HABARI KWA WAKATI KUTOKA HAPA

Tunakuhakikishia kupata habari zote zilizo muhimu kutoka ulimwenguni kote kwa wakati, unaweza kusubscribe mtandao wetu na ukawa unapokea habari zote katika email yako punde tu tuchapishapo machapisho yetu. Jiunge na mitandao yetu ya Facebook na Twitter kutupata kirahisi.

HABARI ZA MICHEZO

Sasa Fichuo tunakuhakikishia kupata taarifa zote za kimichezo kutoka viwanja mbalimbali duniani, lengo ni kuhakikisha hupitwi na lolote katika ulimwengu wa michezo.Jiunge na mitandao yetu ya Facebook na Twitter kutupata kirahisi.

TAARIFA ZA BURUDANI NA HABARI ZA WASANII

Unapenda masuala ya burudani? Ni jukumu letu kuhakikisha unazipata info zote za burudani na wasanii wanaokupa burudani, unapata video mpya, movie pamoja na muziki. Kaa karibu nasi.

KURASA ZA MAGAZETI KILA SIKU

Tunakupatia kila ambacho kinaandikwa katika magazeti ya Tanzania na nje ya Tanzania, usitie shaka ukishindwa kununua gazeti uipendalo, sogea karibu nasi na upate kila unachokihitaji.

MAHUSIANO

Fahamu mambo mengi katika ulimwengu wa mapenzi kwa kupitia dondoo, simulizi na visa mbalimbali kupitia Fichuo Online, Jiunge na mitandao yetu ya Facebook na Twitter kutupata kirahisi.

Jumanne, Machi 13, 2018

GARI LA MIZIGO LACHOMWA MOTO BAADA YA KUMGONGA MUUGUZI NA KUMSABABISHIA KIFO

Kundi la watu limechoma gari la mizigo baada ya dereva wake kumgonga na kufa papo hapo muuguzi wa Zahanati ya Kaseme wilayani Geita.
Tukio hilo limetokea Jana usiku katika Kijiji cha Kaseme wakati marehemu huyo akiwa katika Bodaboda pamoja na watoto wake wawili, mmoja amefahamika kwa jina Paulo Tarafa mwenye miaka 3 na mwingine mchanga wa miezi miwili ambao wao wamenusurika na kifo hicho.
Mashuhuda wa tukio hilo wamesema lori hilo lilikuwa kwenye mwendo kasi na walipojaribu kupishana na gari jingine ndipo likawagonga na mama huyo kuumia kuanzia sehemu ya kiuno hadi miguuni na kusababisha utumbo kutoka nje.
Wamesema sababu kubwa iliyochangia watoto hao kutopatwa na madhara kama marehemu mama yao ni kwa kuwa alikuwa amewapakata kifuani ambako hawakuguswa na gari hilo.
Jina la marehemu ni Martha Paulo ambaye mwili wake umehifadhiwa katika chumba cha maiti kwenye Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Geita.

AZAM TV

NJIA 6 ZA KUJIKINGA NA RADI


    1. Tafuta hifadhi pahali ambapo kuna jumba kubwa au ndani ya gari. Kukiwa na jumba ambalo lina kifaa cha kukinga dhidi ya radi, utakuwa salama zaidi.
    2. Usiwe katika maeneo ya wazi, au kwenye mlima ulio wazi.
    3. Iwapo utakosa pahala pa kujikinga mvua, punguza uwezekano wako wa kupigwa kwa kujikunyata na kujifanya mdogo zaidi. Unaweza kuchutama, kuweka mikono yako kwenye magoti na kufichwa kichwa chako ndani.
    4. Usijikinge mvua chini ya miti.
    5. Iwapo upo pahala ambapo kuna maji, ondoka na kukwepa maeneo ya ufukweni yaliyo wazi. Utafiti umeonesha kwamba kuwa karibu na maji huongeza hatari ya mtu kupigwa na radi.
    6. Kwa kuwa radi huwa nguvu za umeme, unafaa kujiepusha na vitu vya chuma vyenye ncha kali ukiwa kwenye mvua.

