Jumanne, Septemba 30, 2014

TAREHE YA LEO KATIKA HISTORIA

Tarehe 30 Septemba miaka 29 iliyopita alifariki dunia mvumbuzi wa kipimo kinachotumiwa kupimia nguvu ya mitetemeko ya ardhi Charles Richter. Charles Richter alishirikiana na mhakiki mwingine kusanifu nguvu ya mitetemeko kwa mujibu wa nishati inayotokana na mawimbi ya mitetemeko hiyo toka daraja moja hadi 9 na kusajili kipimo cha Rishta. Kabla ya hapo wataalamu walikuwa wakipima mitetemeko ya ardhi kwa mujibu wa athari zake, kipimo ambacho hakikuwa cha kuaminika.

Siku kama ya leo miaka 48 iliyopita nchi ya Botswana ilifanikiwa kupata uhuru kutoka kwa mkoloni Mwingereza. Mwaka 1885 Botswana iliwekwa katika himaya ya mkoloni Mwingereza. Tangu mwaka 1920 mapambano makali ya wapigania uhuru nchini humo yalishadidi na Botswana ikapata uhuru mwaka 1966 na kukaundwa serikali ya jamhuri. Botswana inapatikana kusini mwa bara la Afrika na inapakana na nchi za Afrika Kusini, Zimbabwe na Namibia.

0 comments:

Chapisha Maoni