Jumatatu, Oktoba 09, 2017

PETER CROUCH KAINGIZWA KATIKA REKODI ZA DUNIA ZA KITABU CHA GUINNESS

Mshambuliaji wa klabu ya Stoke ya England Peter Crouch ameingizwa kwenye kitabu cha rekodi za dunia cha Guinness World Records cha mwaka 2018 kwa kufunga mabao mengi zaidi kwa kichwa Ligi ya Premia.
Crouch amefunga mabao 51 kwa kichwa katika ligi hiyo, mabao matano zaidi ya mchezaji wa zamani wa Blackburn na Newcastle Alan Shearer.
Crouch, 36, kwa jumla amefunga mabao 105 Ligi Kuu ya England katika mechi 436 alizochezea jumla ya klabu sita ligi hiyo.
"Iwapo wewe ni mshambuliaji wa kati, unafaa kuwa eneo la hatari, tayari kufunga bao kwa kichwa," amesema Crouch.
"Hivi ndivyo nimekuwa nikicheza na hilo sitawahi kulibadilisha. Washambuliaji wa kati wakaokaa nje ya eneo la hatari hunishangaza sana, siwezi kuelewa huwa wanafikiria nini."
Crouch alifunga bao la ushindi mechi ya karibuni zaidi ya Stoke walipocheza dhidi ya Southampton.

0 comments:

Chapisha Maoni