MHADHIRI wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na mwandishi wa tamthiliya ya “Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe,” Dk. Edwin Semzaba amefariki dunia.
Taarifa kutoka ndani ya familia ya marehemu inasema kuwa, Dk. Semzaba amefariki dunia akiwa amelazwa hospitalini lakini familia hiyo hawajaweka wazi nini chanzo cha kifo cha mtunzi huyo mahiri wa vitabu tanzania.
Dk. Semzaba pia alikuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Umoja wa Waandishi wa Vitabu Tanzania (UWAVITA ).
Jamii ya Watanzania itamkumbuka sana Dk. Edwin Semzaba kwa umahiri wake wa utunzi wa vitabu hasa kitabu cha “Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe” ambacho kilisomwa sana na mpaka sasa kinatumika sana katika kufundishia wanafunzi wa shule za sekondari hapa nchini.
0 comments:
Chapisha Maoni