HABARI KWA WAKATI KUTOKA HAPA

Tunakuhakikishia kupata habari zote zilizo muhimu kutoka ulimwenguni kote kwa wakati, unaweza kusubscribe mtandao wetu na ukawa unapokea habari zote katika email yako punde tu tuchapishapo machapisho yetu. Jiunge na mitandao yetu ya Facebook na Twitter kutupata kirahisi.

HABARI ZA MICHEZO

Sasa Fichuo tunakuhakikishia kupata taarifa zote za kimichezo kutoka viwanja mbalimbali duniani, lengo ni kuhakikisha hupitwi na lolote katika ulimwengu wa michezo.Jiunge na mitandao yetu ya Facebook na Twitter kutupata kirahisi.

TAARIFA ZA BURUDANI NA HABARI ZA WASANII

Unapenda masuala ya burudani? Ni jukumu letu kuhakikisha unazipata info zote za burudani na wasanii wanaokupa burudani, unapata video mpya, movie pamoja na muziki. Kaa karibu nasi.

KURASA ZA MAGAZETI KILA SIKU

Tunakupatia kila ambacho kinaandikwa katika magazeti ya Tanzania na nje ya Tanzania, usitie shaka ukishindwa kununua gazeti uipendalo, sogea karibu nasi na upate kila unachokihitaji.

MAHUSIANO

Fahamu mambo mengi katika ulimwengu wa mapenzi kwa kupitia dondoo, simulizi na visa mbalimbali kupitia Fichuo Online, Jiunge na mitandao yetu ya Facebook na Twitter kutupata kirahisi.

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo HABARI VIDEO. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo HABARI VIDEO. Onyesha machapisho yote

Jumatatu, Machi 13, 2017

TAZAMA MBUNGE GODBLESS LEMA ALIVYOUNGURUMA TINDIGANI, ARUSHA +VIDEO

Akihutubia mkutano wa hadhara leo Tindigani, Arusha.Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema amewatupia lawama viongozi wa dini kwa kuwa waoga hata pale wanapoona katiba na sheria za nchi zinakanyagwa wazi wazi.
Lema ameenda mbali na kusema kama viongozi hao hawatabadilika na kuendelea kuwa waoga na wanafiki atafungua kanisa lake na kuliita Godbless lema church!
Amesisitiza haiwezekani viongozi wa dini wanahubiri mbiguni kuna barabara ya dhahabu lakini wao wanakuwa waoga kwenda kuipita barabara hiyo.Asemema viogozi wa dini wamekuwa waoga na uoga ni dhambi mbaya zaidi.

Ijumaa, Machi 03, 2017

ALICHOZUNGUMZA GODBLESS LEMA BAADA YA KUPEWA DHAMANA LEO +VIDEO

Kama ilivyokuwa ikitarajiwa, Mahakama Kuu Kanda ya Arusha Mjini baada ya kupitia hoja za mawakili pande zote leo imemwachia kwa dhamana Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Godbless Jonathan Lema.
Godbless Jonathan Lema ameachiwa kwa dhamana ya masharti ya wadhamini wawili na kusaini bondi ya shilingi milioni moja. Ukumbuke amekaa katika mahabusu ya gereza la Kisongo kwa zaidi ya miezi mitatu.

Katika viseo ni alichokizungumza Godbless Jonathan Lema baada ya kupata dhamana leo:

