Mshambuliaji kutoka nchini Uingereza na klabu ya Man Utd,
Wayne Mark Rooney amewataka radhi wachezaji wenzake kufuatia adhabu ya
kadi nyekundu iliyomuangukia mwishoni mwa juma wakati wa mchezo wa ligi
dhidi ya West Ham Utd kwenye uwanja wa Old Trafford.
Rooney ambaye pia ni nahodha wa kikosi cha Man Utd, amesema hana budi
kuwataka radhi wachezaji wenzake kutokana na kufahamu kwamba aliwapa
wakati mgumu mara baada ya kuonyeshwa kadi nyekundi zikiwa zimesalia
dakika 30 mchezo huo kumalizika.
Amesema kwa hakika muamuzi Lee Mason alikuwa sahihi kumuonyesha kadi
nyekundu kutokana na kosa la kumchezea ndivyo sivyo kiungo wa West Ham
Utd, Stewart Downing, hivyo hana budi kujutia na kukubali makosa
aliyoyafanya.
Kuadhibiwa kwa mshambuliaji huyo kwa kuonyeshwa kadi nyekundu ya moja
kwa moja kunaashiria ataikosa michezo mitatu ya ligi kuu ya soka nchini
Uingereza inayofuata ambayo itashuhudia Man Utd wakipambana dhidi ya
Everton, West Bromwich Albion pamoja na Chelsea.
Rooney atarejea kwenye kikosi cha Man Utd wakati wa mchezo dhidi ya
mabingwa watetezi Man city ambao pia ni mahasimu wakubwa wa Man Utd
mchezoa mbao utachezwa mwishoni mwa mwezi ujao.
Kadi nyekundu aliyoonyeshwa Wayne Rooney mwishoni mwa juma ni ya
kwanza tangu alivyokumbana na adhabu kama hiyo mwezi Machi mwaka 2009.
0 comments:
Chapisha Maoni