhuru wanaouona katika familia za mafiki zao.
Utafiti uliofanywa katika eneo la Chuo Kikuu cha California, Los Angeles na kuchapishwa hivi karibuni unaonesha kuwa siku chache baada ya kuzuia watoto kutumia vifaa vya kieletroniki vya simu, ufaulu wa watoto katika masomo ulipanda ghafla.
Utafiti unaonesha kuwa kwa wastani watoto nchini Marekani hutumia zaidi ya saa saba na nusu kwa siku katika matumizi ya simu za kupangusa na vifaa vingine vya kielekroniki kama iPads, iPod n.k.
Uamuzi ni wako, kumnunulia mwanao vifaa vya hivyo au kumuweka mbali na mapinduzi hayo ya kiteknolojia.

Jumatano, Septemba 24, 2014

SUAREZ AANZA NA VIJANA WA BARCELONA B

Mshambuliaji kutoka nchini Uruguay Luis Suarez, bado ana hamu ya kuwa sehemu ya kikosi cha FC Barcelona ambacho kwa msimu huu kipo chini ya meneja kutoka nchini Hispania Luis Enrique Martínez García.
Suarez, anaetumikia adhabu ya kufungiwa kucheza soka katika michuano ya kiushindani kwa kipindi cha miezi minne, ameonyesha hamu ya kutaka kurejea na kujiunga na wachezaji wengine wa FC Barcelona ambapo itakuwa ni mara yake ya kwanza baada ya kusajiliwa akitokea Liverpool, kufutia juhudi anazo zionyesha katika mazoezi pamoja na michezo ya kujipima nguvu ambayo inakihusisha kikosi cha Barcelona B.
Usiku wa kuamkia hii leo, mshambuliaji huyo alieacha gumzo nchini Brazil baada ya kumng’ata beki wa kati wa timu ya taifa ya Italia na klabu ya Juventus Giorgio Chiellini, alicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Indonesia chini ya umri wa miaka 19 ambapo Barcelona B imeichapa Indonesia kwa mabao 6 kwa sifuri.
Kocha wa Barcelona Luis Enrique amesema alitaka Suarez kucheza mchezo huo ili kuwa katika hali ya hamasa ya kimchezo, kabla ya kurejea uwanjani rasmi mwishoni mwa mwezi oktoba.
Suarez anaruhusiwa kushiriki michezo ya kirafiki pekee, na hatashiriki michuano ya ligi ya nchini Hispania La Lila mpaka tarehe 24 mwezi oktoba ambapo Barcelona itakutana na Real Madrid

NICK CANNON NA KASHFA YA KUVUNJA NDOA YA AMBER ROSE NA WIZ KHALIFA

Siku mbili baada ya Amber Rose kufuata taratibu za kisheria akidai talaka kwa mumewe Wiz Khalifa, Nick Cannon ameendelea kunyoshewa vidole kuwa chanzo cha yote na kudaiwa kuchepuka na mrembo huyo kwa kipindi kirefu.
Chanzo kimeiambia TMZ kuwa Nick ambaye hivi sasa ni meneja wa Amber Rose amekanusha tuhuma hizo na kudai kuwa hajawahi kuchepuka na Amber na hahusiki kivyovyote na uamuzi wake.
Ameeleza kuwa alikuja kufahamu Amber Rose alikuwa na matatizo ya kifamili kupitia mwanasheria wake wiki iliyopita. Nick anasema baada ya kufahamu hivyo wawili hao walianza kushare masimulizi ya kuacha na kuachana.
Vyanzo mbalimbali vinaeleza kuwa Wiz na Amber Rose, kila mmoja anamtuhumu mwenzake kwa michepuko.
Tangu taarifa hizo zilipoanza kusambaa, Amber Rose amekuwa akipost picha na jumbe za ajabu kwenye Instagram na Twitter akionesha mwili wake.
Kwa upande wa Wiz Khalifa amekuwa akitweet jumbe mbalimbali ikiwa ni pamoja na
Everyone deserves to be loved.
Hayo yanajiri wakati ambapo Nick Cannon yuko kwenye wakati mgumu akisubiri uamuzi wa mkewe Mariah Carey kudai talaka kisheria au kurudisha ndoa yao ambayo hivi sasa iko vipande.

