HABARI KWA WAKATI KUTOKA HAPA

Tunakuhakikishia kupata habari zote zilizo muhimu kutoka ulimwenguni kote kwa wakati, unaweza kusubscribe mtandao wetu na ukawa unapokea habari zote katika email yako punde tu tuchapishapo machapisho yetu. Jiunge na mitandao yetu ya Facebook na Twitter kutupata kirahisi.

HABARI ZA MICHEZO

Sasa Fichuo tunakuhakikishia kupata taarifa zote za kimichezo kutoka viwanja mbalimbali duniani, lengo ni kuhakikisha hupitwi na lolote katika ulimwengu wa michezo.Jiunge na mitandao yetu ya Facebook na Twitter kutupata kirahisi.

TAARIFA ZA BURUDANI NA HABARI ZA WASANII

Unapenda masuala ya burudani? Ni jukumu letu kuhakikisha unazipata info zote za burudani na wasanii wanaokupa burudani, unapata video mpya, movie pamoja na muziki. Kaa karibu nasi.

KURASA ZA MAGAZETI KILA SIKU

Tunakupatia kila ambacho kinaandikwa katika magazeti ya Tanzania na nje ya Tanzania, usitie shaka ukishindwa kununua gazeti uipendalo, sogea karibu nasi na upate kila unachokihitaji.

MAHUSIANO

Fahamu mambo mengi katika ulimwengu wa mapenzi kwa kupitia dondoo, simulizi na visa mbalimbali kupitia Fichuo Online, Jiunge na mitandao yetu ya Facebook na Twitter kutupata kirahisi.

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo BURUDANI. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo BURUDANI. Onyesha machapisho yote

Jumatatu, Februari 26, 2018

UTAMADUNI WA KUCHEZA UTUPU MSIBANI CHINA UNAZIDI KUSHIKA KASI

Muziki unacheza kwa sauti, wacheza utupu wakicheza densi na umati ukishangilia. Katika sehemu zingine huko China hili ndilo unaweza kuliona wakati wa mazishi.
Mapema mwaka huu, China alianza tena kuwakamata wacheza utupu wanaocheza densi kwenye mazishi, harusi na kwenye mahekalu.
Hio sio mara ya kwanza mamlaka zimejaribu kuzuia tabia hizo lakini bado hazijanafikiwa

Related image

Mbona watu huwaajiri wacheza utupu?

Wacheza utupu hutumiwa kuwavutia watu wnaaohudhuria mazishi kwa sababu uwepo wa watu wengi kwenye mazishi huonekana kama heshima kwa marehemu. Imani nyingine zinasema kuwa suala hilo na la kuabudu.
Imani nyingi ni ile kuwa kuwaajiri wacheza utupu kunaweza kuonekana kama ishara ya utajiri.
Maeneo ya vijijini nchini China ndiyo yenya tabia ya kutumia pesa nyingi hata kuliko mapata, kuwalipa wuigizaji, waimbaji, wachekeshaji na wacheza utupu kuwatumbuiza wale waliofiwa.

Image result for Pole dancers ON FUNERALS

Shughuli hii ni maarufu?

Tamaduni hiyo inapatikana sana maeneo ya vijijini ya China na ni maarufu zaidi nchini Taiwan ambapo ilianzia.
"Tamaduni hii ya wacheza utupu kwenye mazishi kwanza lilipata umaarufu nchini Taiwan mwaka 1980," msomi wa chuo cha South Carolina Marc Moskowitz aliiambia BBC.
Tamaduni hii imepata umaarufu nchini Taiwan lakini nchini China serikali imeizuia na watu wengi hawafahamu kuihusu.


BBC

Jumatano, Februari 21, 2018

UNASUMBUKA NA HANGOVER? TUMIA NJIA HII KUIMALIZA. TIBA!!!

