Mtandao wa kijamii wa Ello unapokea
maombi 31,000 ya watumiaji wanaotaka kujiunga kila saa moja hali ambayo
inaibua ushindani mkubwa kwa mtandao wa Facebook.
Muanzilishi wa mtandao huo Paul Budnitz ameiambia BBC kuwa wakati mtandao huo unaazishwa ulilenga watu kuhudumia marafiki 90 tu.
Mtandao
huu kwa mjibu wa muanzilishi umeanzishwa August mwaka huu ukiwa ambapo
hauna gharama yoyote kwa mtumiaji iwe matangazo ama kulipia data.
Hata
hivyo baadhi ya watumiaji wameubatiza kwa jina la Anti-Facebook mtandao
huo, wakimaanisha kwamba ndiye mpinzani mkubwa wa Facebook.
Baadhi
ya wataalam wa masuala ya kimitandao wamekosoa mfumo wa Ello kutotoza
gharama yoyote wakidai kuwa katika siku za usoni huenda mtandao wa Ello
utalazimika kutoza kiasi kidogo cha fedha kwa watumiaji wake.
Paul
Budnitz mtengenezaji wa baiskel za kampuni ya Vermont ameiambia BBC
kuwa wapo imara katika ushindani wa kimitandao na kujigamba kuwa ana
wataalamu wa kutosha kukabiliana na makampuni pinzania.
Hata hivyo
kuhusiana na baadhi ya watu kuuiita kwa jinala bandia la anti-Facebook
mtandao huo yeye amesema wanajiendesha kama mtandao wenye mtazamo wake
binafsi na si kutegemea mtazamo wa mtandao wa Facebook.
0 comments:
Chapisha Maoni