Jumamosi, Februari 25, 2017

TANZANIA NA UGANDA KUIMARISHA UHUSIANO +VIDEO

Serikali ya Tanzania imesema kuwa itaimarisha biashara yake na Uganda kwa lengo la kuinua uchumi wa raia wa mataifa hayo mawili.
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli amesema kuwa tayari Tanzania imeanza kutekeleza miradi mikubwa ikiwemo ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge) ambayo itakwenda pamoja na ujenzi wa bandari kavu Mkoani Mwanza ili kuwapunguzia muda wa usafiri wafanyabiashara wa Uganda wanaolazimika kusafiri hadi bandari ya Dar es Salaam kuchukua mizigo yao inayotoka nje ya nchi kwa meli.
Aidha amesema kuwa serikali yake itakarabati meli ya MV Umoja itakayovusha mizigo hadi bandari ya Port Bell kupitia ziwa Viktoria, mbali na kununua ndege 6 za kusafirisha kwa ajili ya Shirika la ndege la Taifa (ATCL) na kupunguza vizuizi vya barabarani hadi kufikia 3.
"Uwekezaji wa wafanyabiashara wa Uganda hapa nchini Tanzania una thamani ya dola za Marekani milioni 46.05 na umezalisha ajira 1,447"
"Watanzania wanaoishi Uganda ni wengi kuliko wanaoishi katika nchi nyingine yoyote duniani, hii ina maana tunapaswa kushirikiana zaidi na kufanya biashara zaidi"
Kuhusu mradi wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga nchini Tanzania, Rais Magufuli amesema Tanzania ipo tayari kuanzisha ujenzi huo baada ya kukamilisha mazungumzo ya masuala machache yaliyokuwa yaliosalia na ametaka wawekezaji waanze kazi badala kutoa visingizio.
Kwa upande wake Rais Museveni amemshukuru Rais Magufuli kwa mapokezi mazuri aliyoyapata akisema Uganda itaendelea kuwa ndugu na rafiki wa kweli wa Tanzania huku akisisitiza kuwa rafiki na ndugu wa kweli ni lazima wawe wamoja katika maamuzi na mipango mbalimbali ikiwemo maendeleo na biashara.
Vilevile Rais Museveni ametoa wito kwa nchi za Afrika Mashariki na Afrika nzima kuzungumza lugha moja na kuwa na msimamo wa pamoja ili kukabiliana na ukoloni ambao huko nyuma ulitawala kutokana na watawala wa Afrika kukosa umoja.
Kuhusu bomba la Mafuta, Rais Museveni amesema atafuatilia kwa ukaribu utekelezaji wa mradi huo hasa baada ya uamuzi kufanyika kuwa bomba la mafuta yaliyogundulika Hoima nchini Uganda litapitia Tanzania hadi bandari ya Tanga.

VIDEO YA MAGOLI YOTE MATATU KATIKA MECHI YA SIMBA VS YANGA LEO TAIFA

Klabu ya soka ya Simbaimeichapa Yanga 2-1 uwanja wa Taifa Temeke, Dar es Salaam na kuendelea kukaa kileleni mwa ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa 2016-2017.

Ikiwa ni mechi ya pili kwa msimu huu kukutana watani hao wa jadi wenyeji wa Kariakoo jijini Dar, huku ikiwa ni mchezo wa raundi ya pili, winga Ramadhani Kichuya anaifanya Simba kuzima ubishi na tambo za mahasimu wao Yanga baada ya kufunga goli la pili dk 81 baada ya lile la kusawazisha lililofungwa na Laudit Mavugo dk 66. Hii ni baada ya bao la Msuva alilofunga kwa mkwaju wa penati dk 5 na kuifanya Yanga kuongoza mpaka dk ya 65.
Video ya magoli yote matatu katika mechi hiyo hii hapa:

IKULU YA MAREKANI IMEZUIA CNN, BBC, NEW YORK TIMES, KUPATA HABARI ZAKE +VIDEO

Ikulu ya Marekani imevizuia vyombo kadhaa vya habari kuhudhuria mkutano wake na wanahabari. Miongoni mwa vilivyozuiwa ni vituo ambavyo Rais D. Trump aliviita "vyombo vya habari za uongo"
Akizungumza zaidi rais wa Marekani Donald Trump, amesema vita nyingine kubwa anayopigana ni dhidi ya habari za uongo ndio maana kaifikia hatua hiyo ngumu.
Miongoni mwa vilivyozuiwa ni CNN, BBC, The New York Times, LA Times, New York Daily News, BuzzFeed, The Hill, and the Daily Mail.

BAADA YA SAUTI KUVUJA AKIWATAJA VIONGOZI SAKATA LA WEMA, STEVE NYERERE KAYAZUNGUMZA HAYA

Mwigizaji na mchekeshaji mahiri nchini Tanzania, Steven Mengere 'Steve Nyerere', amefanya mkutano na waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Millenium Tower, Makumbusho jijini dar es Salaam ambapo amezungumza mengi juu ya kile ambacho kilisikika siku mbili zilizosikika katika sauti iliyorekodiwa kwa simu akizungumza na mama yake msanii Wema Sepetu.

