Shirika la kimataifa la wahamiaji , IOM limeripoti kuwa jumla ya wahamiaji na wakimbizi 23,664 (1,700 kila siku) walikimbilia bara Uropa kupitia bahari siku 14 za mwanzo wa mwezi wa mwezi Januari mwaka huu.
Hata hivyo shirika hilo lilisema kuwa watu 59 walipoteza maisha yao wakiwa kwenye harakati ya kukimbilia nchi za bara Uropa. Takwimu zilizotolewa na shirika hilo zinaonyesha kuwa Ugiriki iliongoza kwa kupata idadi kubwa zaidi ya wakimbizi 847,084 katika kipindi cha mwaka moja. Takwimu za hivi punde zinaonyesha kuwa wakimbizi 3, 711 walipoteza maisha yao mwaka uliopita katika bahari ya Mediteranea ikilinganishwa na wakimbizi 3,279 waliopoteza maisha yao mwaka wa 2014.
0 comments:
Chapisha Maoni