- Tafuta hifadhi pahali ambapo kuna jumba kubwa au ndani ya gari. Kukiwa na jumba ambalo lina kifaa cha kukinga dhidi ya radi, utakuwa salama zaidi.
- Usiwe katika maeneo ya wazi, au kwenye mlima ulio wazi.
- Iwapo utakosa pahala pa kujikinga mvua, punguza uwezekano wako wa kupigwa kwa kujikunyata na kujifanya mdogo zaidi. Unaweza kuchutama, kuweka mikono yako kwenye magoti na kufichwa kichwa chako ndani.
- Usijikinge mvua chini ya miti.
- Iwapo upo pahala ambapo kuna maji, ondoka na kukwepa maeneo ya ufukweni yaliyo wazi. Utafiti umeonesha kwamba kuwa karibu na maji huongeza hatari ya mtu kupigwa na radi.
- Kwa kuwa radi huwa nguvu za umeme, unafaa kujiepusha na vitu vya chuma vyenye ncha kali ukiwa kwenye mvua.
0 comments:
Chapisha Maoni