Jumapili, Februari 12, 2017

ASKOFU GWAJIMA AFUNGUKA KANISANI, AAHIDI KUMSHTAKI MAKONDA +VIDEO

Askofu wa kanisa la Ufufuo na Uzima la jijini Dar es Salaam, Josephat Gwajima jana aliachiliwa na jeshi la polisi kituo cha kati jijini Dae es Salaam alipokuwa amewekwa kolokoloni baada ya kuguswa na sakata la madawa ya kulevya alipotajwa katika orodha ya pili ya mkuu wa mkoa huo Paul Makonda. 
Baada ya jana kuachiliwa, aliahidi kuwa ataongoza ibada ya leo katika kanisa lake, na hatimaye kukakucha na kisha kutimiza ahadi yake, tazama dakika 57 za mahubiri yake ya leo akiahidi kumshtaki mkuu wa mkoa Paul Makonda kwa mkuu wa nchi rais Magufuli (Video kwa hisani ya BONGO STARS TV)

Jumatatu, Januari 11, 2016

HISTORIA NA VIDEO ZA MATUKIO KATIKA MAPINDUZI YA ZANZIBAR JANUARI 12, 1964

Usiku wa tarehe 12 Januari 1964 kundi la watu 300 walikitwaa kisiwa cha Unguja wakiongozwa na mtu asiyekuwa maarufu kipindi hicho, aliyekuwa akiitwa John Okello, John Okello alikuwa akiishi Pemba ambako alitokea Uganda miaka michache tu. Ndani ya Zanzibar Okello alipata umaarufu kwa vijana majabari, ambao wengi katika wao walikuwa ni makuli na wachukuzi w meli zilizoingia na kutoka bandarini Zanzibar, kundi lake hili John Okello lilikutana kwa siri. Okello aliwapa matumaini ya mabadiliko watu wake hawa, wafuasi, ambao wakifanya kazi pamoja kwa muda mrefu, mara nyingine katika mazingira ya hatari, na tayari kufuata amri za kiongozi yeyote ambaye ataweza kuwalipa. Wao walikuwa waasi wanaotafuta makaazi.
Mchafuko wa kisiasa ulikuwa ukiongezeka ndani ya Zanzibar na Pemba tangu kifo cha Sultani Khalifa katika mwaka 1960. Sultani Khalifa alitawala Zanzibar kwa karibu ya miaka 50, tangu mwaka 1911. Baada ya udanganyifu mkubwa kwa majimbo ya uchaguzi na mseto katika chaguzi kuu mbili za mwaka 1961 vyama vikuu vilishindwa kujipatia wingi wa kura kwa kila kimoja. Waingereza waliondosha majeshi yao kikiwemo kikosi maalumu cha Kiarishi ambacho kilikuwa kimewekwa karibu na uwanja wa gofu na mpaka wa mji mkongwe mapema mwaka 1963. Wakati mfalme mpya, Jemshid akipandisha bendera ya Taifa huru la Zanzibar tarehe 12 Disemba 1963, aliadhimisha uondokaji wa Gavana wa kiingereza Zanzibar na mwisho wa ukoloni Zanzibar.