Inawezekana wewe ni kati ya watu wanaopenda kupiga vyombo (Pombe) kwa kiasi kikubwa, inawezekana ni starehe yako lakini unakerwa sana na hali unayoamka nayo asubuhi, hangover, wengine kwa kiswahili kisicho rasmi sana wanaita mnng'inio na umekuwa ukipata taabu sana kuimaliza hiyo hali pengine kwa kunywa mchemsho au kutoa lock angalau kwa kunywa tena pombe kidogo.
Pamoja na njia zote uzitumiazo kumaliza hiyo hali ya mning'inio, Fichuo leo inakupatia tiba halisi, rahisi na ya asili ya kukuondolea hangover.
Kuna mchanganyiko wa kinywaji-lishe unaitwa BANANA MILKSHAKE, hiki ni kinywaji-lishe kinachotengenezwa kwa mchanganyiko wa maziwa fresh, ndizi mbivu pamoja na asali. Ukipata kinywaji-lishe hiki angalau kikombe/glasi moja katika asubuhi uliyoamka na hangover itaamsha nguvu zako na kutoa uchovu unaokupatia usumbufu.
Kwanini hii ni tiba? Kwakuwa ndizi mbivu husaidia kutuliza tumbo na kumaliza kilevi lichosalia mwilini wakati asali kazi yake ni kusawazisha na kujenga viwango vya sukari iliyoharibika mwilini.
Maziwa yenyewe tunafahamu kwamba yana vitamins zenye msaada mkubwa katika mwili wa binadamu, ambazo ni A, D, E na K

BANANA MILKSHAKE inatengenezwaje? Jifunze hapa;

Katika kutengeneza BANANA MILKSHAKE utahitaji kuwa na maziwa mabichi angalau lita moja, ndizi mbivu kubwa 2 au ndizi kisukari 4 (ndizi mbivu ndogondogo) na asali angalau vijiko vitatu vya chai. (japo hapa pia inategemeana na kiasi cha uzito na ladha uitakayo katika kinywaji-lishe chako.
Chemsha maziwa vizuri kisha wacha yapoe kabisa, kisha yatie katika brenda na uchanganye na ndizi pamoja na asali na ukoroge pamoja. baada ya hapo unaweza kutia katika friji ili upate kiwango cha ubaridi utakaoutaka haraka. Baada ya hapo inakuwa tayari kwa matumizi. Ikikusaidia saidi na wengine kama Fichuo ilivyokusaidia.

Burudika kidogo na wimbo Hangover toka kwa PSY na SNOOP

Jumatano, Mei 17, 2017

MSANII DOGO MFAUME WA KAZI YA DUKANI AFARIKI DUNIA

Msanii wa Bongo Fleva, Mfaume Selemani ‘Dogo Mfaume’, aliyetamba zaidi na wimbo wake wa Kazi ya Dukani amefariki dunia leo.
Dogo Mfaume alikuwa Sober House (alikuwa akipata matibabu ya Matumizi ya Madawa ya Kulevya)
Marehemu alikuwa amepangiwa kufanya Operation ya Kichwa (ambapo alikuwa na Uvimbe) siku ya Ijumaa.

Ijumaa, Mei 12, 2017

THE ROCK ANAUTAKA URAIS WA MAREKANI 2021

Aliyekuwa nyota wa mchezo wa miereka Marekani Dwayne Johnson maarufu 'The Rock' anataka kuwania urais nchini humo.
Katika mahojiano na jarida la GQ, nyota huyo wa uigizaji anasema kuwa amelifikiria sana wazo hilo.
Anasema kwamba iwapo angekuwa rais ingekuwa muhimu.
''Uongozi ni muhimu. Kuchukua jukumu la kila mtu''.
Lakini Johnson sio nyota pekee mwenye maono ya kutaka kuhamia katika ikulu ya Whitehouse 2021.
Mark Zuckerberg , bilionea na mkurugenzi wa mtandao wa facebook pia huenda ana ndoto kama hiyo.
Amekuwa na mpango wa kuwatembelea raia wote wa Marekani katika majimbo 50 na amekuwa akipeperusha hewani ziara zake moja kwa moja katika mtandao wa facebook hatua ambayo inaokena kuupigia debe mtandao huo.

Jumatatu, Mei 08, 2017

UFARANSA YAZUIA WANAMITINDO WEMBAMBA/WASIO NA AFYA

Sheria nchini Ufaransa inayopiga marufuku wanamitindo wembamba wasio na afya imeanza kutekelezwa.
Wanamitindo watahitajika kuwa na cheti cha daktari kuonyesha afya yao kwa misingi ya vipimo vya uzito wao na kimo.
Wizara ya afya inasema kuwa inataka kukabiliana na matatizo ya kutokula na viwango visivyofikiwa vya urembo.
Pia picha za wanamitindo zilizofanyiwq ukarabati zitahitaji kutajwa.
Mswada wa awali ulikuwa umependekeza uzito na kimo cha wanamitindo hatua iliyopingwa vikali na mashirika ya urembo nchini Ufaransa.
Lakini aina tofati ya mswada ulioungwa mkono na wabunge mwaka 2015 unawaruhsuas madaktari kuamua ikiwa mwamitindo ni mwembamba mno kuambatana na uzito wake umri na mwili.
Waajiri wanaovunja sheria hiyo watapigwa faini ya hadi dola 82,000 au kifungo cha miezi sita jela.
Ufaransa sio nchi ya kwanza kuweka sheria inayohusu wanamitindo wembamba- Italia, Uhispania na Israel washafanya hivyo.

