HABARI KWA WAKATI KUTOKA HAPA

Tunakuhakikishia kupata habari zote zilizo muhimu kutoka ulimwenguni kote kwa wakati, unaweza kusubscribe mtandao wetu na ukawa unapokea habari zote katika email yako punde tu tuchapishapo machapisho yetu. Jiunge na mitandao yetu ya Facebook na Twitter kutupata kirahisi.

HABARI ZA MICHEZO

Sasa Fichuo tunakuhakikishia kupata taarifa zote za kimichezo kutoka viwanja mbalimbali duniani, lengo ni kuhakikisha hupitwi na lolote katika ulimwengu wa michezo.Jiunge na mitandao yetu ya Facebook na Twitter kutupata kirahisi.

TAARIFA ZA BURUDANI NA HABARI ZA WASANII

Unapenda masuala ya burudani? Ni jukumu letu kuhakikisha unazipata info zote za burudani na wasanii wanaokupa burudani, unapata video mpya, movie pamoja na muziki. Kaa karibu nasi.

KURASA ZA MAGAZETI KILA SIKU

Tunakupatia kila ambacho kinaandikwa katika magazeti ya Tanzania na nje ya Tanzania, usitie shaka ukishindwa kununua gazeti uipendalo, sogea karibu nasi na upate kila unachokihitaji.

MAHUSIANO

Fahamu mambo mengi katika ulimwengu wa mapenzi kwa kupitia dondoo, simulizi na visa mbalimbali kupitia Fichuo Online, Jiunge na mitandao yetu ya Facebook na Twitter kutupata kirahisi.

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo HABARI. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo HABARI. Onyesha machapisho yote

Jumanne, Machi 13, 2018

GARI LA MIZIGO LACHOMWA MOTO BAADA YA KUMGONGA MUUGUZI NA KUMSABABISHIA KIFO

Kundi la watu limechoma gari la mizigo baada ya dereva wake kumgonga na kufa papo hapo muuguzi wa Zahanati ya Kaseme wilayani Geita.
Tukio hilo limetokea Jana usiku katika Kijiji cha Kaseme wakati marehemu huyo akiwa katika Bodaboda pamoja na watoto wake wawili, mmoja amefahamika kwa jina Paulo Tarafa mwenye miaka 3 na mwingine mchanga wa miezi miwili ambao wao wamenusurika na kifo hicho.
Mashuhuda wa tukio hilo wamesema lori hilo lilikuwa kwenye mwendo kasi na walipojaribu kupishana na gari jingine ndipo likawagonga na mama huyo kuumia kuanzia sehemu ya kiuno hadi miguuni na kusababisha utumbo kutoka nje.
Wamesema sababu kubwa iliyochangia watoto hao kutopatwa na madhara kama marehemu mama yao ni kwa kuwa alikuwa amewapakata kifuani ambako hawakuguswa na gari hilo.
Jina la marehemu ni Martha Paulo ambaye mwili wake umehifadhiwa katika chumba cha maiti kwenye Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Geita.

AZAM TV

NJIA 6 ZA KUJIKINGA NA RADI


    1. Tafuta hifadhi pahali ambapo kuna jumba kubwa au ndani ya gari. Kukiwa na jumba ambalo lina kifaa cha kukinga dhidi ya radi, utakuwa salama zaidi.
    2. Usiwe katika maeneo ya wazi, au kwenye mlima ulio wazi.
    3. Iwapo utakosa pahala pa kujikinga mvua, punguza uwezekano wako wa kupigwa kwa kujikunyata na kujifanya mdogo zaidi. Unaweza kuchutama, kuweka mikono yako kwenye magoti na kufichwa kichwa chako ndani.
    4. Usijikinge mvua chini ya miti.
    5. Iwapo upo pahala ambapo kuna maji, ondoka na kukwepa maeneo ya ufukweni yaliyo wazi. Utafiti umeonesha kwamba kuwa karibu na maji huongeza hatari ya mtu kupigwa na radi.
    6. Kwa kuwa radi huwa nguvu za umeme, unafaa kujiepusha na vitu vya chuma vyenye ncha kali ukiwa kwenye mvua.

      Jumatatu, Machi 05, 2018

      75% YA WANAOACHA KAZI HUACHA SABABU YA 'MABOSS' WAO

      Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na watafiti kutoka shirika la kazi ulimwenguni ILO imebainika kuwa asilimia kubwa ya waajiriwa wanaoziacha kazi zao walikoajiriwa huacha kazi huwa sababu halisi ni 'maboss' wao.
      Tunaambiwa kuwa 75% ya waajiriwa anaojiuzulu nafasi zao katika ajira ni wale wenye matatizo mbalimbali na viongozi wao kwenye mashirika, na 25% inayosalia pekee ni wale wanaoacha kazi zao kwa sababu nyinginezo.
      Mashirika mengi kutokana na ukubwa wake au majina yaliyokuzwa na huduma zitolewazo hapo huvutia watu wengi kutaka kufanya kazi ndani yake lakini punde wajiungapo na mashirika yenyewe hukutana na visanga vya 'maboss' wao. Sasa kumbe kuna mambo mawili hapa, suala la kupata ajira ni moja na kupata viongozi wazuri ni sababu nyingine.
      Lakini hili linatuonesha mambo mawili makubwa; Kwanza inaonesha dhahiri kuwa viongozi ndiyo huharibu picha nzuri ya taasisi na ni hao hao hufanya mahala pa kazi pasiwe salama kwa wafanya kazi.

      Jumapili, Machi 04, 2018

      AJALI NYINGINE MBILI MBAYA ZA MABASI ZILIZOTOKEA LEO NA KUUA. (+PICHA)

      Baada ya taarifa tuliyokupatia jana kuhusu ajali mbili za mabasi ya abiria zilizotokea katika mikoa ya Tanga na Songwe mabasi ya Lim Safari na New Force yakihusika na kisababisha mauti kwa mtu mmoja, leo tena jumapili machi 4, 2018 ajali mbili zimetokea katika mikoa ya Morogoro na Iringa na kusababisha vifo kwa watu 5.
       
       
       
      Katika ajali iliyotokea mkoani Morogoro  watu 5 wamefariki na wengine 9 kujeruhiwa baada ya basi la abiria aina ya New Force kugongana na gari dogo la abiria aina ya hiace eneo ya Rungemba.
      Imethibitika pia kuwa abiria waliofariki ni Jackson Adam, Georgina Aloyce, Revocata lymo, Mangasa Almasi na Witness Leonard.
      Nako mkoani Iringa abiria waliokuwa wakisafiri katika basi la Kampuni ya Ndenjela lenye namba za usajili T491 CJV lililokuwa likitokea Mbeya kuelekea Dar es Salaam, wamenusurika kifo baada ya basi hilo kupata ajali na kupinduka mlima Kitonga. Baadhi ya abiria wamejeruhiwa na hakuna vifo vilivyotokea.