Uchaguzi mwingine uliofanyika mwishoni mwa mwaka 1963 ukiipa ushindi mdogo wa kura Muungano wa vyama viwili ZNP na (chama cha kizalendo Zanzibar) na ZPPP (Chama cha watu wa Pemba na Unguja). A.S.P (Chama cha Afro shirazi) kilikuwa kiwe kipo katika Serikali iliyo na chini ya nusu ya wabunge kwa mtindo wa bunge la Kiingereza na Sultani, akiwa kama ni mtawala tu lakini sio mtawala mwenye maamuzi ya mwisho. Taifa hili la Zanzibar ambalo lilikuwa mwanchana kamili wa Jumuia ya madola na mwanachana mpya wa Umoja wa Mataifa lilidumu kwa siku 33 tu.
Majadiliano makali ya kisiasa na maandamano yalikuwa ni matukio ya kawaida siku hizo. Nakumbuka nilikuwa naendesha baskeli kuelekea shuleni kupitia makundi ya watu yaliyokuwa yakiimba na kusifu majina mbalimbali ya viongozi wa kisiasa, huku yakivuka vizuizi vya barabara vilivyokuwa vikilindwa na askari wa kiingereza. Vikundi mbali bmali vilijadiliana juu ya mambo mbali mbali; mfano Haki dhini ya fursa, Wageni dhidi ya wenyeji wa zamani, Ubepari dhidi ya Ujamaa, Wafanyabiashara dhidi ya wamiliki ardhi, Waunguja dhidi ya Wapemba, Waasia dhidi ya pazia la nyuma la vita baridi na harakati za utaifa na kuondosha ukoloni ambazo zilikuwepo kipindi hiki ndani ya Afrika.
John Okello hakuwa na jawabu ya mambo haya nyeti, lakini alikuwa na kipawa cha kutambua kwamba vikundi hivi vinavyoshindana vinatoa nafasi nzuri kwa mtu wa harakati kama yeye Okello.
Kutoka kushoto ni Karume, Okello na Babu
Hata hivyo, watu kama mia waliojizatiti wangaliwez kutwaa vituo muhimu vya kienyeji vya habari na kambi za Polisi. Mara tu baada ya vituo vya habari na Kambi za polisi pamoja na silaha kudhibitiwa na John Okelo, Ni nani katika visiwa angeweza kumshinda? Jee, wanasiasa wangeliungana na kumshutumu na kumpinga kwa vitendo vyake visivyo halali? Au kama alivyotaraji, wangeendelea kutoaminiana na kutuhumu kwamba kati yao ndio wanaomuunga mkono? Jee, wasingelitaka kukubaliana na yeye, haraka kabla mwengineo hajafanya hivyo? John Okello alichezesha dadu usiku huo wa mwezi wa Januari.
Viongozi wa A.S.P walifadhaishwa na matendo ya Okello (wengi wao, walikuwa hata hawapo visiwani wakati huo). Walikimbilia haraka kuwaunga mkono waasi. Mamia ya wafuasi wa vyama walipigwa na butwaa juu ya wale ambao walikuwa na shuku ya kukata fundo hilo gumu la majadaliano ya kidemokrasia na kukimbilia moja kwa moja kwenye utawala. Hawawalitafuta njia ya kuiandaa jamii kwenda sambamba na kanuni zao. Kanuni siku hizo zilikuwa ni ghali sana kama sarafu ya Marekani. Ubinadamu ulikuwa ni kitu adimu sana.
Baadhi ya viongozi wa ASP baada kuona kwamba serikali itakuwa haina udhibiti na uwezo kujilinda na kutokuwa na imani matokeo ya chaguzi huria zilizofanyika, viongozi hawalitafuta njia za haraka za kuhalalisha udhibiti yale ambayo yaliitwa sasa "Mapinduzi". Makundi ya watu wenye fujo yalikuwa huru. Sheria na amani zilikuwa hazipo katika mitaa ya Zanzibar.
Walimiliki ardhi na wafanya biashara waliburutwa kutoka majumbani na madukani mwao, uporaji na mauaji yalienea mji mkongwe mzima. Kwa kweli mji wenyewe uliporwa.
Waarabu na Waasia , waliokuwa wakiunga mkono vyama vyengine waliuliwa kwa makundi. Kwa usiku mmoja maisha ya watu yasiyovika yalipotea na siku nyengine baadae maelfu ya watu waliikimbia nchi pamoja na kila walichoweza kubeba.
John Okello mwenyewe alijipachika cheo cha Jemedari Mkuu akishirikiana na bataliani zake zenye fujo walianzisha utawala wa vitisho ndani ya visiwa vya Unguja na Pemba. John Okello alitangaza vitisho visivyo vya kawaida na ahadi ya kifo kwa wote watakaojaribu kumpinga yeye. John Okello aliamini alikuwa akipokea maelekezo /dokezo kutoka kwa Mungu na akionyesha uwezo usiokuwa wa kawaida kwa kutumia nambari, kwa mfano tarehe 13 Januari, 1964, alitangaza ujumbe ufuatao." Serikali sasa inaendeshwa na sisi ikiwa mtakuwa wakaidi na kukataa kutii amri, Nitachukua hatua kali mara 88 zaidi ya hatua ninazozichukua hivi sasa" na "Na ikiwa yeyote atashidnwa kutii amri ya kutotoka nje ya nyumba kama walivyofanya wengine.sitokuwa na njia nyengine lakini kutumia silaha nzito. Sisi, ni jeshi lenye nguvu ya 99,099,000".
Vitisho vyake na uwezo wake wa kuvitekeleza viliwatia hofu raia, hasa makundi mbali mbali ya jamii zilizo ndogo. Tarehe 14 Januari, 1964 alitangaza maneno haya ya kufadhaisha" Huyu hapa ni Jemedari Mkuu wa Unguja na PembaNafikiria kuelekea kijiji cha Mtendeni kukiangamiza ikiwa watu wa hapo hawatafuata amri. Baada ya dakika 40 nitawamaliza nyote hasa Wangazija", " na kwa vijana wote wa kiarabu wanaoishi Malindi; Nitapita Malindi nikiwa nimesheheni silaha ambazo mimi mwenyewe ndie nizijuazo. Nataka kuona kila mmoja abakie na chupi na kulala chini. Nataka kuwaona wao wanaimba... Baba wa Waafrika. Mungu Mbariki yeye na malengo yake na yale ya Jemedari Mkuu"
Wakati unyanyasaji uliposima jamii za tamaduni tofauti za Zanzibar zilikuwa zimeparaganyika. Taifa la chama kimoja lilitangazwa. Lakini bado jTaifa hili likihofia uwezekano wa kufufuka upinzani kutoka kwa wapinzani waliokimbia nchi. Wanamapinduzi hawa baadae walijihakikishia udhibiti zaidi baada ya kusaini mkataba wa muungano wa Tanganyika. Hii ingeruhusu maelfu ya marafiki wa kisiasa wa Tanganyika kuingilia kati upinzani wowote wa baadae katika visiwa hivi. Askari polisi wa Zanzibar walibadilishwa kwa askari polisi kutoka Tanganyika ambao ni watiifu kwa chama na pazia la siasa za utengano ziliwakumba wazanzibari ambazo zilitakiwa kudumu kwa zaidi ya miaka 20.
Leo hii siasa hizi za utengano hazipo tena, kumalizika kwa vita vya baridi na kuelekea kwa uchumi wa kisasa umeweza kuifungulia Zanzibar milango kwa ulimwengu wa nje. Uchaguzi wa vyama vingi ulifanyika mwaka 1995 na mwengine unatarajiwa kufanyika mwaka, 2000. Viongozi wa kweli na wenye kujali hali za watu wameibuka Tanzania na hii imewafanya wakimbizi waliokimbia wakati wa mapinduzi kurejea visiwani. Uvumilivu na amani wa watu wa aina tofauti, ambayo ni tabia ya maisha ya wazanzibari, sasa hivi unajitahidi kurejea katika mitaa ya mji mkongwe.

