HABARI KWA WAKATI KUTOKA HAPA

Tunakuhakikishia kupata habari zote zilizo muhimu kutoka ulimwenguni kote kwa wakati, unaweza kusubscribe mtandao wetu na ukawa unapokea habari zote katika email yako punde tu tuchapishapo machapisho yetu. Jiunge na mitandao yetu ya Facebook na Twitter kutupata kirahisi.

HABARI ZA MICHEZO

Sasa Fichuo tunakuhakikishia kupata taarifa zote za kimichezo kutoka viwanja mbalimbali duniani, lengo ni kuhakikisha hupitwi na lolote katika ulimwengu wa michezo.Jiunge na mitandao yetu ya Facebook na Twitter kutupata kirahisi.

TAARIFA ZA BURUDANI NA HABARI ZA WASANII

Unapenda masuala ya burudani? Ni jukumu letu kuhakikisha unazipata info zote za burudani na wasanii wanaokupa burudani, unapata video mpya, movie pamoja na muziki. Kaa karibu nasi.

KURASA ZA MAGAZETI KILA SIKU

Tunakupatia kila ambacho kinaandikwa katika magazeti ya Tanzania na nje ya Tanzania, usitie shaka ukishindwa kununua gazeti uipendalo, sogea karibu nasi na upate kila unachokihitaji.

MAHUSIANO

Fahamu mambo mengi katika ulimwengu wa mapenzi kwa kupitia dondoo, simulizi na visa mbalimbali kupitia Fichuo Online, Jiunge na mitandao yetu ya Facebook na Twitter kutupata kirahisi.

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo TRACKS. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo TRACKS. Onyesha machapisho yote

Jumamosi, Aprili 01, 2017

YAMOTO BAND-BASI MP3

Kutoka jiko la WCB (Wasafi Classic Baby) mpishi mkali wa muziki mzuri producer Laizer katupikia hii kutoka kwa vijana washereheshaji Yamoto Band, hii ni baada ya maneno mengi kuwa vijana hao wanne wameteekezwa na ni ngumu kuwaona tena katika anga la muziki wa bongo fleva kama walivyokuwa wakitesa awali..wimbo wao mpya katika mahadhi yao huu hapa

NEW TRACK: RAPPER DARASSA AMERUDI NA 'UTANITOA ROHO' IPATE HAPA

Rapper aliyefanikiwa kuumaliza mwaka 2016 vizuri na kuuanza mwaka 2017 kwa nguvu kubwa ya wimbo 'Muziki', Darassa amerudi tena na wimbo mwingine, na hapa katika track yake mpya kaimbia mapenzi akinakshi mistari yake na maneno kutoka kwenye wimbo wa zamani wa dansi.
Darassa aliyewahi kufanya vizuri na wimbo mwingine wa mapenzi 'Kama Utanipenda' inasemekana wimbo huu mpya anaohofia kutolewa roho haujatoka kwa ridhaa yake, ni kama umevuja wakati akiwa kwenye mipango ya kuutangaza rasmi.
Japo kuwa unaweza kusema ni aina ya 'Kick' ameitengeneza ili kurudi kuendeleza ufalme wa 'Muziki' ulioanza kufifia hivi karibuni, lakini kwa aina ya wimbo huu mpya hakika ataendelea kuwa katika vichwa vya wapenzi wengi wa muziki.

Alhamisi, Machi 30, 2017

BAADA YA KANDANDA, RONALDINHO SASA KATIKA MUZIKI, TRACK YAKE IKO HAPA +AUDIO

Staa wa soka na mkongwe wa Klabu ya Barcelona na Timu ya Taifa ya Brazil, Ronaldinho Gaucho ameamua kujitosa kwenye tasnia ya muziki ambapo ameachia wimbo wake wa kwanza alioupa jina la Sozinho.
Wimbo aliouachia Ronaldinho ni wa staili laini Kibrazili ya Samba na tafsri ya Sozinho kwa Kiingereza ni ‘Alone’
Hii sio mara ya kwanza kwa Gaucho kufanya kazi ya muziki, mwaka jana alipata nafasi ya kuimba kwenye mashindano ya Rio Paralympics 2016. 
Licha ya kuachia ngoma hiyo, Gaucho amesema: ‘Asanteni marafiki zangu. Huu ni wimbo wangu wa kwanza, bila kumshirikisha mtu yeyote!!!’
Licha ya kustaafu kucheza soka la ushindani mwaka 2015, Staa huyo wa Samba mwenye umri wa miaka 37 amekuwa akijishughulisha na kazi mbalimbali zikiwemo za muziki.