      Jumatatu, Machi 05, 2018

      75% YA WANAOACHA KAZI HUACHA SABABU YA 'MABOSS' WAO

      Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na watafiti kutoka shirika la kazi ulimwenguni ILO imebainika kuwa asilimia kubwa ya waajiriwa wanaoziacha kazi zao walikoajiriwa huacha kazi huwa sababu halisi ni 'maboss' wao.
      Tunaambiwa kuwa 75% ya waajiriwa anaojiuzulu nafasi zao katika ajira ni wale wenye matatizo mbalimbali na viongozi wao kwenye mashirika, na 25% inayosalia pekee ni wale wanaoacha kazi zao kwa sababu nyinginezo.
      Mashirika mengi kutokana na ukubwa wake au majina yaliyokuzwa na huduma zitolewazo hapo huvutia watu wengi kutaka kufanya kazi ndani yake lakini punde wajiungapo na mashirika yenyewe hukutana na visanga vya 'maboss' wao. Sasa kumbe kuna mambo mawili hapa, suala la kupata ajira ni moja na kupata viongozi wazuri ni sababu nyingine.
      Lakini hili linatuonesha mambo mawili makubwa; Kwanza inaonesha dhahiri kuwa viongozi ndiyo huharibu picha nzuri ya taasisi na ni hao hao hufanya mahala pa kazi pasiwe salama kwa wafanya kazi.

      Jumapili, Machi 04, 2018

      AJALI NYINGINE MBILI MBAYA ZA MABASI ZILIZOTOKEA LEO NA KUUA. (+PICHA)

      Baada ya taarifa tuliyokupatia jana kuhusu ajali mbili za mabasi ya abiria zilizotokea katika mikoa ya Tanga na Songwe mabasi ya Lim Safari na New Force yakihusika na kisababisha mauti kwa mtu mmoja, leo tena jumapili machi 4, 2018 ajali mbili zimetokea katika mikoa ya Morogoro na Iringa na kusababisha vifo kwa watu 5.
       
       
       
      Katika ajali iliyotokea mkoani Morogoro  watu 5 wamefariki na wengine 9 kujeruhiwa baada ya basi la abiria aina ya New Force kugongana na gari dogo la abiria aina ya hiace eneo ya Rungemba.
      Imethibitika pia kuwa abiria waliofariki ni Jackson Adam, Georgina Aloyce, Revocata lymo, Mangasa Almasi na Witness Leonard.
      Nako mkoani Iringa abiria waliokuwa wakisafiri katika basi la Kampuni ya Ndenjela lenye namba za usajili T491 CJV lililokuwa likitokea Mbeya kuelekea Dar es Salaam, wamenusurika kifo baada ya basi hilo kupata ajali na kupinduka mlima Kitonga. Baadhi ya abiria wamejeruhiwa na hakuna vifo vilivyotokea.

      Jumamosi, Machi 03, 2018

      TRENI ILIYOPATA AJALI UVINZA ILISABABISHWA NA KICHWA 'KILICHOOKOTWA' BANDARINI!!!???

      Mambo yameanza kuibuka baada ya treni ya kubeba abiria iliyokuwa safarini kutoka Dodoma kwenda Kigoma kupitia Tabora kupata ajali katika eneo la kijiji cha Mpeta, wilayani Uvinza kaskazini magharibi mwa Tanzania, taarifa zinasema.
      Ajali hiyo ilisababishwa na kichwa cha treni kuacha njia na mabehewa mawili kuanguka.
      Kaimu meneja wa wamawasiliano wa Shirika la Reli la Tanzania (TRL) Mohamed Mapondela alithibitisha kwamba watu watatu wamejeruhiwa.
      Utakumbuka pia taarifa za vichwa vya treni ambavyo 'viliokotwa' bandarini Dar es Salaam bila ya mwenyenavyo kufahamika huvku vikiwa na nembo ya TRL baada ya Rais J.P Magufuli kufanya ziara ya kushtukiza bandarini hapo.
      Baada ya ziara ile ya Rais J.P Magufuli baadae ikaja taarifa mpya kutoka kwa waziri Prof. Makame Mbarawa ambaye ni waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano akasema kuwa uchunguzi utafanyika na kisha vichwa hivyo vya treni vikibainika kuwa na sifa vitanunuliwa na serikali.
      Maswali yaliyozuka baada ya ajali ya hivi juzi ni je, vichwa vile vya treni vimekwisha nunuliwa? Vimenunuliwa vingapi? Vimenunuliwa lini? Vimenunuliwa kwa gharama gani? Vilifavyiwa utafiti na kubainika kuwa ni vizima?
      Mwanasiasa Zitto Kabwe, amelizungumzia pia hilo kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter akiitaja kuwa kashfa kubwa

      AJALI MBILI ZA MABASI LEO SONGWE NA TANGA

      Ajali mbili zimetokea leo katika mikoa ya Songwe na Tanga na kusababisha kifo ch mtu mmoja na majeruhi kadhaa.