Video zinazofuata zinaonesha ukweli wa matukio ya mapinduzi ya Zanzibar kama yalivyotukia na kurekodiwa live:

VIDEO NA PICHA WAKATI MESSI NA LLOYD, WASHINDI WA FIFA BALLON D'OR WAKITANGAZWA LEO ZURICH

Muda mfupi uliopita zile tuzo kubwa ulizozisubiri kwa muda mrefu za FIFA BALLON D'OR zimefanyika mjini Zurich na hatimaye mchezaji wa Barcelona Lionel Messi ametangazwa kuwa mchezaji bora wa kiume wakati Carli Lloyd ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa kike.
Wakati huo huo Timu bora ya mwaka FIFPro wachezaji waliopangwa katika kikosi hicho ni:

Kipa: Manuel Neuer, 

Mabeki: Thiago Silva, Marcelo, Sergio Ramos, Dani Alves

Viungo: Andres Iniesta, Luka Modric, Paul Pogba, 

Washambuliaji: Neymar, Lionel Messi, Cristiano Ronaldo

Video ya kutangazwa kwa washindi wa tuzo hizo hii hapa chini, karibu!

Jumatatu, Oktoba 27, 2014

ALICHOZUNGUMZA PADREW NEWCASTLE UNITED

Meneja wa klabu ya Alan Pardew amewatahadharisha mashabiki wa klabu hiyo kuwa wastahamilivu katika kipindi hiki ambacho inaonekana mambo yameanza kuwaendea vyema baada ya msoto wa miezi miwili iliyopita.

Pardew, amesema si wakati mzuri kwa mashabiki wa Newcastle United, kuanza kumwagia sifa kutokana na matokeo yanayooekana viwanjani, zaidi ya kuendelea kuwa pamoja na kikosi chao kwa kukipa nguvu kila kinapocheza nyumbani ama ugenini.
Amesema alikuwa katika wakati mgumu na mara kadhaa aliwasisitiza mashabiki kuwa wavumilivu na kumpa muda wa kufanya mabadiliko ya uchezaji kwenye kikosi cha The Magpies, hivi anaona bado kuna ulazima wa kaliba hiyo kuendelea.
Ushindi wa mabao mawili kwa moja dhidi ya Spurs uliopatiakana jana unakua wa pili mfululizo kwa klabu hiyo ya St James Park, ambapo hali hiyo imeanza kuwarejesha mashabiki kwenye mipango ya kuanza kumuamini Pardew.
Kabla ya ushindi dhidi ya Spurs Newcastle Utd waliifunga Crystal Palace bao moja kwa sifuri ikiwa ni baada ya matokeo ya sare ya mabao mawili kwa mawili dhidi ya Swansea City.
Kufuatia matokeo hayo Newcastle Utd wamechupa hadi katika nafasi ya 14 kwenye msimamo wa ligi wakiwa na point 10.

Jumatatu, Julai 14, 2014

VIDEO: RAIS KIKWETE AKINUNUA SAMAKI GENGENI NA KUGAWA PESA KWA RAIA

RAIS Jakaya Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete, wakinunua samaki katika kibanda, katika Kijiji cha Bweni, Wilaya ya Pangani, mkoani Tanga, juzi, baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa maabara Shuke ya Sekondari Kipumbwi. Pamoja na hayo rais Kikwete ameonekana mwenye furaha kukutana na wakazi wa mji huo kwa kusalimiana na hata kuwapa pesa (picha: Freddy Maro/Ikulu).

