Jumatano, Aprili 06, 2016

ASKARI 500 WALIJIUA MWAKA JANA NCHINI MAREKANI

Takaribani askari 500 wa Jeshi la Marekani walijiua mwaka jana na hivyo kuendeleza mkondo wa idadi kubwa ya wanajeshi wanaojiua nchini humo katika kipindi cha miaka saba iliyopita.
Wizara ya Ulinzi ya Marekani, Pentagon, katika ripoti yake ya Ijumaa ilisema askari 265 walio katika vikosi vya anga, bahari, nchi kavu na kikosi cha marine walijiua mwaka 2015. Aidha askari 210 wa ziada katika jeshi la Marekani walijiua mwaka jana.
Mwaka 2001 wanajeshi 145 walijiua katika Jeshi la Marekani na idadi hiyo imekuwa ikiongezeka kila mwaka.
Msemaji wa Pentagon Luteni Kanali Hermes Gabrielle amesema kuzuia vitendo vya wanajeshi kujiua ni suala linalopewa kipaumbele na Jeshi la Marekani.
Kitendo cha Marekani cha kuzikalia kwa mabavu Iraq na Afghanistan na harakati zake za kichokozi kwingineko duniani si tu zimeleta madhara na hasara kubwa kwa nchi zinazolengwa, lakini zimesababisha pia matatizo makubwa ya kiroho, kinafsi na kisaikolojia kwa wanajeshi vamizi wa Marekani na bila shaka madhara hayo yatadumu kwa muda mrefu kwa wanajeshi hao na kwa jamii nzima ya Marekani.

0 comments:

Chapisha Maoni