MWANAMKE APIGWA RISASI AKIWA KITANDANI NA MUME WAKE MBEYA

MWANAMKE MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA NKUSUBILA KAMINYONGE (70) MKAZI WA MTAA WA KATI SOWETO ALIUAWA KWA KUPIGWA RISASI AINA YA SMG MAENEO YA MKONO WAKE WA KUSHOTO CHINI YA BEGA NA KUPELEKEA KIFO CHAKE.
TUKIO HILO LIMETOKEA USIKU WA KUAMKIA LEO MAJIRA YA SAA 03:00 HUKO MAENEO YA SOWETO, MTAA WA KATI, KATA YA RUANDA, TARAFA YA SISIMBA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA, WATU HAO WALIVUNJA GETI LA NYUMBA NA KISHA KUINGIA NDANI NA KUVUNJA MLANGO WA CHUMBA ALICHOKUWA AMELALA MAREHEMU NA KISHA KUMPIGA RISASI.
WAKATI WATU HAO WANAVAMIA NYUMBA HIYO, MAREHEMU ALIKUWA AMELALA NA MUME WAKE AITWAYE OSIA MALAMBUGI (72) MKAZI WA MTAA WA KATI SOWETO AMBAYE ALISHTUKA BAADA YA KUSIKIA MLIO MKUBWA WA RISASI NA KUKUTA MKE WAKE AMEPIGWA RISASI NA WATU HAO AMBAO WALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO HILO. HAKUNA KITU CHOCHOTE KILICHOCHUKULIWA/KUPORWA. CHANZO CHA MAUAJI HAYO BADO KUFAHAMIKA, UPELELEZI UNAENDELEA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. MSAKO UNAENDELEA KUWATAFUTA WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA WATU HAO WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILO AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.

POMBE ZENYE KEMIKALI MBAYA ZAKAMATWA MBEYA

JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LIMEKAMATA POMBE KALI ZA AINA MBALIMBALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI. POMBE HIZO NI PAMOJA NA BWANA JIN KATONI 05, CHARGER KATONI 03, DOUBLE PUNCH KATONI 02 NA BOSS KATONI 03.
POMBE HIZO ZILIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 23.09.2014 MAJIRA YA SAA 17:00 JIONI HUKO MAENEO YA BWATO, KATA YA IPINDA, TARAFA YA NTEMBELA, WILAYA YA KYELA, MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA ALIKIMBIA MARA BAADA YA KUWAONA ASKARI NA KUTELEKEZA POMBE HIZO, JITIHADA ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.

MAPENZI YAUA MBEYA

Mtu mmoja ambaye amefahamika kwa jina la Hamis Simon aliye na miaka 35 mkazi wa Msanga amekutwa ameuawa kwa kunyongwa shingo na mtu au watu wasiofahamika na kisha kuutelekeza mwili wake kando kando ya mto Msanga.
Mwili wa mtu huyo umekutwa kando ya mto huo juzi asubuhi majira ya saa mbili asubuhi katika kijiji cha cha Msanga kata ya Luhanga tarafa ya Ilongo  katika wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya.
Chanzo cha mauaji hayo kimetajwa kuwa ni wivu wa kimapenzi kwakuwa inasemekana kwamba mke wa marehemu alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanaume mwingine. Mke wa marehemu aitwaye Stelina Petro na mtoto wake aitwaye Magoda Hamis wamekamatwa na jeshi la polisi mkoani Mbeya kwa mahojiano zaidi
Mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi wa kitaalamu na kisha kukabidhiwa kwa ndugu zake kwaajili ya mazishi.

DIALO AMWAGA SIRI ZA LOWASA HADHARANI...AIBU!!!

Diallo anashagaa watu kumwagia sifa Lowasa kuwa ndiye aliyefanikisha kukamilika kwa mafanikio ujenzi wa mradi wa maji wa Ziwa Victoria unaosambaza maji jiji la Mwanza, Shinyanga na Kahama! Diallo anadai kuwa si kweli kuwa ni Lowasa bali ni yeye aliyesimamia mradi huo akiwa Naibu waziri wa Maji na maendeleo ya mifugo! Anaendelea kudai kuwa wakati yeye anasimamia mradi huo Lowasa alikuwa anasimamia DAWASA akiwa Waziri wa Maji na maendeleo ya mifugo!!

Wakiwa ndani ya serikali ya Mkapa, Lowasa akiwa waziri na yeye akiwa naibu waziri, Diallo anadai waligawana majukumu; Lowasa kusimamia DAWASA na yeye kusimamia mradi wa Ziwa Victoria!!
Kwa hiyo Diallo anadai kuwa yeye ndiye anastahili pongezi na sifa za kufanikisha mradi huo na siyo Lowasa!!!
Fichuo Tz inamnukuu...
 Tuhuma za Kundi la Makuwadi wa EL dhidi yangu hayana msingi wowote na kama ni kweli Edward amewapa waziseme kwangu na kuhusisha Mheshimiwa Rais ni mwendelezo wa EL kumdharau Rais ambaye alimpa madaraka makubwa na kosa likiwa kukubali ajiudhuru baada ya kufanya madudu aliyoyafanya. Huu ni mwendelezo wa kumsumbus Rais ambao ulianza tangu 2008 baada ya kujiuzulu uwaziri mkuu. Anayoyasema haya sipendi kuyajibu ila kwa ajili ya kuweka kumbukumbu sawa, imebidi niyajibu lakini nikizingatia kuwa sitaweza kuyajibu yale ninayoyajua chini ya kiapo:
1: Sijamtuma Mzee yeyote kwenda kwa Lowasa kwa sababu sio waziri mkuu tena na hata kama angekuwa bado waziri mkuu nisingeweza kumwambia mtu akaniombee vyeo kwa Lowassa. Hao wazee aliowataja wapo Mwanza na mnaweza kupata namba zao za simu na kuwauliza kama nilishawahi kufanya hivyo. Pili, mwaka 2003/4 haukuwa mwaka wa uchaguzi, ilikuwaje niende kuomba cheo wakati niliingia baraza la Mhe. Rais Mkapa 2001? Wakati huo Lowassa hakuwa waziri mkuu! Tatu, mwaka 2004 sijaonana na JK na Karamagi hajanishawishi kumuunga mkono JK mwaka 2005.