      Huko mkoani Songwe asubuhi ya leo imetokea ajali iliyohusisha magari mawili, basi la abiria kutoka kampuni ya New Force na gari dogo aina ya Altezza ambapo sababu ya ajali hiyo ikitajwa kuwa ni uzembe wa dereva wa gari hilo dogo aliyehama upande na kuligonga basi hilo akiwa mwendo kasi.
      Katika ajali hiyo dereva wa Altezza amefariki katika pahala ilipotokea ajali na mtu mwingine kujeruhiwa vibaya.
      Taarifa zaidi ya hali za abiria kutoka katika basi la New Force ni kuwa hakujatokea kifo wala majeruhi wa kutisha zaidi ya migongano midogo.

      Nako mkoani Tanga, wilayani Korogwe basi la kampuni ya Lim Safari lenye kufanya safari kati ya Dar es Salaam na Arusha limepata ajali na kusababisha majeruhi kadhaa.
      Katika ajali hiyo hakukutokea kifo. Abiria wanaeleza kuwa mwendo wa gari hilo ulikuwa wa kawaida ila wanahisi ilitokea hitiafu iliyopelekea basi hilo kumshinda dereva.

      Jumanne, Februari 27, 2018

      UNAAMBIWA KUOGELEA BAHARINI KUNASABABISHA MAGONJWA!!!

      Kuogelea baharini kunaongeza kwa kiwango kikubwa kuwa na matatizo ya tumbo , kuumwa na masikio na magonjwa mengine , watafiti wamebaini.
      Chuo kikuu cha matibabu cha Exeter na kituo cha Ekolojia na maji ardhini kilifanya utafiti huo.
      Ulibaini kwamba uwezo wa muogeleaji wa baharini kuwa na tatizo la masikio uko juu ikilinganishwa na waogeleaji wa maeneo mengine huku matatizo ya tumbo pia yakipanda hadi asilimia 29.

      Mbali na kuogelea, hatari hizo pia zinashirikisha michezo ya baharini kama vile kuteleza kwa ubao katika mawimbi.
      Watafiti waliangazia tafiti 19 zinazohusiana na uogeleaji wa baharini na magonjwa kutoka Uingereza , Marekani, Australia, New Zealnd , Denmark na Norway.
      Watachanganua matokeo kutoka kwa zaidi ya watu 120,000.
      ''Katika mataifa yalio na wafanyikazi wenye mapato makubwa kama vile Uingereza, kuna dhana kwamba hatari za kuogelea baharini ni chache mno'', alisema Dkt Anne Leonard.Hatahivyo magazeti yetu yanaonyesha kuwa kuogelea baharini hakuongezi uwezekano wa kuugua, kama vile kuumwa na masikio mbali na matatizo yanayohusisha tumbo kama vile kuumwa na tumbo na kuendesha.
      Tunadhani kwamba hii inamaanisha kwamba uchafuzi wa mazingira bado ni swala tete linalowaathiri waogeleaji katika mataifa tajiri duniani.
      Mtafiti mshauri Dkt. Will Gaze alisema: Hatutaki kuwazuia watu kwenda baharini, swala ambalo lina manufaa mengi ya kiafya kama vile kuimarisha maungo.Hatahivyo ni muhimu kwamba watu wanajua athari zake ili waweze kufanya uamuzi.
      Dkt Gaze amesema kwamba watu wengi hupona magonjwa hayo bila kupata tiba yoyote lakini yanaweza kuwa mabaya kwa watu wasio na kinga nzuri kama vile watu wazee na watoto.
      Aliongezea: Tumetoka mbali sana katika kusafisha maji yetu, lakini ushahidi tulionao unaonyesha kuna kazi kubwa ya kufanywa.Tunatumai utafiti huu utachangia juhudu zaidi kusafisha pwani zetu.

