Askofu wa kanisa la Ufufuo na Uzima la jijini Dar es Salaam, Josephat Gwajima jana aliachiliwa na jeshi la polisi kituo cha kati jijini Dae es Salaam alipokuwa amewekwa kolokoloni baada ya kuguswa na sakata la madawa ya kulevya alipotajwa katika orodha ya pili ya mkuu wa mkoa huo Paul Makonda.
Baada ya jana kuachiliwa, aliahidi kuwa ataongoza ibada ya leo katika kanisa lake, na hatimaye kukakucha na kisha kutimiza ahadi yake, tazama dakika 57 za mahubiri yake ya leo akiahidi kumshtaki mkuu wa mkoa Paul Makonda kwa mkuu wa nchi rais Magufuli (Video kwa hisani ya BONGO STARS TV)
0 comments:
Chapisha Maoni