Jumatatu, Februari 13, 2017

POLISI MKOANI MBEYA WATOA ORODHA YA WAFANYA BIASHARA NA WATUMIAJI WA MADAWA YA KULEVYA +AUDIO

Kufuatia mapambano yanayoendelea nchi nzima dhidi ya watu wanaojihusisha na uuzaji na utumiaji wa dawa za kulevya, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limefanya misako na Mafanikio yaliyopatikana katika Misako ni kama ifuatavyo:-


Mnamo tarehe 11.02.2017 majira ya saa 02:00 usiku, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilifanya misako katika maeneo ya Manga na Nsalaga – Uyole na kukamata watuhumiwa wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya ikiwa ni pamoja na wauzaji, wasambazaji na watumiaji [mateja]. Watuhumiwa waliokamatwa kutokana na kujihusisha ba usambazaji na uuzaji wa dawa za kulevya ambao ni 1. SHABAN RAMADHAN [40] Mkazi wa Uyole 2. RASHID YASIN [35] Mkazi wa Nonde 3. RODA MWAMBERA [60] Mkazi wa Mama John 4. MRISHO RAMADHAN [22] Mkazi wa Airport - Iyela na 5. MUSSA KIMBE [33] Mkazi wa Nonde. 
Watuhumiwa wote wapo mahabusu na mahojiano zaidi yanaendelea ili kubaini mtandao mzima wa watu wanaojihusisha na dawa za kulevya. 
Aidha kufuatia misako iliyofanyika kuanzia tarehe 19.01.2017 hadi tarehe 09.02.2017 katika maeneo mbalimbali Mkoani Mbeya, Watuhumiwa wawili walikamatwa katika matukio mawili tofauti wakiwa na dawa za kulevya. 
Katika msako wa kwanza uliofanyika maeneo ya Ilemi Jijini Mbeya, HENRY MWAMFUPE [19] Mkodishaji Baiskeli na Mkazi wa Ilemi alikamatwa akiwa na kete 03 za dawa za kulevya aina ya Heroine. 
Pia katika msako uliofanyika maeneo ya Mbalizi, ANITHA ABEL [21] Mwanafunzi wa Kidato cha tatu katika shule ya Sekondari Sanani iliyopo Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Songwe na Mkazi wa Mbalizi alikamatwa akiwa na kete 15 za dawa za kulevya aina ya Heroine akiwa nyumbani kwao. 
Mtuhumiwa anaishi na mama yake mzazi aliyefahamika kwa jina la MARTHA MWALINDU ambaye alikimbia baada ya kuwaona askari na inasadikika ndiye muuzaji/msambazaji mkubwa wa dawa hizo za kulevya na huwa anamtumia mtoto wake kuuza na kusambaza. Msako mkali wa kumtafuta mtuhumiwa zinaendelea. 
Watuhumiwa hao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani mara baada ya Upelelezi kukamilika. 
Aidha katika misako mbalimbali iliyofanyika walikamatwa watuhumiwa wanaojihusisha na utumiaji wa dawa za kulevya maarufu kama Mateja ambao ni:- 

