Kundi la watu limechoma gari la mizigo baada ya dereva wake
kumgonga na kufa papo hapo muuguzi wa Zahanati ya Kaseme wilayani Geita.
Tukio hilo limetokea Jana usiku katika Kijiji cha Kaseme wakati marehemu huyo akiwa katika Bodaboda pamoja na watoto wake wawili, mmoja amefahamika kwa jina Paulo Tarafa mwenye miaka 3 na mwingine mchanga wa miezi miwili ambao wao wamenusurika na kifo hicho.
Mashuhuda wa tukio hilo wamesema lori hilo lilikuwa kwenye mwendo kasi na walipojaribu kupishana na gari jingine ndipo likawagonga na mama huyo kuumia kuanzia sehemu ya kiuno hadi miguuni na kusababisha utumbo kutoka nje.
Wamesema sababu kubwa iliyochangia watoto hao kutopatwa na madhara kama marehemu mama yao ni kwa kuwa alikuwa amewapakata kifuani ambako hawakuguswa na gari hilo.
Jina la marehemu ni Martha Paulo ambaye mwili wake umehifadhiwa katika chumba cha maiti kwenye Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Geita.

AZAM TV
0 comments:
Chapisha Maoni