Mambo yameanza kuibuka baada ya treni ya kubeba abiria iliyokuwa
safarini kutoka Dodoma kwenda Kigoma kupitia Tabora kupata ajali katika
eneo la kijiji cha Mpeta, wilayani Uvinza kaskazini magharibi mwa
Tanzania, taarifa zinasema.
Ajali
hiyo ilisababishwa na kichwa cha treni kuacha njia na mabehewa mawili
kuanguka.
Kaimu
meneja wa wamawasiliano wa Shirika la Reli la Tanzania (TRL) Mohamed
Mapondela alithibitisha kwamba watu watatu wamejeruhiwa.
Utakumbuka pia taarifa za vichwa vya treni ambavyo 'viliokotwa' bandarini Dar es Salaam bila ya mwenyenavyo kufahamika huvku vikiwa na nembo ya TRL baada ya Rais J.P Magufuli kufanya ziara ya kushtukiza bandarini hapo.
Baada ya ziara ile ya Rais J.P Magufuli baadae ikaja taarifa mpya kutoka kwa waziri Prof. Makame Mbarawa ambaye ni waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano akasema kuwa uchunguzi utafanyika na kisha vichwa hivyo vya treni vikibainika kuwa na sifa vitanunuliwa na serikali.
Maswali yaliyozuka baada ya ajali ya hivi juzi ni je, vichwa vile vya treni vimekwisha nunuliwa? Vimenunuliwa vingapi? Vimenunuliwa lini? Vimenunuliwa kwa gharama gani? Vilifavyiwa utafiti na kubainika kuwa ni vizima?
Mwanasiasa Zitto Kabwe, amelizungumzia pia hilo kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter akiitaja kuwa kashfa kubwa
0 comments:
Chapisha Maoni