      BBC

      Jumatatu, Februari 26, 2018

      NUKUU 6 ZA TUNDU LISSU BAADA YA HUKUMU YA JOSEPH MBILINYI (SUGU) NA EMMANUEL MASONGA

      Jana mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi, Sugu (Chadema)  na mwenzake Katibu wa Chadema Kanda ya Nyasa Emmanuel Masonga walihukumiwa kifungo jela miezi mitano kila mmoja.
      Wawili hao walikuwa wameshtakiwa kwa kosa la kutumia lugha ya dhihaka dhidi ya Rais John Magufuli.

      Wanadaiwa kutenda kosa hilo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika mwezi Desemba 31, 2017 jijini Mbeya.
      Hukumu dhidi yao imetolewa na Mahakama ya hakimu mkazi jijini Mbeya.
      Hati ya mashtaka imesema maneno waliyoyatamka yalienda kinyume na Sehemu 89(1) a ya Sheria za Jinai ambayo inaharamisha kutumiwa kwa lugha ya matusi. Maneno hayo, hati za mashtaka zinasema, yangeweza kusababisha uvunjifu wa amani.
      Image result for SUGU MAHAKAMANI
      Baada ya hukumu hiyo ya jana, mnadhimu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni na mwanasheria mkuu wa chama hicho (Chadema) Tundu Lissu ametoa maneno yake na hapa tunakupatia nukuu 6 za mwanasiasa huyo ambaye pia ni rais wa TLS aliyeko nchini Ubelgiji kwaajili ya matibabu baada ya kushambuliwa na risasi.
      Kwanza, hukumu ya leo (jana) sio mwisho wa mjadala mahakamani. Bado kuna fursa, nay haki, ya rufaa High Court na, ikibidi, Court of Appeal.
      Pili, hukumu ya leo haina maana Sugu atakaa gerezani muda wote huo. Kuna haki ya dhamana pending appeal. Ndivyo ambavyo tumefanya kwa viongozi na wanachama wetu wengi in the past. 
      Tatu, hukumu ya leo haina athari yoyote kwa ubunge wa Sugu. Katiba inaweka masharti ya kifungo cha miezi sita au zaidi, na kwa makosa ya 'utovu wa uaminifu.' Uchochezi au kutoa lugha ya matusi sio makosa ya utovu wa uaminifu. 
      Nne, pamoja na kwamba sijaona nakala ya hukumu, adhabu ya kifungo bila faini kwa kosa la kwanza ni kinyume na sentencing principles. Hii ni mojawapo ya hoja zetu zilizoshinda katika kesi ya Mh. Juakali High Court mwaka jana. 
      Tano, hata kama atakaa gerezani muda wote huo, hukumu za kesi za kisiasa kama hii hazijawahi kuwapunguzia heshima wapigania haki popote pale duniani. 
      On the contrary, kifungo cha aina hii ni beji ya heshima kwa kila mpigania haki na uhuru. Orodha ya mifano ni ndefu sana: Nyerere (ijapokuwa yeye alilipa faini), Kenyatta, Mandela, Mugabe, Fidel Castro, etc. 
      Alichokifanya hakimu leo ni kuwaongeza Sugu na Masonga kwenye orodha hii ya heshima. They'll come out even bigger and stronger than when they went in. 
      Sita, naunga mkono pendekezo la Mh. Zitto kwamba wabunge wetu wote warekodi maneno aliyofungiwa nayo Sugu na kuyaweka mitandaoni ili watukamate na sisi pia. 
      Instead of agonising, let's organise and make this issue bigger and bigger mpaka wakimbie wenyewe au watukamate na kutufunga wote. 
      Na sio wabunge tu, tuhamasishe kila mwanachama wetu na kila anayechukizwa na uonevu huu ayarudie maneno haya ili nao wakamatwe na kufungwa. 
      Tumlazimishe Magufuli na watu wake waamue: waigeuze nchi nzima kuwa gereza moja kubwa, au akubali kusemwa kwa maneno na lugha asiyoipenda. Hiyo ndio maana pekee ya freedom of speech in a democracy.