Jumamosi, Juni 14, 2014

FROLA MBASHA AVAMIWA NA MAJAMBAZI, ADAI WAMETUMWA NA MUME WAKE...VIDEO YA TUKIO IKO HAPA

Yaliyoibuka safari hii ni taarifa kwamba, juzikati, Flora alivamiwa na watu wasiojulikana nyumbani kwake, Tabata Kimanga jijiini Dar dakika chache baada ya yeye kuingia na gari akitokea mafichoni anakoishi kwa sasa.
Kwa mujibu wa chanzo, siku ya tukio ilikuwa  saa 9.15 alasiri ambapo Flora aliingia nyumbani kwake na kufunguliwa geti kubwa kisha kuingiza gari ndani na geti kufungwa tena.

Flora aliingia na gari akitokea hotelini anakoishi kwa sasa. Alikuwa ameshaingia na geti likafungwa. Ghafla, watu wakafika na kugonga geti hilo kwa nguvu huku wakisema watalibomoa geti kama wenyeji hao hawatafungua
kilisema chanzo.
Chanzo kikazidi kudai kwamba, ilibidi Flora apige simu polisi ili wafike kumuokoa yeye na familia yake.
Polisi wawili walifika haraka sana wakiwa na bunduki na kukuta wale watu wamekimbia maana walimsikia Flora akiongea na polisi kuomba msaada.
Lakini polisi wenyewe ilibidi watumie nguvu kubwa kugonga geti na kujitambulisha ndipo akatokea Flora na kuchungulia nje kupitia dirisha dogo. Alipowaona polisi akafungua mlango
kilisema chanzo hicho.
Akihojiwa na polisi hao, Flora alisema watu hao walikimbia na hakuwajua kwa sura wala hawakujitambulisha ni akina nani.
Alizungumza baada ya tukio, Flora alisema: 
Unajua kwa sasa nina hofu sana na nilihisi wale watu walikuwa wakinifuatilia kwa karibu kila sehemu, sasa naogopa kuendelea kuishi hapa, wanaweza kurudi na sijui lengo lao.
Hata hivyo, baada ya askari hao kuondoka katika eneo hilo, Flora naye aliingia kwenye  gari lake akiwa na mdogo wake na kuondoka.
Mume wa Flora, Mbasha naye yupo mafichoni baada ya kudaiwa kumbaka binti wa miaka 17 ndani ya nyumba yao huku utata ukitawala kuhusu ukweli wa tukio hilo ambalo limeigawa jamii.

Jumatano, Juni 11, 2014

BARACK OBAMA AWATOROKA WALIZI WAKE NA KUZAMIA MGAHAWANI KULA BURGER! VIDEO YA TUKIO IPO HAPA

Raisi wa marekani Barak Obama kwa mara nyingine, ametokea kuvunja sheria zake za kama raisi na kujichanganya na wananchi wa kawaida kama ilvyo tabia yake, hivyo kutokea kuwapa shida walinzi wake. Barack Obama aliwatoroka walinzi wake na kwenda kununua burger katika moja ya migahawa inayotumika na wananchi wa kawaida, tukio hilo lilizua uwepo mkubwa wa ulinzi kwa muda mchache tu..ikiwa hii ni mara ya pili kwa tukio kama hilo kutokea…angalia kipande hiki cha video kikionyesha tukio>>>

Jumatano, Juni 04, 2014

MAKUBWA YALIYOMKUTA DAVID BEKHAM KATIKA CHUMBA CHA KUFANYIA MASSAGE...VIDEO IKO HAPA

Mwendesha kipindi maaruf huko nchini marekani ajulikanaye kama Ellen Degenerate, anayesifika kuwzingua watu maarufu sana na wenye nguvu duniani,akiwemo Raisi wa marekani Barack Obama, kupitia show yake iitwayo TheEllenShow, hivi majuzi yalimkuta mwanasoka David Beckham pale alipojikuta anafosiwa kusema maneno bila yeye kujijua kuwa analazimishwa aseme bila hiari yake, tukio hilo lilimtokea akiwa kwenye moja ya chumba ch kufanyia massage, na kumwacha bila kutoamini kile kilichokuwa kinatokea. na hili ndio tukio zima, kupitia camera iliyofichwa katika chumba

Jumanne, Mei 20, 2014

KAMA HUKUSHUDIA MAZISHI YA ADAM KUAMBIANA JANA...BASI NI WAKATI WAKO KUTAZAMA KATIKA VIDEO NILIYOKUWEKEA HAPA


Mazishi ya mwongozaji na mwigizaji wa filamu Bongo, Adam Kuambiana yamefanyika katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar siku ya jana. Kabla ya mazishi mwili wa marehemu uliagwa na maelfu ya watu pamoja na watu mashuhuri pamoja na viongozi wa kisiasa nchini katika Viwanja vya Leaders jijini Dar. Mungu ailaze roho ya marehemu, mahali pema peponi. AMEN!

