Baada ya taarifa tuliyokupatia jana kuhusu ajali mbili za mabasi ya abiria zilizotokea katika mikoa ya Tanga na Songwe mabasi ya Lim Safari na New Force yakihusika na kisababisha mauti kwa mtu mmoja, leo tena jumapili machi 4, 2018 ajali mbili zimetokea katika mikoa ya Morogoro na Iringa na kusababisha vifo kwa watu 5.
Katika ajali iliyotokea mkoani Morogoro watu 5 wamefariki na wengine 9 kujeruhiwa baada ya
basi la abiria aina ya New Force kugongana na gari dogo la abiria aina
ya hiace eneo ya Rungemba.
Imethibitika pia kuwa abiria waliofariki ni Jackson Adam, Georgina Aloyce, Revocata lymo, Mangasa Almasi na Witness Leonard.
Imethibitika pia kuwa abiria waliofariki ni Jackson Adam, Georgina Aloyce, Revocata lymo, Mangasa Almasi na Witness Leonard.
Nako mkoani Iringa abiria waliokuwa wakisafiri katika basi la Kampuni ya
Ndenjela lenye namba za usajili T491 CJV lililokuwa likitokea Mbeya
kuelekea Dar es Salaam, wamenusurika kifo baada ya basi hilo kupata
ajali na kupinduka mlima Kitonga. Baadhi ya abiria wamejeruhiwa na hakuna vifo vilivyotokea.
0 comments:
Chapisha Maoni