      Jumamosi, Machi 03, 2018

      TRENI ILIYOPATA AJALI UVINZA ILISABABISHWA NA KICHWA 'KILICHOOKOTWA' BANDARINI!!!???

      Mambo yameanza kuibuka baada ya treni ya kubeba abiria iliyokuwa safarini kutoka Dodoma kwenda Kigoma kupitia Tabora kupata ajali katika eneo la kijiji cha Mpeta, wilayani Uvinza kaskazini magharibi mwa Tanzania, taarifa zinasema.
      Ajali hiyo ilisababishwa na kichwa cha treni kuacha njia na mabehewa mawili kuanguka.
      Kaimu meneja wa wamawasiliano wa Shirika la Reli la Tanzania (TRL) Mohamed Mapondela alithibitisha kwamba watu watatu wamejeruhiwa.
      Utakumbuka pia taarifa za vichwa vya treni ambavyo 'viliokotwa' bandarini Dar es Salaam bila ya mwenyenavyo kufahamika huvku vikiwa na nembo ya TRL baada ya Rais J.P Magufuli kufanya ziara ya kushtukiza bandarini hapo.
      Baada ya ziara ile ya Rais J.P Magufuli baadae ikaja taarifa mpya kutoka kwa waziri Prof. Makame Mbarawa ambaye ni waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano akasema kuwa uchunguzi utafanyika na kisha vichwa hivyo vya treni vikibainika kuwa na sifa vitanunuliwa na serikali.
      Maswali yaliyozuka baada ya ajali ya hivi juzi ni je, vichwa vile vya treni vimekwisha nunuliwa? Vimenunuliwa vingapi? Vimenunuliwa lini? Vimenunuliwa kwa gharama gani? Vilifavyiwa utafiti na kubainika kuwa ni vizima?
      Mwanasiasa Zitto Kabwe, amelizungumzia pia hilo kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter akiitaja kuwa kashfa kubwa

      AJALI MBILI ZA MABASI LEO SONGWE NA TANGA

      Ajali mbili zimetokea leo katika mikoa ya Songwe na Tanga na kusababisha kifo ch mtu mmoja na majeruhi kadhaa.

      Huko mkoani Songwe asubuhi ya leo imetokea ajali iliyohusisha magari mawili, basi la abiria kutoka kampuni ya New Force na gari dogo aina ya Altezza ambapo sababu ya ajali hiyo ikitajwa kuwa ni uzembe wa dereva wa gari hilo dogo aliyehama upande na kuligonga basi hilo akiwa mwendo kasi.
      Katika ajali hiyo dereva wa Altezza amefariki katika pahala ilipotokea ajali na mtu mwingine kujeruhiwa vibaya.
      Taarifa zaidi ya hali za abiria kutoka katika basi la New Force ni kuwa hakujatokea kifo wala majeruhi wa kutisha zaidi ya migongano midogo.

      Nako mkoani Tanga, wilayani Korogwe basi la kampuni ya Lim Safari lenye kufanya safari kati ya Dar es Salaam na Arusha limepata ajali na kusababisha majeruhi kadhaa.
      Katika ajali hiyo hakukutokea kifo. Abiria wanaeleza kuwa mwendo wa gari hilo ulikuwa wa kawaida ila wanahisi ilitokea hitiafu iliyopelekea basi hilo kumshinda dereva.

      Jumatatu, Februari 26, 2018

      NUKUU 6 ZA TUNDU LISSU BAADA YA HUKUMU YA JOSEPH MBILINYI (SUGU) NA EMMANUEL MASONGA

      Jana mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi, Sugu (Chadema)  na mwenzake Katibu wa Chadema Kanda ya Nyasa Emmanuel Masonga walihukumiwa kifungo jela miezi mitano kila mmoja.
      Wawili hao walikuwa wameshtakiwa kwa kosa la kutumia lugha ya dhihaka dhidi ya Rais John Magufuli.

      Wanadaiwa kutenda kosa hilo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika mwezi Desemba 31, 2017 jijini Mbeya.
      Hukumu dhidi yao imetolewa na Mahakama ya hakimu mkazi jijini Mbeya.
      Hati ya mashtaka imesema maneno waliyoyatamka yalienda kinyume na Sehemu 89(1) a ya Sheria za Jinai ambayo inaharamisha kutumiwa kwa lugha ya matusi. Maneno hayo, hati za mashtaka zinasema, yangeweza kusababisha uvunjifu wa amani.
      Image result for SUGU MAHAKAMANI
      Baada ya hukumu hiyo ya jana, mnadhimu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni na mwanasheria mkuu wa chama hicho (Chadema) Tundu Lissu ametoa maneno yake na hapa tunakupatia nukuu 6 za mwanasiasa huyo ambaye pia ni rais wa TLS aliyeko nchini Ubelgiji kwaajili ya matibabu baada ya kushambuliwa na risasi.
      Kwanza, hukumu ya leo (jana) sio mwisho wa mjadala mahakamani. Bado kuna fursa, nay haki, ya rufaa High Court na, ikibidi, Court of Appeal.
      Pili, hukumu ya leo haina maana Sugu atakaa gerezani muda wote huo. Kuna haki ya dhamana pending appeal. Ndivyo ambavyo tumefanya kwa viongozi na wanachama wetu wengi in the past. 
      Tatu, hukumu ya leo haina athari yoyote kwa ubunge wa Sugu. Katiba inaweka masharti ya kifungo cha miezi sita au zaidi, na kwa makosa ya 'utovu wa uaminifu.' Uchochezi au kutoa lugha ya matusi sio makosa ya utovu wa uaminifu. 
      Nne, pamoja na kwamba sijaona nakala ya hukumu, adhabu ya kifungo bila faini kwa kosa la kwanza ni kinyume na sentencing principles. Hii ni mojawapo ya hoja zetu zilizoshinda katika kesi ya Mh. Juakali High Court mwaka jana. 
      Tano, hata kama atakaa gerezani muda wote huo, hukumu za kesi za kisiasa kama hii hazijawahi kuwapunguzia heshima wapigania haki popote pale duniani. 
      On the contrary, kifungo cha aina hii ni beji ya heshima kwa kila mpigania haki na uhuru. Orodha ya mifano ni ndefu sana: Nyerere (ijapokuwa yeye alilipa faini), Kenyatta, Mandela, Mugabe, Fidel Castro, etc. 
      Alichokifanya hakimu leo ni kuwaongeza Sugu na Masonga kwenye orodha hii ya heshima. They'll come out even bigger and stronger than when they went in. 
      Sita, naunga mkono pendekezo la Mh. Zitto kwamba wabunge wetu wote warekodi maneno aliyofungiwa nayo Sugu na kuyaweka mitandaoni ili watukamate na sisi pia. 
      Instead of agonising, let's organise and make this issue bigger and bigger mpaka wakimbie wenyewe au watukamate na kutufunga wote. 
      Na sio wabunge tu, tuhamasishe kila mwanachama wetu na kila anayechukizwa na uonevu huu ayarudie maneno haya ili nao wakamatwe na kufungwa. 
      Tumlazimishe Magufuli na watu wake waamue: waigeuze nchi nzima kuwa gereza moja kubwa, au akubali kusemwa kwa maneno na lugha asiyoipenda. Hiyo ndio maana pekee ya freedom of speech in a democracy.