Jumapili, Mei 18, 2014

KIFO CHA ADAM KUAMBIANA KATIKA VIDEO, KUANZIA LOCATION MPAKA MOCHWARI MUHIMBILI, TAZAMA HAPA

MWIGIZAJI na Muongozaji filamu maarufu Bongo, Adam Kuambiana amefariki dunia wakati akipelekwa hospitali ya Mama Ngoma iliyopo Mwenge jijini Dar es Salaam kwa matibabu alfajiri ya kuamkia leo. Marehemu alianguka chooni akiwa location katika Gesti ya Silver Rado iliyopo Sinza kwa Remy, Dar. Kabla ya mauti kumfika, Adam alikuwa akilalamika kuwa anasumbuliwa na tumbo. MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI. AMEN!

Jumanne, Mei 13, 2014

TAZAMA VIDEO JINSI JAY Z ALIPOKUNG'UTWA NA DADA WA BEYONCE SOLANGE NDANI YA LIFT


Ni stori iliyoteka vichwa vya habari za burudani duniani kuhusu ugomvi uliozuka kwenye lifti uliomuhusisha rapper Jay Z na shemeji yake msanii Solange. Video inaonyesha Jay Z akipigwa na shemeji yake Solange kwa kutumia pochi aliyoshika mkononi na kurusha mateke mpaka kiatu kutoka.
TMZ wameripoti kuwa tukio hili limetokea kwenye After Party ya Met Gala kwenye hotel ya Standard iliyopo New York City.
Kilichoshangaza watu baada ya kutazama video hii ni kumuona Jay Z, Beyonce na Solange eneo moja na baada ya sekunde chache Solange akabadilika kama vile kunakitu alikuwa anakisubbiri kituke ndio aanze fujo. Pia video inamuonyesha Beyonce akiwa kimya pembeni mwa Jay Z bila kufanya wala kusema lolote.
Mlinzi wa Jay Z alifanya kazi ya ziada kumzuia Solange kutozidisha drama eneo hilo kijua umuhimu wa kufanya jambo hilo kuwa kimya zaidi. Video inamuonyesha Jay Z akijaribu kukaa mbali na shemeji yake na kuwa mpole zaidi bila kuongeza matatizo ata alivyo endelea kumpiga Jay Z hakufanya uamuzi mbaya.
Mlinzi wa Jay Z, Beyonce na Solange walionekana kutoka kwenye hotel hio kama vile hakuna kilichotokea ila Solange alionekana kuwa na uso wa hasira sana ila Beyonce alitabasamu kama kawaida yake. Fahamu Beyonce aliondika na dada yake huku Jay Z akiondoka kwenye Gari tofauti. Kila mtu anayefuatilia hii stori anataka kujua nini haswa kafanya Jay Z mpaka kupelekea Solange kufanya hivyo.

Jumatano, Aprili 23, 2014

MCHAKATO WA KUWAPATA WASHINDI KILIMANJARO TANZANIA MUSIC AWARDS 2014 UNAENDELEA



Kampuni ya TBL leo imekutana na wanahabari kuzungumzia mwenendo wa mchakato wa kuwapata washindi wa vipengele vya tuzo za Tanzania - Kilimanjaro Tanzania Music Award (KTMA).

Kilimanjaro Tanzania Music Awards ni tuzo pekee zinazowaenzi wasanii toka aina zote za muziki.
Tuzo hizi hufanyika kila mwaka jijini Dar es Salaam na huwatambua na kuwatunuku wadau wa muziki Tanzania toka mwaka 1999, zilipoanzishwa na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA). Toka wakati huo, tuzo hizi zimekua maradufu na zimedhaminiwa kwa ushirikiano na bia ya Kilimanjaro Premium Lager toka 2003. Zinawakilisha kilele cha maadhimisho ya kalenda ya muziki kitaifa. Washiriki huteuliwa na wananchi pia kamati maalum yenye wadau wanaoufahamu vizuri muziki wa nchini, wasanii hupigiwa kura kwa vipengele kupitia SMS na katika tovuti.
Washindi hawapati kutambulika na nafasi ya kuonekana katika vyombo vya habari tu, bali hushinda zawadi ya fedha taslimu zinazowasaidia kuendeleza muziki wao. Lengo la Kilimanjaro Tanzania Music Awards ni kuwahamasisha wasanii toka sehemu mbalimbali nchini kufikia kilele cha mafanikio ya kimuziki, kwa kutambua kwamba ndoto zao hazishii ngazi ya kitaifa, bali kimataifa pia.