Jumatatu, Aprili 17, 2017

MOVIE YA FATE OF THE FURIOUS YAVUNJA REKODI YA DUNIA

Filamu ya Fate of the Furious imevunja rekodi ya dunia ya kuwa filamu iliyouzwa sana baada ya kuzinduliwa rasmi.
Filamu hiyo, ambayo ni ya nane katika mwendelezo wa filamu za Fast & Furious, ilipata mauzo ya jumla ya $532.5m (£424.7m) duniani wikendi ya Pasaka.
Hayo ndiyo mauzo ya juu zaidi duniani kwa filamu yoyote siku zake za kwanza baada ya kuzinduliwa rasmi.

Filamu hiyo imepita mauzo ya $529m (£421.8m) rekodi ya awali iliyowekwa na Star Wars: The Force Awakens.
Mauzo hayo ya filamu hiyo nchini Marekani hata hivyo yalikuwa chini ukilinganisha na mauzo ya filamu iliyotangulia.
Furious 7 ilipata mauzo ya $147.2m (£117.3m) nchini Marekani ilipozinduliwa 2015.
Lakini filamu ya sasa imezoa $100.2m (£80m) pekee.
Licha ya kushuka kwa mauzo yake Marekani, filamu hiyo bado ilichangia sehemu kubwa ya mauzo ya filamu Marekani, ambapo ilichangia karibu theluthi mbili.
Mshindani wake wa karibu alikuwa The Boss Baby, ambayo iliuza $15.5m na kuwa ya pili.
Filamu za Fast & Furious zilianza kuuzwa 2001.
Ufanisi wa filamu hii ya sasa ulichangiwa sana na China ambapo mauzo yake yalikuwa $190m (£151m) kwa siku hizo tatu.
Vin Diesel, ambaye ameigiza katika kila filamu ya Fast & Furious amesema anashukuru sana na amefurahishwa sana na ufanisi wa filamu hiyo.
Wengine walioigiza katika Fate of the Furious ni Charlize Theron, Tyrese Gibson na Ludacris.
Filamu nyingine za Furious zitatolewa mwaka 2019 na 2021.

ALIYEMCHEZA JAMES BOND AFARIKI DUNIA

Mwigizaji Clifton James, aliyeigiza kama Liwali JW Pepper kwenye filamu mbili za James Bond, amefariki dunia akiwa na miaka 96.
Alifariki karibu na mji wake aliokulia wa Gladstone, Oregon, siku ya Jumamosi kutokana na matatizo ya ugonjwa wa kisukari.
James alifahamika sana kutokana na uigizaji wake pamoja na Sir Roger Moore katika filamu za Bonds za Live and Let Die na The Man with the Golden Gun miaka ya sabini.
Binti yake Lynn amesema: ''Alikuwa mtu mpenda watu na mwenye uwazi sana. Alipendwa sana na kila mtu.''
Aliongeza: "Sidhani alikuwa na adui hata mmoja. Kwa kweli tulibarikiwa kuwa na yeye maishani."

Jumanne, Aprili 04, 2017

WEMA SEPETU KUSHINE KATIKA JARIDA LA KENYA 'TRUE LOVE'

Safari yake ilianza rasmi mwaka 2006 alipojitwalia taji la Miss Tanzania, akaendelea kujenga jina lake taratibu alipoingizwa rasmi katika ulimwengu wa filamu Tanzania na marehemu Steven Kanumba, akaendelea kukaa katika kilele cha ustaa kwa miaka 10 kutokana na kufanya mambo mengi yaliyovutia watanzania wengi kupitia kampuni yake ya Endless Fame, na hata kuingia katika siasa ndani ya CCM. 
Sasa anaendelea kukaa kwenye vichwa vya watu baada ya kuingia katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kama haitoshi hivi karibuni tutamuona katika jarida kubwa kutoka nchini Kenya la TRUE LOVE! Anaitwa Wema Abraham Sepetu.
Katika ukurasa maaumu wa instagram wa jarida hilo waliyaandika haya:
This month Tanzania’s Sweetheart, the gorgeous @wemasepetu graces our cover. She opens up about Money, Men, Love and Loss. Be sure to grab a copy to see what she has been up to and also read about Easter plans and gateways. Happy new month’- True Love Magazine East Africa