      UTAMADUNI WA KUCHEZA UTUPU MSIBANI CHINA UNAZIDI KUSHIKA KASI

      Muziki unacheza kwa sauti, wacheza utupu wakicheza densi na umati ukishangilia. Katika sehemu zingine huko China hili ndilo unaweza kuliona wakati wa mazishi.
      Mapema mwaka huu, China alianza tena kuwakamata wacheza utupu wanaocheza densi kwenye mazishi, harusi na kwenye mahekalu.
      Hio sio mara ya kwanza mamlaka zimejaribu kuzuia tabia hizo lakini bado hazijanafikiwa

      Related image

      Mbona watu huwaajiri wacheza utupu?

      Wacheza utupu hutumiwa kuwavutia watu wnaaohudhuria mazishi kwa sababu uwepo wa watu wengi kwenye mazishi huonekana kama heshima kwa marehemu. Imani nyingine zinasema kuwa suala hilo na la kuabudu.
      Imani nyingi ni ile kuwa kuwaajiri wacheza utupu kunaweza kuonekana kama ishara ya utajiri.
      Maeneo ya vijijini nchini China ndiyo yenya tabia ya kutumia pesa nyingi hata kuliko mapata, kuwalipa wuigizaji, waimbaji, wachekeshaji na wacheza utupu kuwatumbuiza wale waliofiwa.

      Image result for Pole dancers ON FUNERALS

      Shughuli hii ni maarufu?

      Tamaduni hiyo inapatikana sana maeneo ya vijijini ya China na ni maarufu zaidi nchini Taiwan ambapo ilianzia.
      "Tamaduni hii ya wacheza utupu kwenye mazishi kwanza lilipata umaarufu nchini Taiwan mwaka 1980," msomi wa chuo cha South Carolina Marc Moskowitz aliiambia BBC.
      Tamaduni hii imepata umaarufu nchini Taiwan lakini nchini China serikali imeizuia na watu wengi hawafahamu kuihusu.


      BBC

      Jumapili, Februari 25, 2018

      WATU WANAOSHEREHEKEA SIKUKUU YA CHRISTMAS MWEZI FEBRUARI

      Wanakijiji wanasema kuwa utamaduni huu ambao ulianza enzi za utumwa wakati mababu zao walipozuiwa kusherehekea Krismasi tarehe 24 Desemba kama ilivyo kawaida kwa madhehebu mengi ya Kikristo.
      Badala yake waliamua kuchagua katikati mwa mwezi wa Februari na utamaduni huu umeendelea tangu wakati huo.
      Fataki, muziki na densi huwa sehemu ya sherehe hizo za kuvutia.
      "Watu waliotufanya watumwa walisherehekea Krismas Desemba na hatukuruhusiwa kuwa na mapumziko siku hiyo, lakini tukaambiwa tuchague siku nyingine," alisema, Holmes Larrahondo, mratibu wa sherehe.
      "Katika jamii yetu tunaamini kwamba mwanamke anapaswa kufunga siku 45 baada ya kujifungua, kwa hivyo tunasherehekea Krismas sio mwezi Disemba, bali Februari, kwa hiyo Maria anaweza kudensi pamoja nasi," aliongeza Bw Larrahondo.

      Balmores Viafara, mwalimu mwenye umri wa miaka 53 aliliambia shirika la habari la Ufaransa AFP kwamba kutokana na hilo kwake tarehe 24 Disemba "ni kama siku nyingine yoyote ile ".
      Wakati wa kuabudu, sherehe hizo huitwa "sherehe za kutoa heshma kwa Mungu wetu kwa namna yetu."
      Kama sehemu ya sherehe hizi, wanakijiji hutembelea nyumba mbali mbali "wakimtafuta mtoto Yesu", ambaye huwakilishwa na sanamu ya mbao ambayo hutunzwa na mmoja wa wanavijiji katika nyumbani kwake kwa kwa kipindi cha mwaka kilichosalia.

      Pale sanamu inapopatikana, hutembezwa kijijini na wakazi wa rika zote waliovalia kama malaika na wanajeshi.
      Wacheza densi, hucheza densi inayoitwa fuga; ambapo hucheza wakiigiza hatua za watumwa waliofungwa minyororo.
      Sherehe humalizika majira ya asubuhi mapema.

