Jumanne, Februari 27, 2018

UNAAMBIWA KUOGELEA BAHARINI KUNASABABISHA MAGONJWA!!!

Kuogelea baharini kunaongeza kwa kiwango kikubwa kuwa na matatizo ya tumbo , kuumwa na masikio na magonjwa mengine , watafiti wamebaini.
Chuo kikuu cha matibabu cha Exeter na kituo cha Ekolojia na maji ardhini kilifanya utafiti huo.
Ulibaini kwamba uwezo wa muogeleaji wa baharini kuwa na tatizo la masikio uko juu ikilinganishwa na waogeleaji wa maeneo mengine huku matatizo ya tumbo pia yakipanda hadi asilimia 29.

Mbali na kuogelea, hatari hizo pia zinashirikisha michezo ya baharini kama vile kuteleza kwa ubao katika mawimbi.
Watafiti waliangazia tafiti 19 zinazohusiana na uogeleaji wa baharini na magonjwa kutoka Uingereza , Marekani, Australia, New Zealnd , Denmark na Norway.
Watachanganua matokeo kutoka kwa zaidi ya watu 120,000.
''Katika mataifa yalio na wafanyikazi wenye mapato makubwa kama vile Uingereza, kuna dhana kwamba hatari za kuogelea baharini ni chache mno'', alisema Dkt Anne Leonard.Hatahivyo magazeti yetu yanaonyesha kuwa kuogelea baharini hakuongezi uwezekano wa kuugua, kama vile kuumwa na masikio mbali na matatizo yanayohusisha tumbo kama vile kuumwa na tumbo na kuendesha.
Tunadhani kwamba hii inamaanisha kwamba uchafuzi wa mazingira bado ni swala tete linalowaathiri waogeleaji katika mataifa tajiri duniani.
Mtafiti mshauri Dkt. Will Gaze alisema: Hatutaki kuwazuia watu kwenda baharini, swala ambalo lina manufaa mengi ya kiafya kama vile kuimarisha maungo.Hatahivyo ni muhimu kwamba watu wanajua athari zake ili waweze kufanya uamuzi.
Dkt Gaze amesema kwamba watu wengi hupona magonjwa hayo bila kupata tiba yoyote lakini yanaweza kuwa mabaya kwa watu wasio na kinga nzuri kama vile watu wazee na watoto.
Aliongezea: Tumetoka mbali sana katika kusafisha maji yetu, lakini ushahidi tulionao unaonyesha kuna kazi kubwa ya kufanywa.Tunatumai utafiti huu utachangia juhudu zaidi kusafisha pwani zetu.

BBC

0 comments:

Chapisha Maoni