Jumatano, Aprili 06, 2016

MARAIS JOHN POMBE MAGUFULI WA TANZANIA NA PAUL KAGAME WA RWANDA WAZINDUA DARAJA LA RUSUMO

Marais Kagame na Magufuli wakifungua kituo cha mpakani Rusumo baada ya Rais Magufuli kuwasili mpakani na kukaribishwa kwa nyimbo za mataifa mawili ya Tanzania na Rwanda.
Rais Dkt. John Magufuli akiwa nchini Rwanda akiwa pamoja na Mwenyeji wake rais wa nchi hiyo Paul Kagame wanatarajia pia kufungua daraja la kimataifa la Rusumo.
Baada ya Uzinduzi huu viongozi hao wawili watakwenda Jijini Kigali ambako watakuwa na mazungumzo muhimu pamoja na kuweka shada la maua ya kumbukumbu ya mauaji ya Kimbari yaliyotokea mwaka 1994 nchini humo

0 comments:

Chapisha Maoni