Mzungu huyo ambaye jina tunalihifadhi, alidaiwa kufanya tukio hilo la
kinyama Mei 26, mwaka huu na inadaiwa Aneth alipomkatalia, alimtimua
nyumbani hapo kwa kumtupia virago.
Chanzo makini kilidai kuwa, baada ya kutupiwa virago bila kupewa
mshahara wake sambamba na kipigo, Aneth aliripoti tukio hilo katika
Kituo Kidogo cha Polisi cha Tabata, Dar na muda mfupi polisi walifika
nyumbani hapo lakini Mzungu huyo hakutoka ndani, akakataa kuzungumza
chochote.
Taarifa zilidai kuwa, baada ya polisi kukutana na kizingiti hicho,
walimpigia simu kiongozi wao ambaye aliwaamuru warudi kituoni wajipange
upya.
Akisimulia zaidi ishu hiyo, Aneth alisema polisi walipoondoka eneo
hilo, umati uliochukizwa na kitendo hicho ulikusanyika nje ya nyumba ili
kumdhibiti ‘mtasha’ huyo kwa lolote.
Kuna jirani mmoja alipiga simu tena kituo cha polisi alipoona hali ya hewa imechafuka ndipo polisi wakafika kwa mara nyingine na difenda na kufanikiwa kuingia ndani kwa kutumia geti kubwa, walipofika walikuta milango imefungwa lakini ilisemekana aliruka ukuta na kutimkia kusikojulikana.
Polisi waliniambia nimpigie simu ajisalimishe lakini nilipompigia alisema hayupo na kama tunamhitaji tukutane sehemu huku na yeye akiwa na polisi wake
kilisema chanzo.
Mmiliki wa nyumba hiyo anayeishi Kigamboni, Mr. Cris alipoulizwa
kuhusiana na ishu hiyo, alikiri kupokea malalamiko na manyanyaso kutoka
kwa Aneth.
Akisimulia zaidi maisha anayoishi na Mzungu huyo, Aneth alisema:
Alikuwa akinitafutia sababu za kunitimua kwani hivi karibuni kwa bahati mbaya nilipoteza ufunguo wa ndani, akanipiga mateke na kunisababishia maumivu makali mwilini kiasi cha kushindwa kutembea.
Lakini lililoniuma zaidi ni hili la kunilazimisha eti nifanye mapenzi na mbwa wake, amekuwa akifanya hivyo mara kwa mara mimi nikaona siyo sawa na nilipokataa ndipo yakanikuta hayo.
Aneth aliripoti matukio hayo katika Kituo Kidogo cha Polisi Tabata na
kupewa fomu ya matibabu (PF-3) sambamba na kufunguliwa jalada la kesi
namba TBT/RB/3132/2014/ SHAMBULIO na jalada la uchunguzi lenye namba
TBT/IR/1829/2014/UCHUNGUZI.
0 comments:
Chapisha Maoni