      MATUMIZI SAHIHI YA GIA D, L, 2, 3 NA O/D KATIKA GARI AMBAZO NI AUTOMATIC

      Fichuo inafahamu kuwa yawezekana wewe ni moja ya watu wanaopata shida katika matumizi ya GIA Automatic, kwanza ujue kabisa katika hali ya kawaida gari yako inapaswa kuwa katika D kwa maana ya Drive na hii inategemeana na mazingira ya barabara na hali yali ya hewa kama ni nzuri lakini 2, 3 hutumika tu pale unapokuwa ama unashuka mteremuko mkali au unapanda mlima mkali kama vile Sekenke na unataka ushuke au upande kwa speed ile ile ila isizidi 40/60 hapo ndipo unashauriwa kutumia 2, 3
      Namba 2, 3 na L huwa inalock GEAR BOX ili gear zisibadilike (-/+) kama ambavyo zinabadika ukiweka D na itambulike kuwa unaweza kubadili toka D kwenda 2 au 3 wakati wowote gari inapokuwa katika mwendo ila hakikisha usiwe speed zaidi ya 40/60 maana kinachofanyika ni kwamba D inasababisha sahani DISKS zilizomo ndani ya GEARBOX kufanya kazi na hii hupelekea ile hydrolic iliyomo kupata joto linalotoka katika zile sahani ambalo joto lile husababisha GEARBOX kutokuwa na nguvu ile ile (constant velocity) na ndo maana ukiweka 2, 3 au L gear box inakuwa kwenye lock na sahani hazisuguani maana inakuwa inatumika sahani/disk moja tu kwa hiyo inasaidia ile hydrolic kupoa pia na ndo maana gari huongeza nguvu kwa ghafla.
      Image result for automatic transmission L inatumika pale unapokuwa either umekwama au unavuta gari jingine au tera ila inapaswa itumike kwa muda mfupi sana maana inanguvu sana na pia inaongeza ulaji wa mafuta, kwahiyo kama ukitoka katika mkwamo na unaona bado barabara si nzuri labda utelezi au unavuta mzigo kwa mwendo mrefu basi unaweka 2 au 3 na wakati huohuo unaweza kuweka hata D kama hali ya njia na mzigo vinaruhusu na unaweza kuongeza walau speed 40/60 au zaidi kama utaweka D kwa maana rahisi zaidi ni kwamba 2,3,na L inafanya kazi kama gari ya Manual na hii inakuwa rahisi kwa yeyote ambaye anafahamu kuendesha manual.
      Image result for car on mud Over Drive inatumika pale gari inapokuwa speed zaidi ya 60/80 kutegemeana na aina ya gari na hili hutokea bila wewe kujua maana gari yenyewe  hufanya hivyo ndio maana unashauriwa iwe ON muda wote kusudi gari ichague ni wakati gani iweke ON/OFF maana ukiwa chini ya speed 60/80 hata kama umeweka ON bado inakuwa haifanyi kazi.
      Mwisho ni kwamba OD unaweza kuitumia kama break/stop engine hasa unapokuwa zaidi ya Speed 80 na wakati huo iko ON yaani katika dashboard taa ya OD izime...ikiwaka maana yake iko OFF, basi ili upunguze mwendo kwa haraka unachofanya ni kuweka OFF na wakati huo unakanyaga break taratibu utaona mwenyewe gari lako linavyopunguza mwendo taratibu na wakati mwingine si lazima ukanyage break, we iweke OFF tu halafu toa mguu katika pedal ya mafuta gari lazima li slow down na kama lilikuwa ni tuta na umeshalipita basii iweke tena ON ongeza mafuta au unaweza kuweka 2 au 3 ili gari ianze kwa kasi zaidi na ikiisha changanya basi rudi kwenye D na endelea kama kawaida.

      Ijumaa, Februari 23, 2018

      ZIFAHAMU KAZI/AJIRA 10 ZENYE KUSABABISHA STRESS ZAIDI

      Leo tunakufichulia ajira 10 ambazo husababisha msongo zaidi wa mawazo (STRESS). Kutokana na matamanio ya wengi kuona watu fulani wamefanikiwa kupitia shughuli wanazozifanya..kumekuwa na ombwe kubwa la watu wakitaka kufanya shughuli hizo pasi kujali changamoto ambazo ziko ndani ya ajira/shughuli hizo.
      Ziko ajira nyingi zenye hatari, ambazo kutokana na changamoto zake watu wanaozifanya shughuli hizo hujikuta wakiishia kupata msongo mkubwa wa mawazo, kunawengine huishia kukata tamaa na kujiuzulu kufanya hizo kazi ama kuzifanya bila raha.

      Hapa tunakuletea aina 10 za ajira zenye kuleta zaidi msongo wa mawazo;

      10. Utangazaji wa Redio na Tv kwa kiasi cha 47.93%

      Image result for radio and tv broadcasting
      Hii ni kutokana na changamoto za kazi yenyewe. Watangazaji wamekuwa wakiwindwa sana  na maadui wa tasnia yao ambao wamekuwa wakiumbuliwa na matangazo yanayorushwa  katika Redio na Tv. Wapo wanaouawa, wapo wanaofungwa magerezani na hata wanao vamiwa na kushambuliwa.

      9. Udereva wa TAXI kwa 48.18%

      Image result for taxi
      Hii unaambiwa nayo ni kazi yenye changamoto kwa kiasi cha 48.18%. Hii ni kwa mujibu wa jarida la Forbes ambalo liliangalia haswa changamoto za wateja wanaokodi magari, ziko za ulevi,lugha za kigeni na uhalifu.

      8. Uafisa mahusiano kwa 48.50%

       Image result for haji manara
      Mara nyingi hawa ndiyo wenye dhamana na taswira za makampuni kwa wahudumiwa. Iwapo kampuni itaenda mrama au itakutana na kashfa basi hawa ndio hupata kazi ngumu ya kuisafisha kambuni na ndio maana kazi yao inashika nafasi ya 8 kwa kusababisha msongo wa mawazo.

      7. Mkurugenzi Mtendaji kwa 48.56%

      Image result for c.e.o
      Huyu huwa ndio kiongozi wa ngazi ya juu katika kambuni, anajukumu kubwa la kuifanya kampuni ifanye kazi vile inavyotakiwa, hutu huyu hutakiwa kutumia akili nyingi sana kubuni na kupanga mikakati ya kuifanikisha kampuni.

      6. Uandishi wa Habari wa Magazetini kwa 49.90%

      Image result for news covering
      Hii sababu zake hazitofautiani sana na hatari zilizopo hapo juu katika no. 10 ya Utangazaji wa Redio na Tv, isipokuwa kwa upande wa magazeti waandishi huwa hatarini sana kutokana na uwapo wa nafasi kubwa ya kutoa maoni yao au taarifa kwa urefu.

      5. Uandaaji wa Matukio kwa 51.15%

      Image result for event coordinator
      Hapa napo zipo changamoto nyingi kwa wahusika, tufafahamu nguvu kubwa ya kuandaa matukio, hofu kubwa ni je, vipi tukio unaloandaa likifeli? Hapo ndipo unapata stress!

      4. Uaskari kwa 51.64%

      Image result for askari polisi
      Sote tunafahamu changamoto ya kusimamia masuala ya ulinzi na usalama, kila siku kunaripotiwa kutokea kwa visa vidogo na vikubwa vya uhalifu. Askari ndio watu tuwategeao kwa kiasi kikubwa kuyadhibiti haya, sio Tanzania tu, hata mataifa mengine ulimwenguni.

      3. Urubani kwa 60.54%

       Image result for pilot
      Ni kazi ambayo hutumia akili nyingi na inahitaji utimamu wa akili na mwili kiafya. Urubani ni masuala ya kihesabu sana, unaruka kwa makadirio ya namba kitaalamu tofauti na udereva wa barabarani. Vipi ukizikosea hesabu zako au kukiwa na hali mbaya ya hewa huko angani? Najua umefahamu kiwango cha stress kinachotoka hapa.

      2. Zima Moto kwa 72.68% 

      Image result for fire rescue
      Inawezekana kwa hapa kwetu Tanzania hatujakutana na visa vikali vya moto, lakini kwa wenzetu metaifa mengine imekuwa kawaida kwao kupambana na matukio haya, hugharimu muda, nguvu, akili na pesa za uwezeshaji wa shughuli zenyewe.

      1. Wapiganaji wa Vita kwa 72.74%

      Image result for african soldiers
      Hapa bila shaka tutakubaliana, hakuna asiyeijua hatari ya vita. Aendaye vitani kuna mambo matatu; Unusurike, upate ulemavu au upoteze maisha kabisa!

