HABARI zikufikie mpenda burudani kuwa staa anayeunda kundi la P-Square, Peter Okoye hayuko poa kiafya na bado anahitaji maombi.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Peter ambaye pia ni pacha na Paul, alitupia picha akiwa hospitali katika harakati ya kuchukua vipimo kisha akaandika maneno yaliyosomeka;
“Naelekea kuchukua kipimo cha CT Scan leo. Najaribu kuwa mwenye afya kwa asilimia 100. Haikuwa jambo rahisi kuwa katika hali hii ya sasa kwa wiki chache zilizopita. Asanteni sana jamani kwa maombi yenu, nawapenda na muendelee kuniombea.”
Baada ya kuachia picha na maneno hayo, mashabiki wake wengi walijumuika naye kwenye ukurasa wake huo na kumpa pole huku wengine wakimuombea apone haraka.
0 comments:
Chapisha Maoni