1. AYUBU ABDALLAH [42] Mkazi wa Ilomba jijini Mbeya 

2. EMANUEL SIMBEI [43] Mkazi wa Sokomatola 

3. IMAN ABBAS [33] Mkazi wa Majengo 

4. SHABAN SHAIBU [19] Mkazi wa Nonde 

5. KENY SANGA Mkazi wa Sokomatola 

6. PASCHAL PIUS [28] Mkazi wa Itiji 

7. PILIM KAYANGE [20] Mkazi wa Uhindini 

8. ELISHA MWAIHABI [19] Mkazi wa Nonde 

Wengine ni:- 

9. DANIEL KANJANJA [43] Mkazi wa Uhindini 

10. MUSSA KIPESA [37] Mkazi wa Iwambi 

11. CHARLES GERVAS [28] Mkazi wa Nonde 

12. KIMANZI KILONZA [44] Mama John 

13. SHABAN SHAIBU [26] Mkazi wa Nonde 

14. EMANUEL LUCAS [18] Mkazi wa Ilomba 

15. RICHARD GONDWE [40] Mkazi wa Ivumwe 

16. HENRY LEMA [35] Mkazi wa Mama John 

17. RAMADHAN ABBAS [18] Mkazi wa Sae 

18. EDWARD MWASEKA [30] Mkazi wa Majengo 

19. LUSEKELO KIDION [26] Mkazi wa Mwakibete 

20. ALINANUSWE STIVEN [26] Mkazi wa Ilolo 

21. JUSTIN WISTON [23] Mkazi wa Mafiati 

22. MICHAEL KASHILILIKA [20] Mkazi wa Manga 

23. KANI ASANGALWISYE [28] Mkazi wa Ituha. 

Watuhumiwa wapo mahabusu wanaendelea kuhojiwa ili kupata mtandao halisi wa wauzaji na wasambazaji wa dawa za kulevya.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Naibu Kamishina wa Polisi DHAHIRI A. KIDAVASHARI anatoa wito kwa wananchi kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kuwafichua watu na mtandao wa watu wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya ili wakamatwe na hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao. 
Aidha Kamanda KIDAVASHARI anatoa wito kwa wananchi kufanya kazi na kuacha kujihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya kwani inasababisha kupotea kwa nguvu kazi ya taifa na kurudisha nyuma maendeleo ya mtu binafsi na taifa kwa ujumla.

Hapa ni wakati RPC Kidavashari akitoa orodha hiyo;

Jumanne, Agosti 05, 2014

UNAFAHAMU KUWA 'GERE' YA WEUSI NI COPY? ORIGINAL YAKE IKO HAPA, ISIKILIZE AMA ICHUKUE

Story kubwa katika vichwa vya wapenzi wengi wa burudani ya muziki wa kitanzania ni kuhusu Wimbo wa Kundi la Weusi unaitwa "Gere" ambao unadaiwa kuwa ni copy ya wimbo wa Msanii wa HipHop kutoka Cleveland Marekani anayeitwa Machine Gun Kelly na wimbo wake unaitwa Peso amewashirikisha Ma rapa Meek Mill na Pusha T uliotoka mwanzoni mwa mwaka 2013, akizungumzia Ishu Hii Rapper Joh Makini amekanusha na kupiga pasi kwa Mtaarishaji wa wimbo wa Gere Producer Nahreel kwa sababu yeye ndiye aliyehusika kwenye Upishi wa ngoma nzima, kwani wao waliikuta beat imeshatengenezwa. Producer huyo alipohojiwa na Fichuo Tz Blog aliruka futi mia na kudai kuwa tuhuma hizo si za kweli kwasababu kama yeye angekua anatabia mbaya za ku copy midundo ya watu basi. Hebu usikilize hapa halafu fananisha...!


Kama umeshindwa kuudownload na kuusikiliza hapo, basi ingia katika link hii utaupata_____ http://www.audiomack.com/song/ghostzonemedia/machine-gun-kelly-peso-feat-pusha-t-meek-mill

Alhamisi, Juni 12, 2014

SIKILIZA/DOWNLOAD WIMBO MPYA WA DIAMOND-MDOGO MDOGO HAPA

Baada ya purukushani zoooote za tuzo za Afrika Kusini na mishe mishe zote za shows za Marekani, sasa Diamond platnumz amerudi home sweet home Tanzania na kuachia ngoma mpyaaaaaaa inaitwa Mdogo Mdogo na imetambulishwa katika media tofauti pamoja na kuachiwa katika media tofauti na sasa imetua mikononi mwangu nami nakupa kupitia hapa, sasa waweza kuidownload na kuisikiliza pia hapahapa>>>>

Jumapili, Juni 08, 2014

SIKILIZA MANENO YA MTOTO WA MZEE SMALL AKIELEZEA SABABU YA KIFO NA KUHUSU MAZISHI

Msanii mkongwe hapa nchini Said Wangamba maarufu kwa jina la ``Mzee Small` amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Small Wangamba aliyejizolea sifa kwa sanaa ya uigiza huku akijipiga kifua kudhihirisha umwamba pindi anapoigiza na amekuwa ni mtu mwenye misimamo mikali kwa kile asichokihitaji.
Small alizaliwa mwaka 1955 Kilwa na ameacha mke na watoto sita na maziko yake yatafanyika kesho saa kumi jioni katika makaburi ya Tabata Segerea.

