Jumamosi, Machi 03, 2018

AJALI MBILI ZA MABASI LEO SONGWE NA TANGA

Ajali mbili zimetokea leo katika mikoa ya Songwe na Tanga na kusababisha kifo ch mtu mmoja na majeruhi kadhaa.

Huko mkoani Songwe asubuhi ya leo imetokea ajali iliyohusisha magari mawili, basi la abiria kutoka kampuni ya New Force na gari dogo aina ya Altezza ambapo sababu ya ajali hiyo ikitajwa kuwa ni uzembe wa dereva wa gari hilo dogo aliyehama upande na kuligonga basi hilo akiwa mwendo kasi.
Katika ajali hiyo dereva wa Altezza amefariki katika pahala ilipotokea ajali na mtu mwingine kujeruhiwa vibaya.
Taarifa zaidi ya hali za abiria kutoka katika basi la New Force ni kuwa hakujatokea kifo wala majeruhi wa kutisha zaidi ya migongano midogo.

Nako mkoani Tanga, wilayani Korogwe basi la kampuni ya Lim Safari lenye kufanya safari kati ya Dar es Salaam na Arusha limepata ajali na kusababisha majeruhi kadhaa.
Katika ajali hiyo hakukutokea kifo. Abiria wanaeleza kuwa mwendo wa gari hilo ulikuwa wa kawaida ila wanahisi ilitokea hitiafu iliyopelekea basi hilo kumshinda dereva.

1 comments:

  1. Duhh pole kwa abilia wote ikumbukwe ajali ni popote hivyo ukiona umzm bc ni jambo la kumshukuru allah

    JibuFuta