      Jumanne, Februari 20, 2018

      HAYA NI MAMBO 10 MUHIMU AMBAYO HUKUFUNDISHWA SHULENI...MUHIMU SANA KUYAFAHAMU

      Kwa miaka zaidi ya 15 ambayo umekaa kwenye mfumo wa elimu umejifunza vitu vingi sana. Kwanza ulijifunza jinsi ya kusoma na kuandika, baadae ukajifunza vitu muhimu kwenye historia, jografia, sayansi na hata mahesabu. Mwisho kabisa ukapata elimu ya utaalamu na hatimaye ukamaliza masomo yako kwenye utaalamu au ujuzi uliochagua kusoma.
      Pamoja namambo hayo mengi na mazuri uliyojifunza kwa miaka hiyo mingi kuna mambo mengi sana ambayo ni muhimu kwenye maisha hukupata nafasi ya kujifunza au kufundishwa. Kutokujua mambo hayo muhimu kuhusu maisha ndio kumekuwa chanzo kikubwa cha wahitimu wengi kuona maisha ni magumu sana wanapofika mtaani.
      Leo tuangalie mambo kumi muhimu ambayo hukufundishwa shuleni ila ni ya muhimu sana kwenye maisha yako.

      Mambo haya kumi muhimu ni; 

      1. Wewe ni wa pekee.

      Katika watu zaidi ya bilioni saba wanaoishi kwenye dunia hii hakuna hata mmoja ambaye anafanana na wewe kwa kila kitu. Wewe ni wa pekee, una uwezo mkubwa sana na una vipaji na ubunifu wa kipekee. Ukishajua hili itakuwa rahisi kwako kufanikiwa kwani hutoweza kujilinganisha na mtu mwingine.
      Shule imefanya kazi nzuri sana ya kukulazimisha kujilinganisha na wengine kwenye kila jambo unalofanya. Hii ni kwa sababu shuleni ulikuwa unafanya mtihani mmoja na wanafunzi wengine wote hivyo kupimwa kwa kulinganishwa.
      Acha sasa kujilinganisha na wengine na tambua wewe ni wa pekee na hakuna anayeweza kufanta unayoweza kufanya wewe.

      2. Unaweza kufanya chochote unachotaka.

      Kwa kuwa wewe ni wa pekee, pia una uwezo mkubwa sana wa kuweza kufanya MAMBO MAKUBWA SANA. Kamwe usijishushe na kujiona wa chini, unaweza kufanya jambo lolote unalotaka kulifanya kwenye maisha yako. Unaweza kuyafanya maisha yako kuwa bora kuanzia sasa unapomaliza kusoma hapa. Kitu muhimu ni wewe kujua ni kitu gani unataka kwenye maisha yako na kukitafuta kwa juhudi na maarifa.

      3. Hakuna jibu moja sahihi.

      Mitihani uliyokuwa unafanya shuleni ilikulenga kuchagua jubu moja sahihi na kuacha mengine ambayo sio sahihi. Kwa bahati mbaya sana maisha hayako hivyo. Hakuna jibu moja sahihi au ambalo sio sahihi, yote ni majibu na yana usahihi na makosa kadiri maisha yanavyozidi kwenda.
      Usidanganyike kwamba kuna kitu kimoja ukifata ndio utafanikiwa kwenye maisha, njia ya mafanikio ina vikwazo na changamoto nyingi. Usirudishwe nyuma na changamoto hizi kwa sababu ya mambo uliyofundishwa shuleni kwamba jibu sahihi ni moja tu.

      4. Maana ya mafanikio.

      Kila mtu kwenye maisha anataka kupata mafanikio makubwa, ila ni wachache sana ambao wanajua maana halisi ya mafanikio. Shuleni ulifundishwa kwamba kufanikiwa na kupita kiwango fulani cha maksi au hata kuwapita wengine darasani kwa ufaulu wa maksi.
      Kwa bahati mbaya sana kwenye maisha mafanikio hayapimwi hivyo. Ukiangalia mafanikio kwa kutaka kuwashinda wengine au kuwa sawa na wengine utaishi maisha yako yote kukimbiza upepo. Maana ukijitahidi ukanunua gari kuna mtu utamkuta ana magari mengi zaidi yako, ukasema mafanikio ni kujenga nyumba kwa sababu kila mtu ana nyumba utakutana na mtu mwenye nyumba kubwa, nzuri na nyingi kuliko ya kwako. Kwa akili hii utaumia kichwa na kuona maisha yako hayana maana.
      Badala ya kuendeshwa na mafanikio ya wengine kaa chini na uandike maana yako mwenyewe ya mafanikio kisha ishi kuitimiza maana hiyo.

      5. Hakuna mtu yeyote au kitu chochote kinaweza kukupa furaha.

      Hili ni jambo muhimu sana ambalo hukupata nafasi ya kufundishwa. Furaha inatoka ndani yako mwenyewe, hupewi na mtu au kitu unachomiliki.
      Kama unafikiri mwenzi wako ndio atakupa furaha basi kuna siku utaumizwa sana, kama unafikiri fedha nyingi ndio zitakupa furaha uko kwenye tatizo kubwa. Furaha ipo ndani yako na utaipata kutokana na maisha unayoishi na mambo unayoyafanya kwako na kwa watu wengine.

      6. Kufaulu darasani hakumaanishi kufaulu kwenye maisha.

      Mazingira ya darasani yanatabirika, kaa darasani, soma kwa bidii, jiandae na mtihani na utafaulu. Mazingira ya kwenye maisha hayatabiriki hata chembe, unaweza kufanya kazi kwa juhudi na maarifa na bado yakatokea mambo yakakurudisha nyuma. Mitihani ya shuleni unajua ni lini inakuja hivyo unaweza kujiandaa muda huo ila mitihani ya kwenye maisha haina ratiba na hivyo inakukuta hujajiandaa. Ndio maana kufaulu darasani hakumaanishi ndio utafaulu kwenye maisha, kuna mambo mengi sana unatakiwa kujifunza.

      7. Kukosea/kufeli ndio kujifunza.

      Shuleni kufeli ni kwamba hujui au hujajiandaa vizuri na hivyo kukufanya uonekane wewe ni mwanafunzi dhaifu. Ila kwenye maisha kukosea au kufeli ndio njia sahihi ya kujifunza. Hujajifunza jambo lolote kweye maisha kama hujafeli au kuhsindwa kwenye jambo hilo. Badala ya kuogopa kufeli kwa sababu utaonekana ni dhaifu, hebu anza kuchukua kufeli kama sehemu ya kujifunza kwenye maisha yako.

