Jumatatu, Septemba 29, 2014

KUBWA KUTOKA IRINGA LEO

Ili kuwa na maendeleo ya elimu wazazi na walezi Mkoani Iringa wametakiwa kuendelea na uchangiaji wa michango ya sekta hiyo na kutowaruhusu wanafunzi waliohitimu darasa la saba kwenda kutumikishwa kazi za ndani.
Akiwa katika mahafari ya darasa la saba shule ya msingi Ilambilole wilaya ya Iringa Vijijini Mwenyekiti wa jumuhiya ya wazazi Mkoa wa Iringa Bw.Ephrahim Mhekwa amesema nidhamu kwa wanafunzi na ushirikiano wa kutosha kati ya walimu na wazazi hupelekea ufaulu mzuri kwa wanafunzi.
Bw.Ephrahimu ameongeza kuwa wananchi wanatakiwa kufanya kazi kwa bidii wakizingatia uhifadhi wa mazingira pia kuwa makini na matamko yanayotolewa nabaadhi ya vyama vya pamoja kuelimishana wao kwa wao juu ya maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi.
Aidha wakisoma lisara mbele ya mgeni rasmi wahitimu wa shule hiyo wamewataka wadau mbalimbali kutoa misaada ya hali na mali ili kupambana na changamoto za uhaba wa majengo na samani.
Hata hivyo sherehe hizo zimeenda sambamba na harambee iliyoendeshwa na diwani wa kata ya Nduli-Kising'a wilaya ya Iringa Vijijini Mh.Ritha Mlagala ambapo zaidi ya milioni mbili imepatikana pia mabati 50,siment 50 na madawati 10 yametolewa na mgeni rasmi Bw.Ephrahim Mhekwa kwa ajili ya ukarabati wa majengo na ununuzi wa vifaa mbalimbali vya shule hiyo.

0 comments:

Chapisha Maoni