Jumatano, Aprili 23, 2014

MCHAKATO WA KUWAPATA WASHINDI KILIMANJARO TANZANIA MUSIC AWARDS 2014 UNAENDELEA



Kampuni ya TBL leo imekutana na wanahabari kuzungumzia mwenendo wa mchakato wa kuwapata washindi wa vipengele vya tuzo za Tanzania - Kilimanjaro Tanzania Music Award (KTMA).

Kilimanjaro Tanzania Music Awards ni tuzo pekee zinazowaenzi wasanii toka aina zote za muziki.
Tuzo hizi hufanyika kila mwaka jijini Dar es Salaam na huwatambua na kuwatunuku wadau wa muziki Tanzania toka mwaka 1999, zilipoanzishwa na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA). Toka wakati huo, tuzo hizi zimekua maradufu na zimedhaminiwa kwa ushirikiano na bia ya Kilimanjaro Premium Lager toka 2003. Zinawakilisha kilele cha maadhimisho ya kalenda ya muziki kitaifa. Washiriki huteuliwa na wananchi pia kamati maalum yenye wadau wanaoufahamu vizuri muziki wa nchini, wasanii hupigiwa kura kwa vipengele kupitia SMS na katika tovuti.
Washindi hawapati kutambulika na nafasi ya kuonekana katika vyombo vya habari tu, bali hushinda zawadi ya fedha taslimu zinazowasaidia kuendeleza muziki wao. Lengo la Kilimanjaro Tanzania Music Awards ni kuwahamasisha wasanii toka sehemu mbalimbali nchini kufikia kilele cha mafanikio ya kimuziki, kwa kutambua kwamba ndoto zao hazishii ngazi ya kitaifa, bali kimataifa pia.

0 comments:

Chapisha Maoni