Leo tunakufichulia ajira 10 ambazo husababisha msongo zaidi wa mawazo (STRESS). Kutokana na matamanio ya wengi kuona watu fulani wamefanikiwa kupitia shughuli wanazozifanya..kumekuwa na ombwe kubwa la watu wakitaka kufanya shughuli hizo pasi kujali changamoto ambazo ziko ndani ya ajira/shughuli hizo.
Ziko ajira nyingi zenye hatari, ambazo kutokana na changamoto zake watu wanaozifanya shughuli hizo hujikuta wakiishia kupata msongo mkubwa wa mawazo, kunawengine huishia kukata tamaa na kujiuzulu kufanya hizo kazi ama kuzifanya bila raha.
Hapa tunakuletea aina 10 za ajira zenye kuleta zaidi msongo wa mawazo;
10. Utangazaji wa Redio na Tv kwa kiasi cha 47.93%
Hii ni kutokana na changamoto za kazi yenyewe. Watangazaji wamekuwa wakiwindwa sana na maadui wa tasnia yao ambao wamekuwa wakiumbuliwa na matangazo yanayorushwa katika Redio na Tv. Wapo wanaouawa, wapo wanaofungwa magerezani na hata wanao vamiwa na kushambuliwa.
9. Udereva wa TAXI kwa 48.18%
Hii unaambiwa nayo ni kazi yenye changamoto kwa kiasi cha 48.18%. Hii ni kwa mujibu wa jarida la Forbes ambalo liliangalia haswa changamoto za wateja wanaokodi magari, ziko za ulevi,lugha za kigeni na uhalifu.
8. Uafisa mahusiano kwa 48.50%
Mara nyingi hawa ndiyo wenye dhamana na taswira za makampuni kwa wahudumiwa. Iwapo kampuni itaenda mrama au itakutana na kashfa basi hawa ndio hupata kazi ngumu ya kuisafisha kambuni na ndio maana kazi yao inashika nafasi ya 8 kwa kusababisha msongo wa mawazo.
7. Mkurugenzi Mtendaji kwa 48.56%
Huyu huwa ndio kiongozi wa ngazi ya juu katika kambuni, anajukumu kubwa la kuifanya kampuni ifanye kazi vile inavyotakiwa, hutu huyu hutakiwa kutumia akili nyingi sana kubuni na kupanga mikakati ya kuifanikisha kampuni.
6. Uandishi wa Habari wa Magazetini kwa 49.90%
Hii sababu zake hazitofautiani sana na hatari zilizopo hapo juu katika no. 10 ya Utangazaji wa Redio na Tv, isipokuwa kwa upande wa magazeti waandishi huwa hatarini sana kutokana na uwapo wa nafasi kubwa ya kutoa maoni yao au taarifa kwa urefu.
5. Uandaaji wa Matukio kwa 51.15%
Hapa napo zipo changamoto nyingi kwa wahusika, tufafahamu nguvu kubwa ya kuandaa matukio, hofu kubwa ni je, vipi tukio unaloandaa likifeli? Hapo ndipo unapata stress!
4. Uaskari kwa 51.64%
Sote tunafahamu changamoto ya kusimamia masuala ya ulinzi na usalama, kila siku kunaripotiwa kutokea kwa visa vidogo na vikubwa vya uhalifu. Askari ndio watu tuwategeao kwa kiasi kikubwa kuyadhibiti haya, sio Tanzania tu, hata mataifa mengine ulimwenguni.
3. Urubani kwa 60.54%
Ni kazi ambayo hutumia akili nyingi na inahitaji utimamu wa akili na mwili kiafya. Urubani ni masuala ya kihesabu sana, unaruka kwa makadirio ya namba kitaalamu tofauti na udereva wa barabarani. Vipi ukizikosea hesabu zako au kukiwa na hali mbaya ya hewa huko angani? Najua umefahamu kiwango cha stress kinachotoka hapa.
2. Zima Moto kwa 72.68%
Inawezekana kwa hapa kwetu Tanzania hatujakutana na visa vikali vya moto, lakini kwa wenzetu metaifa mengine imekuwa kawaida kwao kupambana na matukio haya, hugharimu muda, nguvu, akili na pesa za uwezeshaji wa shughuli zenyewe.
1. Wapiganaji wa Vita kwa 72.74%
Hapa bila shaka tutakubaliana, hakuna asiyeijua hatari ya vita. Aendaye vitani kuna mambo matatu; Unusurike, upate ulemavu au upoteze maisha kabisa!
0 comments:
Chapisha Maoni