      8. Kuweka malengo.

      Hiki ni kitu kimoja muhimu sana ambacho hukupata nafasi ya kufundishwa na kusisitiziwa vizuri wakati upo shuleni. Ni vigumu sana kuweza kufikia mafanikio makubwa unayotegemea kwenye maisha yako kama hutaweka malengo makubwa na mipango ya kufikia malengo yako. Kwa kushindwa kufanya hivi unawapa nafasi watu wengine wakutumie wewe kufikia malengo yao. Nakuomba ubonyeze hapa kufungua makala za malengo na ujifunze zaidi kuhusu malengo na jinsi unavyoweza kutekeleza hilo kwenye maisha yako.

      9. Matumizi ya fedha binafsi.

      Fedha ni muhimu sana kwenye maisha yetu na huenda sababu kubwa iliyokufanya ukae shuleni miaka yote hiyo ni kupata fedha baadae. Pamoja na umuhimu huu wa fedha hukuwahi kupata nafasi ya kufundishwa matumizi na mipango binafsi ya fedha unazozipata. Hii inakusababishia kuwa na matumizi mabaya ya fedha na kuona maisha magumu kila siku.
      Ni muhimu sana kuwa na matumizi mazuri ya fedha zako kwani hiki ndio kitakuwezesha kufikia mafanikio makubwa unayotazamia. Kujifunza zaidi kuhusu fedha tafadhali jiunga na KISIMA CHA MAARIFA na utapata kujifunza mambo mengi muhimu kwenye maisha.

      10. Haijalishi unajua nini bali unamjua nani.

      Umeaminisha shuleni kwamba kama ukisoma kwa juhudi na maarifa, ukajua vitu vingi sana basi unaweza kufikia mafanikioa makubwa sana. Kujua vitu vingi sana hakuwezi kukusaidia kama huwajui watu muhimu. Hivyo kwa kuwa umeshajua vitu vingi sasa wekeza nguvu sako kuwajua watu sahihi ili kuweza kufikia malengo yako. Mafanikio yako yatatokana na watu muhimu ulionao kwenye mtandao wako. Hivyo jua watu wengi sana na muhimu zaidi jua wale ambao watakusaidia kufanikiwa kwenye taaluma au shughuli unazofanya.

      Alhamisi, Oktoba 12, 2017

      UCHAGUZI WA RAIS DRC WASOGEZWA MBELE

      Tume ya uchaguzi katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo imeahirisha uchaguzi wa rais hadi Aprili 2019. Imesema zoezi la uandikishaji wapiga kura katika jimbo la Kasai ya Kati halijakamilika
      Tume ya uchaguzi katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo imeahirisha uchaguzi wa rais hadi Aprili 2019, ikitaja kutokamilika kwa zoezi la uandikishaji wapiga kura katika jimbo la Kasai ya Kati kwa sababu ya machafuko na mapigano kati ya jeshi na waasi. Zaidi ya watu 5,000 wameuwawa jimboni humo na zaidi ya milioni moja kuyahama makazi yao tangu Agosti mwaka jana.
      Rais wa tume ya uchaguzi amesema kucheleweshwa huko ni muhimu na kwamba maafisa watahitaji siku 504 kuandaa uchaguzi wa rais. Rais Joseph Kabila, ambaye alichukua madaraka baada ya baba yake, Laurent Desire Kabila, kuuwawa 2001, alifikia makubaliano na upinzani Desemba mwaka jana 2016 kuwa uchaguzi ufanyike Desemba 2017. 
      Tayari Kabila amemaliza mihula yake miwili kwa mujibu wa katiba, lakini mahakama iliamuru anaweza kubakia madarakani hadi utakapofanyika uchaguzi mpya.

      Jumanne, Oktoba 10, 2017

      VIJIJI NDILO ENEO MUHIMU ZAIDI KWA UKUAJI WA UCHUMI

      Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa FAO jana lilitoa ripoti ikisema, katika miongo kadhaa ijayo kama sehemu za vijijini katika nchi zinazoendelea zikiweza kutimiza maendeleo yenye uwiano na uzalishaji wa chakula na viwanda vinavyohusika, uchumi wa nchi hizo utaweza kukua kwa kasi, na kutoa nafasi za ajira kwa mamilioni ya vijana.
      Ripoti hiyo kuhusu hali ya chakula na kilimo kwa mwaka 2017 imeeleza kuwa, eneo la vijiji linahitaji kufanyiwa mageuzi kamili ili kuchochea maendeleo, na kukidhi mahitaji ya chakula na ajira kwa vijana na idadi kubwa ya watu inayoendelea kuongezeka.
      Ripoti pia inaona kuwa, sera madhubuti na uwekezaji kwenye mfumo wa chakula vijijini, pamoja na uungaji mkono kwa sekta za kilimo zenye uhusiano wa karibu na maeneo ya miji haswa miji midogo na ya ukubwa wa kati, vitachangia kuongeza ajira, na kuwafanya watu wengi zaidi kubaki vijijini.

      Jumapili, Oktoba 08, 2017

      PEMBE YA AFRIKA KUKUMBWA NA MAPIGANO SABABU YA MABADILIKO YA HALI YA HEWA

      Mkurugenzi wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP, Bw. Erik Solheim amesema eneo la Pembe ya Afrika linaweza kuwa kitovu cha mapigano makubwa wakati athari za mabadiliko ya hali ya hewa zikiongeza ugumu wa kutafuta malisho na maji.

      Akizungumza wakati wa maonyesho ya filamu ya "A Climate for Conflict" jijini Nairobi, Kenya, Solheim amesema kuongezeka kwa joto duniani kitakuwa chanzo kikuu cha mapigano ya wenyewe kwa wenyewe, ugaidi, na kuhama kwa lazima katika eneo kubwa la Pembe ya Afrika.
      Bw. Solheim amesema, uhusiano kati ya mabadiliko ya hali ya hewa na ukosefu wa usalama utajadiliwa kwa kina katika mazungumzo ya mabadiliko ya hewa yatakayofanyika hivi karibuni.

      Pembe ya Afrika ni ipi?

      Pembe la Afrika ni jina la sehemu ya mashariki kabisa ya bara la Afrika yenye umbo la pembetatu; ni kama rasi iliyoko kati ya Ghuba ya Aden na Bahari Hindi yenyewe.
      Eneo hili linajumuisha nchi za leo za Somalia na Jibuti pamoja na sehemu ya mashariki ya Ethiopia; wakati mwingine Ethiopia yote pamoja na Eritrea huhesabiwa humo.
      Nchani mwa pembe iko Puntland iliyotangaza uhuru wake lakini inahesabiwa kama sehemu ya Somalia na mataifa mengi, jirani yake ni Somaliland ambayo ni pia sehemu ya Somalia iliyotangaza uhuru wake.
      Kwa kutumia wazo la pembe la Afrika kubwa kuna eneo la 2,000,000 km² linalokaliwa na wakazi milioni 94.2 million (Ethiopia: milioni 79, Somalia: milioni 10, Eritrea: milioni 4.5 na Jibuti: milioni 0.7).

