Jumanne, Oktoba 10, 2017

VIJIJI NDILO ENEO MUHIMU ZAIDI KWA UKUAJI WA UCHUMI

Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa FAO jana lilitoa ripoti ikisema, katika miongo kadhaa ijayo kama sehemu za vijijini katika nchi zinazoendelea zikiweza kutimiza maendeleo yenye uwiano na uzalishaji wa chakula na viwanda vinavyohusika, uchumi wa nchi hizo utaweza kukua kwa kasi, na kutoa nafasi za ajira kwa mamilioni ya vijana.
Ripoti hiyo kuhusu hali ya chakula na kilimo kwa mwaka 2017 imeeleza kuwa, eneo la vijiji linahitaji kufanyiwa mageuzi kamili ili kuchochea maendeleo, na kukidhi mahitaji ya chakula na ajira kwa vijana na idadi kubwa ya watu inayoendelea kuongezeka.
Ripoti pia inaona kuwa, sera madhubuti na uwekezaji kwenye mfumo wa chakula vijijini, pamoja na uungaji mkono kwa sekta za kilimo zenye uhusiano wa karibu na maeneo ya miji haswa miji midogo na ya ukubwa wa kati, vitachangia kuongeza ajira, na kuwafanya watu wengi zaidi kubaki vijijini.

0 comments:

Chapisha Maoni