Siku kama ya leo miaka 22 iliyopita, ulifanyika uchaguzi huru wa
kwanza nchini Angola. Katika uchaguzi huo chama cha MPLA kilichokuwa
kikiongoza nchini humo tangu mwaka 1976 kilipata ushindi na kiongozi
wake Jose Edward Dos Santos akachaguliwa tena kuingoza nchi hiyo. Ni
vyema kuashiria hapa kwamba, Angola ilitumbukia katika vita vya wenyewe
kwa wenyewe baada ya kupata uhuru kutoka kwa mkoloni Mreno hapo mwaka
1975. Vita vya ndani nchini humo vilihitimishwa rasmi mwaka 2002 baada
ya kuuawa kiongozi wa chama cha upinzani cha UNITA Jonas Savimbi.
Siku kama ya leo miaka 33 iliyopita, muwafaka na tarehe 7 Mehr 1360
Hijria Shamsia, aliuawa shahidi Hujjatul Islam Sayyid Abdul Karim
Hasheminejad mwanachuoni na mwanamapambano shupavu wa Iran katika mji wa
Mashhad. Sayyid Hasheminejad aliuawa shahidi baada ya kupigwa risasi na
mmoja wa wanachama wa kundi la Munafikiin. Mwanachuoni huyo alikuwa
mstari wa mbele katika harakati za mapinduzi nchini Iran dhidi ya
utawala wa Shah, na aliwahi kuteswa na kuwekwa gerezani mara kadhaa.
Siku kama ya leo miaka 113 iliyopita, alizaliwa mwanafizikia
mashuhuri wa Italia Enrico Fermi katika mji wa Roma. Baada ya
kukamilisha masomo ya chuo kikuu aliweza kuvumbua kanuni ya Mwendo wa
Molekuli ya Gesi. Fermi alifanya uchunguzi kuhusu mabadiliko ya atomu na
akafanikiwa kutengeneza betri ya atomu kwa kuipasua na kutoa nje
nishati yake. Mwanafizikia huyo wa Italia alifariki dunia mwaka 1954.
Na miaka 96 iliyopita muwafa na leo, nchi ya Bulgaria ilisalimu amri
baada ya kushindwa mara kadhaa katika Vita Vikuu vya Kwanza vya Dunia.
Bulgaria ilikuwa pamoja na Ujerumani, utawala wa Othmania, Austria na
Hungary na zilikuwa zikipigana dhidi ya Ufaransa, Russia, Uingereza na
Italia. Baada ya Bulgaria kushindwa katika vita vya Macedonia, Desemba
15 mwaka 1918 ilitia saini Mkataba wa Salonica katika mji wenye jina
hilo nchini Ugiriki ya leo.
0 comments:
Chapisha Maoni