Jumatatu, Aprili 03, 2017

WALICHOKIZUNGUMZA NEY WA MITEGO NA MWAKYEMBE HIKI HAPA

Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, hatimaye amerejea kutoka Makao Makuu ya nchi mjini Dodoma, ambapo alienda kuitikia wito wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison George Mwakyembe.
Hivi karibuni Nay alishikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kuachia Wimbo wa Wapo uliokuwa na mashairi ya kuilenga serikali lakini baada ya siku chache Waziri Mwakyembe alitoa agizo la kuachiwa msanii huyo na wimbo huo kupigwa baada ya kusikilizwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli na kufurahishwa nao.

Baada ya Jeshi la Polisi kumuachia Nay, waziri alimuomba kufika Dodoma kukutana naye na kuzungumza mengi kuhusiana na sanaa. Over Ze Weekend limekuchambulia alichoambiwa;
“Nimeshaonana na Waziri Mwakyembe, kufuatia wito wake, ambapo nilifika hadi kwenye ofisi zake na tuliongea mambo mengi ikiwemo yeye kuniulizia kwa makini tungo yangu hiyo ambayo kwa kiasi kikubwa katika maongezi yetu alionekana akisifia sana kazi zangu.
“Kubwa zaidi aliloniambia yaani ikiwa pamoja na kunielezea dhamira ya Rais Magufuli, kuachia huru wimbo wangu, baada ya kuusikiliza kwa makini na kubaini hauna dosari ya kuufanya ufungiwe na mimi kunitia hatiani kama ilivyokuwa imechukuliwa na Jeshi la Polisi ambao waliniweka hadi rumande.
“Mwakyembe alisema kuwa rais amesikia wimbo wangu na kufurahishwa na mawazo yangu hivyo akaamua kumuagiza Over aniachie huru na wimbo uendelee kupigwa, ila aliomba kama kuna uwezekano nitunge wimbo mwingine ambao nitazungumzia mambo mengi ya kijamii ikiwa ni pamoja na juhudi za serikali.
“Zaidi alisema kuwa kama kuna uwezekano itabidi huu wimbo nifanye remix yake ambayo itanifanya niongeze mistari yenye kuzungumzia janga la madawa ya kulevya, wakwepa kodi na hata wale wote ambao wamekuwa wakipinga harakati za kiuchumi ikiwa sambamba na kuhujumu uchumi wetu.
“Waziri Mwakyembe, amenitaka pia niwe makini zaidi katika kazi yangu kwani nyimbo ambazo nimekuwa nikiimba hakika zimekuwa zikigusa moja kwa moja hisia za watu, jambo ambalo wengine wenye mioyo isiyokuwa na uvumilivu ni rahisi kushindwa kunivumilia na kujikuta wakitaka kunizuru moja kwa moja.
“Hakika nimefurahia ushauri wake na wawatu wengine kwani nikiwa katika ofisi zake niliweza kuongea pia na Naibu Waziri wa Kazi Vijana na Ajira, Anthony Mavunde, ambaye pia aliniambia amekuwa akiheshimu na kuvutiwa sana na kazi zangu, hivyo naye kwa pamoja aliniambia niongeze umakini hasa kwenye tungo zangu ili siku moja zisiweze kuniingiza kwenye mitafaruku na watu.
“Kusema kweli wito wa Mwakyembe ulikuwa ni mzuri sana kwani umenipa mafunzo makubwa ya namna ya kuongeza ubunifu katika sanaa yangu, ila pia nimeweza kujifunza na kuwajua watu ambao sisi wasanii tumekuwa tukiwafikiria kama si wafuatiliaji wa kazi zetu, kumbe wao ndiyo wanasikiliza mstari kwa mstari.
“Nasema hivi kwa sababu wakati naongea na Mwakyembe alinigusia mistari kibao ya nyimbo zangu hata zile za nyuma jambo lililonishangaza na kunishitua kwani sikuwahi kutegemea kama angekuwa mfuatiliaji wa sanaa yetu kiasi cha kujua kila jambo, maana mimi hata kipindi anateuliwa nilikuwa namuona kama hataweza kusimamia kazi zetu kwa kuamini hajui chochote kwenye sanaa, kumbe sivyo hivyo.
“Nichukue nafasi hii kumpongeza Rais Magufuli kwa wema wake alionionyesha, kwani amenijenga kwa kiasi kikubwa na kwamba nimefarijika kusikia akiusifia sana wimbo wangu kwani ni jambo linalotia moyo sana, nitumie fursa hii pia kumpongeza Mwakyembe kwa kunionyesha kuwa anaitambua sanaa na anajua kila kitu kwenye tasnia hii, jambo ambalo naamini kupitia yeye tutazidi kunufaika na kazi zetu za muziki ambazo wengi wetu ndiyo ajira tulizojianzishia,”
“Hakika kupitia wimbo wangu huu nimepata elimu ambayo nitahakikisha naifikisha kwa Watanzania walio wengi ili siku moja niweze kuisaidia serikali yangu kuelimisha mambo muhimu ambayo kwa namna moja au nyingine huko nyuma sikujua kama serikali iko karibu na wasanii namna hii,” 
alisema Nay.

