Mkurugenzi wa Real Madrid, Jose Angel Sanchez anadai kuwa vilabu kadhaa vya EPL huenda vikakumbwa na adhabu ya kufungiwa kusajili, kama ilivyopewa klabu yake (Telegraph), Real Madrid bado wanataka kumnunua kipa wa Manchester United David de Gea, 25, mwisho wa msimu huu, licha ya adhabu waliyopewa ya kutosajili (Independent), Real Madrid pia wanataka Manchester United wamsajili kiungo Toni Kross, 26, ili wapate fedha za kumsajili Edinson Cavani, 28, kutoka PSG (A Bola), meneja wa zamani wa Manchester United, Sir Aex Ferguson, 74, atakuwa tayari kumsaidia Ryan Giggs, iwapo Louis van Gaal atafukuzwa kazi (People), kocha wa zamani wa Chelsea, Jose Mourinho anaamini atachukua 'mikoba' ya Van Gaal, ndani ya kipindi cha miezi sita, na tayari amewaomba baadhi ya wasaidizi wake wakubali kuungana naye Old Trafford (Sun), Jose Mourinho, 52, alikataa nafasi ya kurejea tena Real Madrid kwa sababu anataka kubakia katika EPL (Times), Liverpool wapo tayari kutoa pauni milioni 25 kumsajili mshambuliaji wa Leicester City Jamie Vardy, 29, mwisho wa msimu (Star), Barcelona walituma 'watambua vipaji' wake kwenda kumtazama beki wa Everton, John Stones siku ya Jumamosi (Mail), Barcelona wana uhakika wa kumsajili kiungo wa Arsenal, Aaron Ramsey, 25, ambaye ni moja ya kipaumbele kwa klabu hiyo mwisho wa msimu (Express), West Brom wanataka kulipwa pauni milioni 7 kwa anayemtaka Callum McManaman, 24, baada ya QPR na Middlesbrough kuanza kumnyatia winga huyo (Telegraph), Sunderland watapanda dau zaidi la pauni milioni 14 kumtaka mchezaji wa Swansea Andre Ayew, 26, baada ya pauni milioni 11 kukataliwa (Express), beki wa zamani wa Arsenal, Ashley Cole, 35, anafikiria kwenda LA Galaxy ya Marekani baada ya kuondoka Roma (LA Times), Chelsea wanamtazama beki wa Crystal Palace, Scott Dann, 28, kuziba nafasi ya nahodha John Terry, 35 (Mirror), Chelsea pia wanamfuatilia kiungo wa Leicester City, Riyad Mahrez, 24 (Star), West Ham wanajiandaa kutoa pauni milioni 10 kumtaka mshambuliaji wa Liverpool, Mario Balotelli, 25, anayecheza kwa mkopo AC Milan (Brentwood Gazette), Swansea wanataka kumfukuza kazi kocha Alan Curtis, baada ya klabu hiyo kuporomoka hadi kwenye ukanda wa kushuka daraja, takriban wiki mbili baada ya kumpa kazi hiyo kufuatia kufukuzwa kwa Gary Monk (Sun), Newcastle wanataka kumchukua mshambuliaji wa Swansea Bafetimbi Gomis, 30 (Mail).
Salim Kikeke
0 comments:
Chapisha Maoni