Jumatatu, Februari 26, 2018

NUKUU 6 ZA TUNDU LISSU BAADA YA HUKUMU YA JOSEPH MBILINYI (SUGU) NA EMMANUEL MASONGA

Jana mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi, Sugu (Chadema)  na mwenzake Katibu wa Chadema Kanda ya Nyasa Emmanuel Masonga walihukumiwa kifungo jela miezi mitano kila mmoja.
Wawili hao walikuwa wameshtakiwa kwa kosa la kutumia lugha ya dhihaka dhidi ya Rais John Magufuli.

Wanadaiwa kutenda kosa hilo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika mwezi Desemba 31, 2017 jijini Mbeya.
Hukumu dhidi yao imetolewa na Mahakama ya hakimu mkazi jijini Mbeya.
Hati ya mashtaka imesema maneno waliyoyatamka yalienda kinyume na Sehemu 89(1) a ya Sheria za Jinai ambayo inaharamisha kutumiwa kwa lugha ya matusi. Maneno hayo, hati za mashtaka zinasema, yangeweza kusababisha uvunjifu wa amani.
Image result for SUGU MAHAKAMANI
Baada ya hukumu hiyo ya jana, mnadhimu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni na mwanasheria mkuu wa chama hicho (Chadema) Tundu Lissu ametoa maneno yake na hapa tunakupatia nukuu 6 za mwanasiasa huyo ambaye pia ni rais wa TLS aliyeko nchini Ubelgiji kwaajili ya matibabu baada ya kushambuliwa na risasi.
Kwanza, hukumu ya leo (jana) sio mwisho wa mjadala mahakamani. Bado kuna fursa, nay haki, ya rufaa High Court na, ikibidi, Court of Appeal.
Pili, hukumu ya leo haina maana Sugu atakaa gerezani muda wote huo. Kuna haki ya dhamana pending appeal. Ndivyo ambavyo tumefanya kwa viongozi na wanachama wetu wengi in the past. 
Tatu, hukumu ya leo haina athari yoyote kwa ubunge wa Sugu. Katiba inaweka masharti ya kifungo cha miezi sita au zaidi, na kwa makosa ya 'utovu wa uaminifu.' Uchochezi au kutoa lugha ya matusi sio makosa ya utovu wa uaminifu. 
Nne, pamoja na kwamba sijaona nakala ya hukumu, adhabu ya kifungo bila faini kwa kosa la kwanza ni kinyume na sentencing principles. Hii ni mojawapo ya hoja zetu zilizoshinda katika kesi ya Mh. Juakali High Court mwaka jana. 
Tano, hata kama atakaa gerezani muda wote huo, hukumu za kesi za kisiasa kama hii hazijawahi kuwapunguzia heshima wapigania haki popote pale duniani. 
On the contrary, kifungo cha aina hii ni beji ya heshima kwa kila mpigania haki na uhuru. Orodha ya mifano ni ndefu sana: Nyerere (ijapokuwa yeye alilipa faini), Kenyatta, Mandela, Mugabe, Fidel Castro, etc. 
Alichokifanya hakimu leo ni kuwaongeza Sugu na Masonga kwenye orodha hii ya heshima. They'll come out even bigger and stronger than when they went in. 
Sita, naunga mkono pendekezo la Mh. Zitto kwamba wabunge wetu wote warekodi maneno aliyofungiwa nayo Sugu na kuyaweka mitandaoni ili watukamate na sisi pia. 
Instead of agonising, let's organise and make this issue bigger and bigger mpaka wakimbie wenyewe au watukamate na kutufunga wote. 
Na sio wabunge tu, tuhamasishe kila mwanachama wetu na kila anayechukizwa na uonevu huu ayarudie maneno haya ili nao wakamatwe na kufungwa. 
Tumlazimishe Magufuli na watu wake waamue: waigeuze nchi nzima kuwa gereza moja kubwa, au akubali kusemwa kwa maneno na lugha asiyoipenda. Hiyo ndio maana pekee ya freedom of speech in a democracy.

0 comments:

Chapisha Maoni