Vyombo vikuu vya habari duniani vimejizuia kurusha hewani matamshi ya
Rais wa Argentina katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ambayo
yalikosoa vikali siasa za Marekani kimataifa.
Katika hotuba yake kwenye mkutano wa 69 wa Baraza Kuu, Bi. Cristina
Fernandez de Kirchner Rais wa Argentina ameelezea masuala mbalimbali
kuanzia mabadiliko yanayotakiwa kwenye Mfuko wa Fedha wa Kimataifa hadi
matatizo ya Wapalestina na vita dhidi ya ugaidi.
Ameihoji Marekani kwamba imekuwaje sasa inashambulia baadhi ya
makundi kama lile la kigaidi la Daesh ambalo imekuwa ikiliunga mkono ili
liangushe serikali ya Syria.
Rais hiyo amekosoa siasa za alizoziita za ‘kindumilakuwili’ za
Marekani, na kuuliza kwamba
Daesh na Al Qaeda wanapata wapi silaha? Jana walikuwa makundi ya ukombozi na leo ni magaidi?
Katika hatua nyiningine, rais huyo wa Argentina ametupilia mbali
madai yanayotolewa dhidi ya Iran tangu mwaka 1994 kuhusiana na
shambulizi la bomu lililolenga kituo cha Mayahudi mjini Buenos Aires, na
kusema kwamba uchunguzi uliofanywa na na nchi yake umethibitisha kwamba
Iran haikuhusika katika shambulio hilo.
Wapiganaji wa kudni la Daesh ambalo sasa ni kundi la kigaidi, mwaka
2012 lilipewa mafunzo na maajeti wa shirika la kijesusi la Marekani
(CIA) huko nchini Jordan kwa lengo la kuiondoa madarakani serikali ya
Syria.
0 comments:
Chapisha Maoni