Jumapili, Aprili 02, 2017

MR EAZI ALIYESHIRIKISHWA NA BEN POL KATIKA 'PHONE' SASA AMELETA YA KWAKE HII 'FIGHT' +VIDEO

Anafahamika kama Mr Eazi katika katika ulimwengu wa muziki, lakini jina lake halisi ni Oluwatosin Oluwole Ajibade, mzaliwa wa Port Harcourt, nchini Nigeria, umri wake ni miaka 28 na tayari ametoa albam ambayo ni Life Is Eazi: Accra to Lagos. Sisi watanzania tulimfahamu kupitia wimbo alioshirikishwa na Mwanamuziki staa wa RnB Ben Pol katika 'Phone'.
Sasa Mr Eazi katuletea wimbo mpya unaitwa 'Fight' na hapa kashirikiana na Dj Cuppy mwenyeji wa Nigeria, mwanamke mwenye miaka 24 ambaye ni maarufu zaidi kwa kucheza na mashine yaani DJ

Jumamosi, Aprili 01, 2017

YAMOTO BAND-BASI MP3

Kutoka jiko la WCB (Wasafi Classic Baby) mpishi mkali wa muziki mzuri producer Laizer katupikia hii kutoka kwa vijana washereheshaji Yamoto Band, hii ni baada ya maneno mengi kuwa vijana hao wanne wameteekezwa na ni ngumu kuwaona tena katika anga la muziki wa bongo fleva kama walivyokuwa wakitesa awali..wimbo wao mpya katika mahadhi yao huu hapa

NEW TRACK: RAPPER DARASSA AMERUDI NA 'UTANITOA ROHO' IPATE HAPA

Rapper aliyefanikiwa kuumaliza mwaka 2016 vizuri na kuuanza mwaka 2017 kwa nguvu kubwa ya wimbo 'Muziki', Darassa amerudi tena na wimbo mwingine, na hapa katika track yake mpya kaimbia mapenzi akinakshi mistari yake na maneno kutoka kwenye wimbo wa zamani wa dansi.
Darassa aliyewahi kufanya vizuri na wimbo mwingine wa mapenzi 'Kama Utanipenda' inasemekana wimbo huu mpya anaohofia kutolewa roho haujatoka kwa ridhaa yake, ni kama umevuja wakati akiwa kwenye mipango ya kuutangaza rasmi.
Japo kuwa unaweza kusema ni aina ya 'Kick' ameitengeneza ili kurudi kuendeleza ufalme wa 'Muziki' ulioanza kufifia hivi karibuni, lakini kwa aina ya wimbo huu mpya hakika ataendelea kuwa katika vichwa vya wapenzi wengi wa muziki.