Alhamisi, Aprili 10, 2014

SUALA LA SERIKALI MBILI NA SERIKALI TATU BADO LINALETA MZOZO, TAZAMA VIDEO

Huku suala la muundo wa Muungano likizidi kuligawa Bunge Maalum la Katiba, wajumbe wa Kamati mbalimbali za Bunge hilo wanaowakilisha Walio Wachache wameonekana kuunga mkono serikali tatu huku wale wanaowakilisha Walio Wengi wakiupinga. 
Mwakilishi wa Maoni ya Wachache toka Kamati No. 5 ya Bunge hilo Maalum, David Kafulila, amesisitiza kuwa serikali ya Muungano iliyopendekezwa na Rasimu ya Pili ya Katiba yaweza kujiendesha kwa kutafuta vyanzo mbalimbali vya mapato.
Kwa mfano, mapato ya ushuru wa bidhaa bandarini yanaweza kutumiwa vyema kuiendesha serikali hiyo itakayofanya kazi kwa kuzingatia mfumo wa serikali tatu: Uamuzi ambao Mh. Kafulila anaamini utajenga misingi imara ya uendeshaji wa serikali.
Hata hivyo, katika ripoti yake iliyowakilisha maoni ya Walio Wengi, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Assumpter Mshama amedai kuwa mfumo wa kiutawala wa serikali 3 utadhoofisha Muungano.
Hoja hiyo imeakisiwa katika ripoti iliyotolewa na Mwenyekiti wa Kamati No. 2, Shamsi Vuai Nahodha, aliyedai kuwa wajumbe wa Kamati yake wameukataa mfumo wa Shirikisho La Serikali Tatu wakisema unahatarisha usalama wa nchi wanachama.
Lakini mtazamo huo umepingwa na mjumbe aliyewakilisha Walio Wachache kwenye Kamati hiyo, Emmanuel Makaidi, aliyebainisha kuwa mfumo wa Serikali 3 utasaidia kukuza demokrasia, ambayo ndiyo kiini cha maendeleo ya nchi yoyote duniani.

Jumatano, Aprili 09, 2014

HUKO THAILAND MWANAUME AAMUA KUFUNGA NDOA NA MAITI YA MPENZI WAKE ILI KUTIMIZA AHADI, VIDEO YA TUKIO ZIMA IKO HAPA

In this tragic love story from Thailand, a man decided to go ahead with the wedding he and his girlfriend had planned, even though she sadly died in a car crash, just day before the big event.
29-year old Sarinya Kamsook and her 28-year-old boyfriend, Chadil Deffy, were to be married this year. A wedding is considered the most special event of a woman’s life and it was no different for Sarinya. She was eagerly counting the days to the moment when she would finally say ‘I do’, along with the love of her life, but fate had other plans for the young couple. Merely days before the wedding, Sarinya was involved in a car crash, leaving her severely injured.
She still could have been saved with timely medical attention. However, the doctors made her wait for 6 hours due to an overcrowded ICU instead of transferring her to another hospital. During this time, she succumbed to her injuries and passed away.
Deffy and Sarinya had been together for 10 years, before they finally decided to settle down. They had postponed the wedding several times, due to busy schedules and the fact that Deffy wanted to complete his education before he got married. However, after Sarinya’s untimely death, he couldn’t let her go without fulfilling her deepest desire. So, he decided to marry her anyway. On the 4th of January, in Buddhist ceremony, Deffy married the corpse of his girlfriend. The event took place in Surin, a city in northern Thailand. During the ceremony, he expressed his devotion and deep love for Sarinya. Several friends and relatives attended the wedding, and it was even aired on national television in Thailand. The story, along with pictures from the wedding have now become an internet sensation, sparking several debates.

The images show Deffy kissing the forehead of his girlfriend’s corpse and placing a wedding ring on her finger. Hopefully her soul now rests in peace, having received her final wish. As a tribute to their immense love, Thai Youtube users have created various video collages, like the one below. A Facebook page dedicated to the two has so far been “liked” by over 30,000 people.