Mimi ndiye niliyetumwa kumwambia Lowassa asigombee 2005 kwavile dhambi na tuhuma dhidi yake zilizotolewa na Mwalimu zilikuwa kwenye mioyo ya watanzania na asingeweza kupata kura za ushindi isipokuwa angempunguzia JK kura zake na wote kukosa. Karamagi tumekutana naye bungeni baada ya kuchaguliwa ubunge baada ya kifo cha Mhe. Kinyondo. Mimi nimezaliwa na kukua kwa kuzingatia nidhamu ya Kisukuma, sijalelewa kihuni kufika kumsema mtu kama JK.

Namsema EL kwa sababu ni mchafu, na sasa sitayasema yaliyo mazito au machafu zaidi dhidi yake, hadi nitakapoona kweli kachukua fomu kugombea Urais! Mimi sijasema Lowassa alidhulumu CCM kupata hisa Vodacom, nilichosema CCM ilikuwa iwe mbia wa MTN, kampuni iliyonyimwa leseni wakijua fika kuwa ilikuwa ikisaidie chama, badala yake wakafanya njama kuvunja tume ya mawasiliano kihuni, na hapohapo wakaipatia vodacom leseni lowasa kwa kutumia watoto wake, alipata walikipata. Ushahidi kuhusu hili ni kampuni yake kupewa U-Super Dealer wa Vodacom ambayo uliwafanya wanufaike kwa kuuza simu nchi nzima.

Kama wanasema Lowassa ni mzima, naomba akakimbie uwanja wa Taifa azunguke hata mara moja kama hataishia ICU. Na kama ni mzima, anatumia fedha za nchi kwenda kutibiwa nini ujerumani kila wakati au Ujerumani nako siku hizi kuna waganga wa kienyeji? Pili kwanini alikwenda kuombewa kwa Emmanuel Ministries huko Nigeria? Kampeni za Urais zinahitaji afya nzuri, sio mzaha kuweka mgonjwa akatufia kwenye jukwaa! Kuhusu tuhuma ya rushwa toka kwa Kimaro, nina hakika Kimaro bado yupo hai, na kama ni mkweli aseme ukweli.

Kimaro ni rafiki yangu na nilimshawishi akawekeza hoteli ya Nyumbani sasa ni JB Belmonte, Mwanza. Sijachukua fedha ili nimpatie kitalu kwavile yeye sio mwindaji na sijasikia kuwa ana hiyo biashara. Ninachofahamu ana mahoteli na ndiyo biashara yake. Rais yupo kama alishaniita kunieleza hilo anaweza akasema, ni mkweli. Tuhuma za mimi kuhongwa na Kimaro alizianzisha Lowassa baada ya mimi kutaka kumuondoa Mkurugenzi wanyama pori wizara ya Maliasili.

Mkurugenzi huyo alikuwa na mahusiano naye na baadae walikuja kuoza watoto wao. Hilo kila mtanzania analifahamu, na alimtetea sana abaki wizarani wakati huo. Lowassa yupo kwenye mtandao wa yote yanayosemwa kuhusu wanyama pori. Pia tuhuma za kumtapeli aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Mhe Karume ndio nazisikia leo. Karume sijafika nyumbani kwake Zanzibar na wala hata alipokuwa Ikulu Zanzibar. Yupo na anaweza kuulizwa, ni mkweli atasema yaliyo kweli.

Huyo msichana anayesemekana nilimpa mimba, mhudumu wa Dodoma hotel, ndiyo namsikia leo, na kama yupo aniletee mtoto huyo kwani ndio nasikia kwenye watu wa Lowassa baada ya kuweweseka na machache tu tuliyoyaweka hadharani. Mwisho la kupewa fedha na mtuhumiwa wa IPTL nalo jipya simfahamu, labda Lowassa anamfahamu! Tatizo la huyu Lowassa, ni kupata URAIS, asipoupata sijui kama atabaki na afya ya kuridhisha. Anatuhumu watu tusiounga mkono jitihada zake tu, je wanaogombea watakuwa na hali gani mbele yake? Ushauri wa bure kwa wapambe wa Lowassa: Kuleni fedha yake maana ni halali yenu, fedha za kukwapua kwa njia zisizo halali ni haki ya kila mtu kuzitafuna, ila Urais hatopata.Kidumu Ccm.