Jumapili, Januari 17, 2016

MWANAMUZIKI MOS DEF ALIVYOTIMULIWA AFRIKA KUSINI

Mwanamuziki mashuhuri kutoka Marekani Mos Def, ambaye anajulikana kwa majina mengine kama Dante Terrell Smith au Yasiin Bey alifikishwa mbele ya mahakama ya Bellville, mjini Cape Town Afrika kusini baada ya kukamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Cape town akitumia stakabadhi zisizofaa,Mayihlome Tshwete, msemaji wa wizara ya mambo ya ndani amesema.
Mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 42 anasemekana kuingia Afrika kusini akitumia pasipoti ya utalii ya Marekani na kisha kujaribu kuondoka akitumia pasipoti nyingine isiyotambulika.Idara ya polisi nchini Afrika kusini imemshtaki Mos Def kwa kosa la kutumia stakabadhi za usafiri za ulaghai.
Aidha uchunguzi zaidi umebaini kuwa mkewe Mos Def amekuwa akiishi Afrika kusini kinyume na sheria baada ya muda wake wa pasi kuisha, Tshwete alisema. Amri imetolewa kwa mama huyo wa watoto wanne kuondoka nchini humo kabla ya siku 14 kuisha.

0 comments:

Chapisha Maoni