Mtu mmoja amefariki Mkoani Iringa kwa ajali ya barabarani huku jeshi la
polisi likimshikilia mtu mmoja kwa tuhuma ya kukutwa na madawa ya
kulevywa aina ya bhangi.
Kamanda wa jeshi la polisi Mkoani Iringa ACP Ramadhani Mungi amesema
Godfrey Nkini umri miaka 40 mkazi wa Dar es Saalam amefariki baada ya
kutokea ajali ya kugongana kwa magari mawili ya mizigo maeneo ya
Rungemba barabara kuu ya Iringa-Mbeya wilaya ya Mufindi Mkoa wa Iringa.
Kamanda Mungi ameongeza kuwa ajali hiyo imehusisha gari lenye namba za
usajili T.135 BTD likiwa na tera namba T.347 BAS aina Scania lililokuwa
likiendeshwa na marehemu akitokea nchini Congo kuelekea Dar es Salaam na
kugongana na gari namba T.538 APP lenye tera namba T.605 BFM Aina ya
Scania likiendeshwa na Charles Paison umri miaka 40 mkazi wa Mbeya.
Aidha amesema ajali hiyo imepelekea majeruhi kwa Charles Paison na
Thabiti Saleh umri miaka 30 mkazi wa Dar es Salaam ambao wamelazwa
hospitari ya Mafinga wilaya ya Mufindi Mkoa wa Iringa kwa matibabu
zaidi chanzo chake kikiwa ni mwendo kasi.
Hata hivyo Kamanda Mungi amesema askari polisi wakiwa doria maeneo ya
Makorongoni Manispaa na Mkoa wa Iringa wamemkamata Zarina Juma umri
miaka 25 mkazi wa mawelewele Manispaa ya Iringa akiwa na bhangi kete 68
alizozihifadhi kwenye mfuko wa suruali chanzo kikiwa ni kujipatia
kipato.
0 comments:
Chapisha Maoni