      AIRBUS KULETA NDEGE ZITAKAZOTUMIA BETRI

      Kampuni ya kutengeneza ndege ya Airbus imetangaza kuwa itaanza kuunda ndege kama hii inayotumia betri.
      Ina uwezo wa kubeba waty 4 na kusafiri kwa kasi ya kilomita 120 kwa saa.
      Hasa itatumika kuepuka msongamano wa magari pale mtu anapokuwa na dharura. 
      Ndege hii mpya inatarajiwa mwaka 2018.

      MATAIFA AMBAYO WATU WAKE HUISHI MAISHA MAREFU

      Utafiti uliofanywa unaonyesha kuwa, wananchi wa Japan, Uhispania, Uswisi na Korea Kusini wanaishi maisha marefu zaidi ikilinganishwa na watu wa maeneo mengine katika pembe mbalimbali duniani.
      Utafiti huo unaonyesha kuwa, Wajapani wanaishi kwa wastani wa miaka 83 hadi kufariki dunia. Sababu kubwa inayotajwa kuchangia katika kurefusha umri wa Wajapani ni vyakula vya asili wanavyokula. Viazi vitamu na samaki ni aina ya vyakula vyenye mchango mkubwa. Pia, jamii ya Japan inatajwa kuwa ni jamii imara isiyo na migogoro mingi jambao ambalo linawasaidia kupunguza msongo wa mawazo.
      Nchini Uhispania wastani wa kuishi ni miaka 82.8. Kwa mujibu wa utafiti huo, siri kubwa ya kufikia umri huu ni utajiri wa mafuta bora kwa afya ya mwanadamu yaani mafuta ta zaituni na ulaji wa mboga za majani kwa kiasi kikubwa. Jambo jingine ni tabia ya Wahispania ya kupendelea kutembea zaidi kwa miguu na kuendesha baiskeli hata kama wana magari.
      Nchi nyingine ni Uswisi ambayo ni mojawapo ya nchi tajiri barani Ulaya. Raia wa nchi hii wanaishi kwa wastani wa miaka 81. Wamefanikiwa kufikia wastani huo mkubwa kwa sababu ya huduma bora za afya, usalama wa raia na mali zao na upendo uliotapakaa katika viunga vya nchi hii tajiri.
      Wakati huo huo, tafiti za hivi karibuni zinaitaja Korea Kusini kuwa nchi ya kwanza duniani kwa raia wake kuishi miaka mingi. Wastani wa umri wa kuishi huko Korea Kusini ni miaka 90. Wamefikia wastani huo kwa kupendelea kula vyakula vilivyochachishwa ambavyo inasemekana vinasaidia kupunguza mafuta mwilini, kuongeza kinga ya mwili, na kuzuia kansa. Pia vyakula vya Wakorea vina kiwango kikubwa cha ufumwele (fibre).

      Jumanne, Oktoba 03, 2017

      KAZI ZITAKAZOWEZA KUREFUSHA MAISHA YA WAZEE

      Kubeba bidhaa waliyonunua, kufanya ukulima kidogo kwenye bustani na kusafisha nyumba kunaweza kuwasaidia watu wazee kuwa na maisha marefu yenye afya, kulingana na wataalamu wa afya.
      Madaktari wanasema kuwa mamilioni ya watu wazee huanguka kila mara kwa sababu hawafanyi mazoezi.
      Robo ya watu walio na umri wa zaidi ya miaka 65 hawafanyi mazoezi yoyote ya kuwapa nguvu, kulingana na madaktari ambao wanaonya kuwa kuongezeka kwa nafasi za kunua bidha mitandaoni kunamaanisha kuwa watu hawaendi madukani na kubeba bidhaa kutoka huko hadi nyumbani kwao.
      Madaktari wanasema kuwa watu wengi hawafahamu umuhimu wa kufanya mazoezi ya kuwapa nguvu wanapoendelea kuongeza miaka.
      Ni vyema kwa watu kufanya mazoezi ya kuwapa nguvu angalau mara mbili kwa wiki, kama kubeba mizigo mizito. Lakini utafiti uliohusisha zaidi ya watu wakongwe elfu mbili nchini Uingereza ulionyesha kuwa wengi wao hawafanyi mazoezi kamwe.
      Mmoja kati ya watu watano alisema hawajui kufanya mazoezi na wengine walisema hawataki tu kuyafanya.
      Ajali za kuanguka miongoni mwa watu wazee huchangia asilimia kubwa ya majeraha inayohusisha kuvunjika kwa mifupa ya sehemu ya kiuno, na hugharimu takriban dola bilioni moja kutibu kila mwaka.
      Profesa Karen Middleton, ni afisa mkuu mtendaji wa CSP, na anasema tunakuwa dhaifu tunapokuwa wazee.
      "Utafiti unaonyesha kuwa kufanya mazoezi ya kutupa nguvu kuna faida nyingi na ni muhimu watu kuzingatia haya."
      Anasema inaweza kuwa kupalilia shambani au kusimama mara 10 kutoka kwenye kiti.
      "Siku hizi tunabeba mifuko chache sana tukitoka dukani na mara nyingi tunanunua bidhaa mitandaaoni."
      Profesa Middleton anasema kubeba mifuko ya chakula na bidhaa nyingine kutoka sokoni kunachangia mazooezi kwenye misuli.

      Alhamisi, Septemba 28, 2017

      NYERERE ALIUCHUKULIAJE UKAHABA? ALIAMUA NINI WALIPOFUKUZWA NA RC RWEGASIRA 1980?

