Kuogelea baharini kunaongeza kwa
kiwango kikubwa kuwa na matatizo ya tumbo , kuumwa na masikio na
magonjwa mengine , watafiti wamebaini.
Chuo kikuu cha matibabu cha Exeter na kituo cha Ekolojia na maji ardhini kilifanya utafiti huo.
Ulibaini kwamba uwezo wa muogeleaji wa baharini kuwa na tatizo la
masikio uko juu ikilinganishwa na waogeleaji wa maeneo mengine huku
matatizo ya tumbo pia yakipanda hadi asilimia 29.
Mbali na kuogelea, hatari hizo pia zinashirikisha michezo ya baharini kama vile kuteleza kwa ubao katika mawimbi.
Watafiti waliangazia tafiti 19 zinazohusiana na uogeleaji wa
baharini na magonjwa kutoka Uingereza , Marekani, Australia, New Zealnd ,
Denmark na Norway.
Watachanganua matokeo kutoka kwa zaidi ya watu 120,000.
''Katika
mataifa yalio na wafanyikazi wenye mapato makubwa kama vile Uingereza,
kuna dhana kwamba hatari za kuogelea baharini ni chache mno'', alisema
Dkt Anne Leonard.Hatahivyo magazeti yetu yanaonyesha kuwa kuogelea
baharini hakuongezi uwezekano wa kuugua, kama vile kuumwa na masikio
mbali na matatizo yanayohusisha tumbo kama vile kuumwa na tumbo na
kuendesha.
Tunadhani kwamba hii inamaanisha kwamba uchafuzi wa
mazingira bado ni swala tete linalowaathiri waogeleaji katika mataifa
tajiri duniani.
Mtafiti mshauri Dkt. Will Gaze alisema: Hatutaki
kuwazuia watu kwenda baharini, swala ambalo lina manufaa mengi ya kiafya
kama vile kuimarisha maungo.Hatahivyo ni muhimu kwamba watu wanajua
athari zake ili waweze kufanya uamuzi.
Dkt Gaze amesema kwamba
watu wengi hupona magonjwa hayo bila kupata tiba yoyote lakini yanaweza
kuwa mabaya kwa watu wasio na kinga nzuri kama vile watu wazee na
watoto.
Aliongezea: Tumetoka mbali sana katika kusafisha maji
yetu, lakini ushahidi tulionao unaonyesha kuna kazi kubwa ya
kufanywa.Tunatumai utafiti huu utachangia juhudu zaidi kusafisha pwani
zetu.
BBC
BBC
0 comments:
Chapisha Maoni