Jumatano, Septemba 24, 2014

MAPENZI YAUA MBEYA

Mtu mmoja ambaye amefahamika kwa jina la Hamis Simon aliye na miaka 35 mkazi wa Msanga amekutwa ameuawa kwa kunyongwa shingo na mtu au watu wasiofahamika na kisha kuutelekeza mwili wake kando kando ya mto Msanga.
Mwili wa mtu huyo umekutwa kando ya mto huo juzi asubuhi majira ya saa mbili asubuhi katika kijiji cha cha Msanga kata ya Luhanga tarafa ya Ilongo  katika wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya.
Chanzo cha mauaji hayo kimetajwa kuwa ni wivu wa kimapenzi kwakuwa inasemekana kwamba mke wa marehemu alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanaume mwingine. Mke wa marehemu aitwaye Stelina Petro na mtoto wake aitwaye Magoda Hamis wamekamatwa na jeshi la polisi mkoani Mbeya kwa mahojiano zaidi
Mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi wa kitaalamu na kisha kukabidhiwa kwa ndugu zake kwaajili ya mazishi.

0 comments:

Chapisha Maoni