Mkurugenzi wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP, Bw. Erik Solheim amesema eneo la Pembe ya Afrika linaweza kuwa kitovu cha mapigano makubwa wakati athari za mabadiliko ya hali ya hewa zikiongeza ugumu wa kutafuta malisho na maji.
Akizungumza wakati wa maonyesho ya filamu ya "A Climate for Conflict" jijini Nairobi, Kenya, Solheim amesema kuongezeka kwa joto duniani kitakuwa chanzo kikuu cha mapigano ya wenyewe kwa wenyewe, ugaidi, na kuhama kwa lazima katika eneo kubwa la Pembe ya Afrika.
Bw. Solheim amesema, uhusiano kati ya mabadiliko ya hali ya hewa na ukosefu wa usalama utajadiliwa kwa kina katika mazungumzo ya mabadiliko ya hewa yatakayofanyika hivi karibuni.
Pembe ya Afrika ni ipi?
Pembe la Afrika ni jina la sehemu ya mashariki kabisa ya bara la Afrika yenye umbo la pembetatu; ni kama rasi iliyoko kati ya Ghuba ya Aden na Bahari Hindi yenyewe.
Eneo hili linajumuisha nchi za leo za Somalia na Jibuti pamoja na sehemu ya mashariki ya Ethiopia; wakati mwingine Ethiopia yote pamoja na Eritrea huhesabiwa humo.
Nchani mwa pembe iko Puntland iliyotangaza uhuru wake lakini inahesabiwa kama sehemu ya Somalia na mataifa mengi, jirani yake ni Somaliland ambayo ni pia sehemu ya Somalia iliyotangaza uhuru wake.
Kwa kutumia wazo la pembe la Afrika kubwa kuna eneo la 2,000,000 km² linalokaliwa na wakazi milioni 94.2 million (Ethiopia: milioni 79, Somalia: milioni 10, Eritrea: milioni 4.5 na Jibuti: milioni 0.7).
0 comments:
Chapisha Maoni