Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria
amesema katika Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwamba, maafisa
wa nchi yake bado wanafanya jitihada za kuwakomboa wasichana wa shule
karibu 200 waliotekwa nyara na kundi la kigaidi la Boko Haram mwezi
Aprili.
Rais Jonathan ameongeza kuwa, ingawa miezi zaidi ya mitatu
imepita tangu wasichana hao wa shule watekwe nyara, lakini hawajaacha
kufanya jitihada za kuwakomboa. Rais wa Nigeria anakosolewa ndani na nje
ya nchi kwa kuchelewa kuchukua hatua za kuwakomboa wasichana hao
waliotekewa nyara na Boko Haram na kushindwa kulitokomeza kundi hilo.
Wakati huo huo, jeshi la Nigeria
limetangaza kwamba, zaidi ya wapiganaji 135 wa kundi la Boko Haram
wamejisalimisha kwa vikosi vya usalama vya serikali na kukabidhi silaha
zao huko kaskazini mashariki mwa nchi.
0 comments:
Chapisha Maoni