Alhamisi, Machi 30, 2017

BAADA YA KANDANDA, RONALDINHO SASA KATIKA MUZIKI, TRACK YAKE IKO HAPA +AUDIO

Staa wa soka na mkongwe wa Klabu ya Barcelona na Timu ya Taifa ya Brazil, Ronaldinho Gaucho ameamua kujitosa kwenye tasnia ya muziki ambapo ameachia wimbo wake wa kwanza alioupa jina la Sozinho.
Wimbo aliouachia Ronaldinho ni wa staili laini Kibrazili ya Samba na tafsri ya Sozinho kwa Kiingereza ni ‘Alone’
Hii sio mara ya kwanza kwa Gaucho kufanya kazi ya muziki, mwaka jana alipata nafasi ya kuimba kwenye mashindano ya Rio Paralympics 2016. 
Licha ya kuachia ngoma hiyo, Gaucho amesema: ‘Asanteni marafiki zangu. Huu ni wimbo wangu wa kwanza, bila kumshirikisha mtu yeyote!!!’
Licha ya kustaafu kucheza soka la ushindani mwaka 2015, Staa huyo wa Samba mwenye umri wa miaka 37 amekuwa akijishughulisha na kazi mbalimbali zikiwemo za muziki.

Jumatatu, Machi 27, 2017

NEY WA MITEGO AACHIWA KUTOKA MIKONONI MWA JESHI LA POLISI, NI KWA AMRI YA RAIS

Mwanamuziki Emmanuel Elibariki a.k.a Nay wa Mitego, ambaye alikuwa amekamatwa na jeshi la polisi Tanzania kuhusiana na wimbo wake, ameachiliwa huru.
Wa Mitego ameachiliwa huru saa chache baada ya Waziri wa Habari nchini Tanzania Dkt Harrison Mwakyembe kuagiza aachiliwe huru.
"Saa hizi sina kubwa la kuongea. Wimbo umeruhusiwa. Nashukuru. Nafurahi kusikia taarifa ya serikali kwamba wameruhuru wa Wapo upigwe. Upigwe kwa nguvu," amesema Wa Mitego baada ya kuachiliwa huru.
Kuhusu kuuboresha wimbo huo, amesema: "Hili nitalifanyia kazi. Siwezi kusema saa hizi ni vitu gani kwa sababu ndio nimetoka huko. Lakini nitalifanyia kazi kwa sababu tayari ni wimbo wa kila mtu, wimbo wa Watanzania, wimbo wa watu wote."
Dkt Mwakyembe hata hivyo alimtaka Nay wa Mitego auboreshe zaidi wimbo wake, kwa mujibu wa ujumbe uliopakiwa katika ukurasa Rasmi wa Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania kwenye Twitter.
Sehemu ya maudhui ya wimbo huo inagusia tuhuma za kughushi vyeti ambazo zimekuwa zikigonga vichwa vya habari nchini Tanzania
Wimbo huo mpya wa Ney wa Mitego, ulianza kusambaa katika mitandao ya kijamii wiki iliyopita.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Ulrich Matei alikuwa amesema mwanamuziki huyo alikamatwa kwa kosa la kutoa wimbo wenye maneno ya kashfa dhidi ya serikali.
Mwanamuziki Ney wa Mitego akamatwa Tanzania
Magufuli ayaonya magazeti Tanzania
Mapema leo, Baraza la Sanaa la Taifa Tanzania (Basata), lilikuwa limetangaza kuufungia wimbo huo kwa jina Wapo usichezwe kwenye vyombo vya habari au kutumika kwa namna yoyote ile.
"Basata linawakumbusha wasanii na wadau wote wa kazi za sanaa kuzingatia ubunifu wa hali ya juu kufanya kazi za sanaa, hata kufikisha ujumbe mbalimbali wa kufundisha, kuelimisha, kuburudisha na hata kuonya," taarifa kutoka kwa baraza hilo ilisema.
Wa Mitego baada ya kuachiliwa huru
"Baraza linawaonya wale wote wanaotumia kazi zilizopigwa marufuku, ikumbukwe kuwa kutumia kazi zilizopigwa marufuku ni ukiukwaji wa sheria za nchi (na) hatua kali zitachukuliwa juu yao."
Awali kulikuwa na taarifa kwenye vyombo vya habari kwamba Rais wa Tanzania John Magufuli alikuwa ameagiza wimbo huo uendelee kuchezwa.

Kiongozi wa upinzani kutoka chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe hata hivyo alionekana kukerwa na taarifa hizo.
Bw Kabwe alisema Rais hana mamlaka yoyote ya kuamua wimbo uchezwe au usichwezwe.
"Ilikuwa ni makosa kumkamata Nay na agizo la Rais halina maana pia," aliandika kwenye Twitter.