Jumapili, Mei 18, 2014

NGOMA MPYA YA ADM NA PNC IKO HAPA 'BASI NJOO' UNAWEZA KUISIKILIZA NA KUIDOWNLOAD HAPA-HAPA

PNC kwa mara nyingine tena ameonesha uwezo wake baada ya kushirikishwa na jamaa kutoka mkoani Mbeya , ADM, ngoma inaitwa basi njoo, chukua time yako kuisikiliza na hautojutia muda wako...ni kutoka studio za Baoda Records pande za Tunduma, Wilayani Momba mkoani Mbeya. unaweza kuidownload pia hapa hapa...

Ijumaa, Mei 16, 2014

UNAWEZA KU'PLAY' HAPA AU KU'DOWNLOAD' WIMBO MPYA WA LINEX MJEDA-ONGA ONGA

Good newz kwa mashabiki wa msanii Linex Sunday Mjeda,  na  mashabiki wote wa muziki wa bongo flava na muziki wa kitanzania kwa ujumla, sasa Linex Sunday mjeda ameachia wimbo mpyaaaaaaaaaaaaa unaitwa 'Onga Onga' no good music kiukweli unaweza kuudownoad na kuusikiliza hapa

Jumatano, Mei 14, 2014

HATIMAYE 'PROKOTO' YA VICTORIA KIMANI FT. OMMY DIMPOZ NA DIAMOND IMETOKA, NI BONGE LA NGOMA, SIKILIZA AU DOWNLOAD HAPA

Baada ya kusubiriwa kwa muda mrefu sana kwa wimbo uliopewa jina la PROKOTO na kupewa promo ya nguvu kupitia vituo vingi vya redio, television, blogs na social networs hatimaye wimbo wa Victoria Kimani aliowashirikisha Diamond na Ommy Dimpoz ‘Prokoto’ umetoka. Wimbo umerekodiwa kwenye studio za Surround Sounds chini ya producer Tudd Thomas. Hapa nimekuwekea wimbo huo usikilize na kuudownload ni bonge langoma aisee

Jumapili, Mei 11, 2014

CHUKUA HAPA WIMBO MPYA WA DIAMOND-KITORONDO, SOMA PIA ALICHOKIANDIKA KUHUSU WIMBO HUO

Kuna wimbo mpya wa Diamond, nikiwa na maana kwamba haujawahi sikika masikioni mwa watu umesambaa tangu jana katika mitandao tofauti, kiukweli hauna quality kabisa, uko hapa unaweza kuusikiliza na kuudownload ukitaka, mwenyewe amedai kuwa haukuwa tayari na kuomba usitumike katika media, namnukuu hapa...
Moja ya nyimbo zangu ambazo ziko store hazija toka nimeikuta mtandaoni na sijui imefikaje, tena ikiwa kwenye mfumo wa Voicenote, yaani haina quality kabisaa... Tafadhari, kwa yoyote atakaeipata Asiitumie kwenye media ama hadhara, kwasababu Haijatoka na haiko Qualified....
Wimbo wenyewe unaweza kuupata hapa...

Jumapili, Aprili 27, 2014

DOWNLOAD/PLAY NGOMA KALI TOKA KWA OBY ONE FT. DON MUSIC & GESTRYDER

Ijumaa, Aprili 25, 2014

Jumatano, Aprili 23, 2014

MCHAKATO WA KUWAPATA WASHINDI KILIMANJARO TANZANIA MUSIC AWARDS 2014 UNAENDELEA



Kampuni ya TBL leo imekutana na wanahabari kuzungumzia mwenendo wa mchakato wa kuwapata washindi wa vipengele vya tuzo za Tanzania - Kilimanjaro Tanzania Music Award (KTMA).

