Jumapili, Februari 25, 2018

WATU WANAOSHEREHEKEA SIKUKUU YA CHRISTMAS MWEZI FEBRUARI

Wanakijiji wanasema kuwa utamaduni huu ambao ulianza enzi za utumwa wakati mababu zao walipozuiwa kusherehekea Krismasi tarehe 24 Desemba kama ilivyo kawaida kwa madhehebu mengi ya Kikristo.
Badala yake waliamua kuchagua katikati mwa mwezi wa Februari na utamaduni huu umeendelea tangu wakati huo.
Fataki, muziki na densi huwa sehemu ya sherehe hizo za kuvutia.
"Watu waliotufanya watumwa walisherehekea Krismas Desemba na hatukuruhusiwa kuwa na mapumziko siku hiyo, lakini tukaambiwa tuchague siku nyingine," alisema, Holmes Larrahondo, mratibu wa sherehe.
"Katika jamii yetu tunaamini kwamba mwanamke anapaswa kufunga siku 45 baada ya kujifungua, kwa hivyo tunasherehekea Krismas sio mwezi Disemba, bali Februari, kwa hiyo Maria anaweza kudensi pamoja nasi," aliongeza Bw Larrahondo.

Balmores Viafara, mwalimu mwenye umri wa miaka 53 aliliambia shirika la habari la Ufaransa AFP kwamba kutokana na hilo kwake tarehe 24 Disemba "ni kama siku nyingine yoyote ile ".
Wakati wa kuabudu, sherehe hizo huitwa "sherehe za kutoa heshma kwa Mungu wetu kwa namna yetu."
Kama sehemu ya sherehe hizi, wanakijiji hutembelea nyumba mbali mbali "wakimtafuta mtoto Yesu", ambaye huwakilishwa na sanamu ya mbao ambayo hutunzwa na mmoja wa wanavijiji katika nyumbani kwake kwa kwa kipindi cha mwaka kilichosalia.

Pale sanamu inapopatikana, hutembezwa kijijini na wakazi wa rika zote waliovalia kama malaika na wanajeshi.
Wacheza densi, hucheza densi inayoitwa fuga; ambapo hucheza wakiigiza hatua za watumwa waliofungwa minyororo.
Sherehe humalizika majira ya asubuhi mapema.

0 comments:

Chapisha Maoni