      UTAMADUNI WA KUCHEZA UTUPU MSIBANI CHINA UNAZIDI KUSHIKA KASI

      Muziki unacheza kwa sauti, wacheza utupu wakicheza densi na umati ukishangilia. Katika sehemu zingine huko China hili ndilo unaweza kuliona wakati wa mazishi.
      Mapema mwaka huu, China alianza tena kuwakamata wacheza utupu wanaocheza densi kwenye mazishi, harusi na kwenye mahekalu.
      Hio sio mara ya kwanza mamlaka zimejaribu kuzuia tabia hizo lakini bado hazijanafikiwa

      Related image

      Mbona watu huwaajiri wacheza utupu?

      Wacheza utupu hutumiwa kuwavutia watu wnaaohudhuria mazishi kwa sababu uwepo wa watu wengi kwenye mazishi huonekana kama heshima kwa marehemu. Imani nyingine zinasema kuwa suala hilo na la kuabudu.
      Imani nyingi ni ile kuwa kuwaajiri wacheza utupu kunaweza kuonekana kama ishara ya utajiri.
      Maeneo ya vijijini nchini China ndiyo yenya tabia ya kutumia pesa nyingi hata kuliko mapata, kuwalipa wuigizaji, waimbaji, wachekeshaji na wacheza utupu kuwatumbuiza wale waliofiwa.

      Image result for Pole dancers ON FUNERALS

      Shughuli hii ni maarufu?

      Tamaduni hiyo inapatikana sana maeneo ya vijijini ya China na ni maarufu zaidi nchini Taiwan ambapo ilianzia.
      "Tamaduni hii ya wacheza utupu kwenye mazishi kwanza lilipata umaarufu nchini Taiwan mwaka 1980," msomi wa chuo cha South Carolina Marc Moskowitz aliiambia BBC.
      Tamaduni hii imepata umaarufu nchini Taiwan lakini nchini China serikali imeizuia na watu wengi hawafahamu kuihusu.


      BBC

      Jumapili, Februari 25, 2018

      WATU WANAOSHEREHEKEA SIKUKUU YA CHRISTMAS MWEZI FEBRUARI

      Wanakijiji wanasema kuwa utamaduni huu ambao ulianza enzi za utumwa wakati mababu zao walipozuiwa kusherehekea Krismasi tarehe 24 Desemba kama ilivyo kawaida kwa madhehebu mengi ya Kikristo.
      Badala yake waliamua kuchagua katikati mwa mwezi wa Februari na utamaduni huu umeendelea tangu wakati huo.
      Fataki, muziki na densi huwa sehemu ya sherehe hizo za kuvutia.
      "Watu waliotufanya watumwa walisherehekea Krismas Desemba na hatukuruhusiwa kuwa na mapumziko siku hiyo, lakini tukaambiwa tuchague siku nyingine," alisema, Holmes Larrahondo, mratibu wa sherehe.
      "Katika jamii yetu tunaamini kwamba mwanamke anapaswa kufunga siku 45 baada ya kujifungua, kwa hivyo tunasherehekea Krismas sio mwezi Disemba, bali Februari, kwa hiyo Maria anaweza kudensi pamoja nasi," aliongeza Bw Larrahondo.

      Balmores Viafara, mwalimu mwenye umri wa miaka 53 aliliambia shirika la habari la Ufaransa AFP kwamba kutokana na hilo kwake tarehe 24 Disemba "ni kama siku nyingine yoyote ile ".
      Wakati wa kuabudu, sherehe hizo huitwa "sherehe za kutoa heshma kwa Mungu wetu kwa namna yetu."
      Kama sehemu ya sherehe hizi, wanakijiji hutembelea nyumba mbali mbali "wakimtafuta mtoto Yesu", ambaye huwakilishwa na sanamu ya mbao ambayo hutunzwa na mmoja wa wanavijiji katika nyumbani kwake kwa kwa kipindi cha mwaka kilichosalia.

      Pale sanamu inapopatikana, hutembezwa kijijini na wakazi wa rika zote waliovalia kama malaika na wanajeshi.
      Wacheza densi, hucheza densi inayoitwa fuga; ambapo hucheza wakiigiza hatua za watumwa waliofungwa minyororo.
      Sherehe humalizika majira ya asubuhi mapema.