Kilimanjaro Tanzania Music Awards ni tuzo pekee zinazowaenzi wasanii toka aina zote za muziki.
Tuzo hizi hufanyika kila mwaka jijini Dar es Salaam na huwatambua na kuwatunuku wadau wa muziki Tanzania toka mwaka 1999, zilipoanzishwa na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA). Toka wakati huo, tuzo hizi zimekua maradufu na zimedhaminiwa kwa ushirikiano na bia ya Kilimanjaro Premium Lager toka 2003. Zinawakilisha kilele cha maadhimisho ya kalenda ya muziki kitaifa. Washiriki huteuliwa na wananchi pia kamati maalum yenye wadau wanaoufahamu vizuri muziki wa nchini, wasanii hupigiwa kura kwa vipengele kupitia SMS na katika tovuti.
Washindi hawapati kutambulika na nafasi ya kuonekana katika vyombo vya habari tu, bali hushinda zawadi ya fedha taslimu zinazowasaidia kuendeleza muziki wao. Lengo la Kilimanjaro Tanzania Music Awards ni kuwahamasisha wasanii toka sehemu mbalimbali nchini kufikia kilele cha mafanikio ya kimuziki, kwa kutambua kwamba ndoto zao hazishii ngazi ya kitaifa, bali kimataifa pia.

Ijumaa, Machi 28, 2014

J'ODIE ATUPA KETE NYINGINE KATIKA MASIKIO YA MASHABIKI WAKE, NI WIMBO UITWAO SUGAR COCONUT, USIKILIZE NA KUDOWNLOAD HAPA

Mwanamuziki kutoka nchini Nigeria J'odie aliyewika na wimbo Kuch Kuch Baby alioutoa mwaka 2011 na hatimaye kuvuma sana Tanzania mwaka 2013-2014 sasa amekuletea kazi nyingine inaitwa Sugar Coconut, isikilize ama idownload katika link hii https://www.hulkshare.com/search/J'odie Sugar Coconut video.mp3

Video yake nitakuletea punde tu kupitia mtandao wako huu.

Jumatatu, Machi 10, 2014

NAJUA BADO HUJAUPATA WIMBO MPYA WA LANGA VOCOLISER 'PENDANA NA MIMI', UKO HAPA...NI NAFASI YAKO YA KUDOWNLOAD NA KUUSILIZA HAPA

Najua bado hujaupata wimbo huu, tumia dakika zako 3 na sekunde 57 kuusikiliza na kuudown load kupitia link hii https://www.hulkshare.com/fichuo_tz/langa-pendana-na-mimi-prod-by-kesse-touch

Alhamisi, Machi 06, 2014

DOWNLOAD/PLAY USHAHARIBU YA SNURA MUSHI HAPA

Baada ya kupata majanga ya kufungiwa video yake ya Nimevurugwa baada ya kuonekana kukosa maadili  kwa jamii...sasa mwanamuziki na mchezaji filamu nguli katika anga la Bongo movie Snura Mushi sasa ameachia ule wimbo uliokuwa ukisubiriwa sana 'Ushaharibu'.
Kuusikiliza na kudownload ingia katika link http://www.hulkshare.com/hugoline/snura-ushaharibu

Jumatano, Machi 05, 2014

SARAHA NA MARLAW KATIKA WIMBO MPYA, DOWNLOAD NA KUUSIKILIZA HAPA 'KILA NDOTO'

Sasa baada ya kumsikia msanii mkongwe katiga game ya muziki wa bongo flava Bongo, Marlaw katika No Go siku chache zilizopita, ni nafasi nyingine ya kuisikia sauti yake tamu kupitia wimbo alioufanya na nyota mwingine wa muziki wa kizazi kipya mwenye asili ya Sweeden, Mwanadada SaRaha katika wimbo uitwao 'Kila ndoto'.
Kama unauhitaji usikilize na kuuchukua katika link hii, ni bonge la ngoma...    https://soundcloud.com/sarahamusic/kila-ndoto-saraha-ft-marlaw

Jumatatu, Januari 27, 2014

SHILOLE KUIACHIA 'CHUNA BUZI' JANUARI 31, 2014


Jumapili, Januari 26, 2014

USIKILIZE HAPA WIMBO MPYA WA JOSE CHAMELLION NA DAVIDO 'ALL DI GIRLS'