RAIS MAGUFULI AMEAMURU NAY WA MITEGO AACHIWE NA KUTAKA WIMBO WAKE 'WAPO' UENDELEE KUPIGWA NCHINI

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, ameliagiza Jeshi la Polisi kumuachia huru Msanii Ney wa Mitego aliyekuwa akishikiliwa na Jeshi hilo.
Waziri Mwakyembe ameishauri pia BASATA kuondoa zuio lake dhidi ya wimbo huo, na badala yake uendelee kupigwa tu kama nyimbo nyingine.
Akiongea na Wandishi wa Habari muda huu mjini Dodoma, Dk. Mwakyembe amesema hata Rais Magufuli amefurahishwa na wimbo huo wa WAPO, na kumshauri Msanii huyo kama inawezekana aendelee kutaja watu wengine kama vile Wakwepa Kodi, Wauza Unga, Wabwia Unga, Wezi pamoja na watu wengine wasio na maadili mema katika jamii.

Jumapili, Machi 26, 2017

MWANAMITINDO ALIYEUGUA 'UGONJWA WA PAKA'

Mwanamitindo Caitin Stickels ana tatizo nadra sana la kiafya ambalo hufahamika kama 'Ugonjwa wa macho ya paka' ambalo humsababishia maumivu makali sana.
Lakini bado hajakata tamaa.
Tatizo hilo la kiafya humfanya aonekane kama paka.
Hali yake ilimvutia mpiga picha za mitindo kutoka Uingereza Nick Knight.
Alimtazama mwanamitindo huyo wa miaka 29 kutoka Seattle mara ya kwanza kwenye Instagram.
Tangu wakati huo, amevuma kama mwanamitindo na hata picha zake zikachapishwa katika jarida la V Magazine.
"Ni mabadiliko makubwa zaidi mema yaliyowahi kutokea katika maisha yangu," aliambia BBC.
Ugonjwa huo wa macho ya paka hufahamika kitaalamu kama Schmid-Fraccaro Syndrome.
Watu wenye ugonjwa huo wanaweza kuwa na matatizo katika maumbile ya masikio yao, moyo na kwenye figo.
Wakati mwingine, viungo vingine mwilini huathiriwa.
Sura ya Caitin si kama ya wanamitindo wengi ambao wamevuma sana.
'Urembo' wake si kama ule wengi waliozoea kuona ukiangaziwa kwenye majarida, filamu na runinga.
"Sikuwahi kuwa na ndoto ya kuwa mwanamitindo au kufikiria ningeshiriki katika tasnia ya mitindo na mavazi,"
"Mahangaiko mengi kwangu kutokana na ugonjwa huu huwa ni ndani ya moyo wangu," anasema.
"Nafikiri jambo jingine ni kwamba macho yangu huwa hawayumbuki kivyake; na hivyo hukaa kama ya paka wakati wote.
"Hii hata hivyo huniwezesha kuona vyema usiku, ninaweza nikatatizwa na jua kali. Nalipenda jua na mara nyingi hutokea nje na kutembea, lakini hilo hutatiza macho yangu."
Caitin anasema pia hupata maumivu makali mwilini na kupata kichefuchefu.
"Mwili wangu huathiriwa sana na mabadiliko katika mazingira, lakini kwa sababu umekuwa hivyo kwa muda mrefu, watu wengi niliotangamana nao huwa hawatambui kwamba kuna tatizo. Mimi ni mgumu kama jiwe."
"Kazi yangu ya uanamitindo, uigizaji na uimbaji hunisaidia sana kusahau maumivu niliyo nayo moyoni.
"Ni figo moja pekee yangu inayofanya kazi, kwa hivyo huwa inanibidi kunywa maji sana.
"Na sura yangu? Watoto wakati mwingine ndio hunishangaa. Lakini sana huwa sikabiliwi na unyanyapaa.
"Utoto wangu ulikuwa vile vile. Watoto ni watoto tu, ni kweli walinicheka na kunichezea. Lakini nani hakufanyiwa hivyo?"
"Sote huwa na kasoro pahala fulani na sote ni watu binafsi. Hakuna aliyekamilika," anaongeza.
"Jambo moja ni kwamba sote hatufanani na hakuna asiye na doa pahali."

BBC

NAY WA MITEGO KAKAMATWA NA POLISI MOROGORO ASUBUHI YA LEO, SABABU NI #WAPO?