       HUENDA ni jambo lisiloingia akilini kwa hali ya kawaida, pale mwenendo uonekanao ni dhambi kwa Mungu, kutetewa na mtu atambuliwaye na wengi ni Mcha-Mungu!
      Hata hivyo, kwa mujibu wa kauli ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, aliyejulikana vile, hata ikatabirika baada ya kifo chake kuwa angetangazwa Mwenye Heri hatimaye Mtakatifu, si sahihi mwanadamu kumhukumu mwenziwe isipokuwa Mungu Mwenyewe!
      Ndiyo maana ilipopangwa operesheni ya kurejesha makahaba makwao kwa shuruti Dar es Salaam mnamo miaka ya 1980, Mwalimu Nyerere alimuita Ikulu aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo kwa wakati ule, Joseph Rwegasira, akitaka aende akamfafanulie utaratibu na madhumuni ya operesheni ile!
      Alipofika, kauli ya kwanza ya Mwalimu ilimtumainisha kuwa huenda operesheni yake iliungwa mkono pale alipohoji, “Nasikia umeamua kuwahamisha mama zangu warudi makwao wakalime maharagwe!” Rwegasira alijibu haraka kwa kusema, “Unajua Mwalimu, hatua yangu hii ni kutekeleza kaulimbiu yetu ya ‘Kilimo ni Uti wa Mgongo wa Taifa Letu’, na operesheni ya ‘Kilimo cha Kufa na Kupona’, pengine hata kaulimbiu ya awali tuliyoita, ‘Siasa ni Kilimo,’ ndipo nikaiona ni muafaka kabisa!”
      Hapo ndipo hoja ya Mwalimu iliyofuatia ilimshtua Rwegasira, pale aliposema, “Nimekuita unieleweshe ni watu wa aina gani ulioteua warudishwe makwao kwa utekelezaji huo, pia utaratibu unaotumika!”
      Katika mazungumzo yangu na Rwegasira aliniambia ya kuwa angeweza, kuzua aina nyinginezo za watu alioandaa wasafirishwe makwao, lakini kwa jinsi alivyoniamba mwenyewe, ilibidi akiri ya kuwa ilihusu makahaba tu.
      Kwani aligundua kwa hisia ya kuwa Mwalimu alikwishakujua hali halisi, hivyo akasema wazi, “Nimedhamiria tu makahaba mheshimiwa, kwa kuzingatia matendo yao!” Ndipo Baba wa Taifa aliishia kuhoji, “Kwa hiyo umewahukumu kwa ukahaba wao, au kuna sababu nyingine?” Hapo, Rwegasira alikaa kimya kwa kutokuwa na jibu muafaka!
      Hata hivyo, Baba wa Taifa aliendelea kudadisi kwa kuhoji, “Ikiwa umeamua kuwatimua makahaba, je, mazingira ya kule utakakowahamisha, umeyaandaaje?”
      Kwa kuwa hoja ya Baba wa Taifa ilikuja kinyume na matarajio ya Rwegasira, isitoshe hakuelewa mwelekeo wa hoja ile, alibaki kimya, ndipo Mwalimu aliamuamuru kwa kusema, “Ukiweza kutimiza hilo, njoo unieleze nibariki operesheni yako!”
      Aliongeza kwa kusema, “Kama usingekuwa mtani wangu wito wangu ungeishia hapa, lakini hebu nikufafanulie chanzo cha ukahaba, ndipo aliuliza iwapo Rwegasira anafahamu wateja wa makahaba ni kina nani, akawa amejibu kuwa ni wanaume!
      Mwalimu alicheka akamuuliza, “Wewe si mwanaume, je, huko waliko makahaba unakwenda?” Rwegasira alijibu, “Hapana!” Akahoji tena, “Mimi si mwanaume, je, huko naenda?” Rwegasira alijibu, “Hapana Mwalimu!” Ndipo alianza kumchambulia kuanzia wanaume wasiojua kumtaka mapenzi mwanamke, wasiotaka bughudha ya kutunza familia hivyo hawaoi, hata waliobarikiwa nguvu nyingi za mwili wakienda huko kuzipunguza ili wasisumbue wake zao! Na hapo ndipo Mwalimu alifafanua hoja yake kwa Rwegasira akisema, “Nilipotaka nijue mazingira ya huko utakakowaondoa umeyaandaje, nilijua hao wateja wao wasipowakuta, matokeo ni kubakwa mama zetu, wake zetu, wanafunzi wetu, vilema wetu, hata vichaa wetu! Ndiyo maana katika miji yote duniani makahaba wapo!”
      Mwalimu alimalizia kwa kumwambia Rwegasira ya kuwa, hata mataifa yaliyojigamba kuwa na utawala bora na wa sheria, yalishindwa kubuni sheria ya kutawala miili ya watu hususani wanawake hivyo kudhibiti ukahaba, pia michezo hatari kama ndondi na kareti, ikaishia kuhalalisha biashara zinazohusisha ukahaba kwa namna moja au nyingine, tena zikitozwa kodi ya mapato kwa Serikali.
      Hatimaye Mwalimu alitaja kuhusishwa kwa ukahaba katika Maandiko Matakatifu, ambapo makahaba hawakuhukumiwa kwa ukahaba wao, isipokuwa walihimizwa wawe na matendo mema, sawa na walivyohimizwa watu wengine!
      Alitoa mfano wa kahaba aliyemkimbilia Yesu alipokimbizwa na umati uliotaka wamponde mawe mpaka afe kama mila yao inavyoruhusu. Yesu aliuambia ule umati akisema, “Ikiwa miongoni mwenu kuna asiyepata kutenda mnalomtuhumu nalo, na awe wa kwanza kumtupia jiwe!”
      Yesu alishusha macho kuendelea kuchora kielelezo chake, na alipoinua macho sekunde kadhaa baadaye, hakuona mtu hata mmoja! Ndipo alimuamuru kahaba akisema, ‘Inuka uende zako, kawe na matendo mema.’
      “Je,” Mwalimu alimhoji Rwegasira akisema, “Kwani Yesu alishindwa kumtamkia kahaba aache ukahaba?” Hapo ndipo Mwalimu alitaja kahaba mwingine aliyemkuta Yesu mahali akifanyiwa karamu akamuangukia akilia, mpaka alimlowesha miguu na kumpangusa kwa nywele zake, akampaka manukato! Yesu alimuambia mwenyeji wake akisema: “Huyu mwanamke amekuzidi, kwa kuniosha miguu kama ilivyo desturi yetu, ambapo wewe hukufanya vile.”
      Kwa msingi huu, Mwalimu alimtamkia Balozi Joseph Rwegasira akisema: “Kwa kupewa akili na Mwenyezi Mungu, mwanadamu hatahukumiwa kwa dhambi ya mwenziwe, ndipo kwa hali hiyo, litatimilika agizo la Mwenyezi Mungu kuwa, ‘Usihukumu mwenzio, ndipo nawe hutahukumiwa!’
      Maongezi yaliyowezesha kuandikwa makala hii wakati wahusika; Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, na Balozi Joseph Rwegasira walishatangulia mbele ya haki, yalifanywa kati yangu (Mtangazaji Mstaafu Florian Kaiza), na Balozi Rwegasira.
      Tulikutana jijini Beijing China nilikokuwa kwa kazi ya mkataba katika Idhaa ya Kiswahili ya Radio China Kimataifa (CRI), kati ya mwaka 1986 hadi 1993.
      Balozi Rwegasira alikuwa katika msafara wa Mwalimu akiwa Mwenyekiti wa Tume ya Ushirikiano wa Nchi za Kusini.
      Alikwenda China kuukabidhi uongozi wa nchi hiyo, ripoti ya tume ile baada ya kuvunjwa rasmi mwaka 1992.