Siku chache baada ya mwanamuziki Nay wa Mitego kutoa single yake mpya kwa jina la WAPO, wimbo ambao amesikika akipasuka uhalisia wa mambo yanayoendelea nchini, asubuhi ya leo taarifa kutoka mkoani Morogoro zinaeleza kuwa mbongo fleva huyo anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani humo pasipo sababu ya msingi kufahamika mara moja
Japokuwa inahisiwa kuwa kilichompelekea kushikiliwa ni suala la aina ya maneno aliyoyatumia katika wimbo wake, wapenzi na wadau wengi wa muziki wa bngo fleva wamehoji juu ya uhalali wa jeshi hilo kumshikilia Nay wakati wapo BASATA wenye mamlaka ya kufuatilia shughuli zote za wasanii Tanzania.(iwapo sababu ni wimbo #Bado)
Mwenyewe kupidia Instagram, Nay amethibitisha kukamatwa kwake:
Nimekamatwa kweli. Muda Huu nikiwa hotel Morogoro baada ya kumaliza Kazi yangu iliyo ni leta. Napelekwa Mvomelo Police.
Nawapenda Watanzania wote.
✊🏿✊🏿 #Truth
#Wapo

Jumamosi, Machi 25, 2017

ZIFAHAMU MBIO ZA 'DAREDEVIL'

Picha hizi zinaonyesha zaidi ya wanaume 2,500 ambao walishiriki katika mbio maarufu kama "Daredevil" za mwaka 2017 mjini Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Ijumaa (jana) wakati tukio la misaada lilianza katika miji mitatu nchini humo: mji wa Cape Town,Durban na Nelspruit siku hiyo hiyo.
Katika tukio hilo waandalizi wanajaribu kuongeza uelewa wa umma wa kuzuia saratani kupitia mipango y kilomita 5 na wanaamini kwamba kuzuia ni rahisi kuliko tiba.

VIDEO MPYA: LADY JAYDEE NA H_ART THE BAND KUTOKA KENYA WAMEKUJA NA 'ROSELLA'

Kwenye zile zinazotrend wekeend hii kutoka East Africa ni pamoja na hii ya H_Art The Band kutoka Kenya na Malkia wa Bongo Fleva Lady JayDee.
H_Art The Band kutoka Kenya na Lady JayDee wameshirikiana kutuletea wimbo wao mpya ‘Rosella’ ambayo video yake imeongoza na Kevin Bosco Jnr.
‘Rosella’ ni wimbo unaosimulia stori  ya mapenzi kati ya watu wawili waliobaki njia panda. Akiwa muoga wa kueleza hisia zake, Rosella anabaki kuumia akitamani yule ampendaye ajue kile kilichopo moyoni mwake, akiendelea kujiuliza kama kweli jamaa kabadilika… Lakini hata kama angekuwa na ujasiri wa kufanya hivyo, mwanaume huyo ana sababu zinazomfanya afikirie tofauti na pengine kujuta na kukata tamaa juu ya penzi hilo licha ya kuwa bado anampenda sana mrembo huyo.
Watazame na sikiliza stori za pande zote mbili kwenye hizi dakika tano hapa chini.

Ijumaa, Machi 24, 2017

DIAMOND, BELLE 9 NA SAIDA CAROLI KUJA NA ALBUM MOJA

WASANII wa Muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ na Abednego Damian ‘Belle9’ wamembeba msanii mwenzao anayeimba nyimbo za asili, Saida Kalori kwa kushiriki katika albamu yake itakayoitwa Naamka.
Saida aliyewahi kutamba na Wimbo wa Chambua Kama Karanga ‘Maria Salome’ alisema kuwa anamshukuru Mungu amerudi tena kwenye gemu na wasanii hao wamempa nguvu ya kufanya vizuri katika albamu
hiyo.
“Nimeamka tena jamani nashukuru nimebebwa na wasanii wenzangu Diamond na Belle9 ambao nimewashirikisha kwenye nyimbo zangu ambazo zipo kwenye albamu itakayotoka hivi karibuni,” alisema Saida.
Kwa nyakati tofauti Belle9 ameachia Wimbo wa Give It To Me ambapo ndani yake ameweka vionjo vya Wimbo wa Chambua Kama Karanga wakati Diamond naye amefanyia ‘remix’ ya wimbo huo wa Saida kwa kuita jina la Salome