Yaliyoibuka safari hii ni taarifa kwamba, juzikati, Flora alivamiwa
na watu wasiojulikana nyumbani kwake, Tabata Kimanga jijiini Dar dakika
chache baada ya yeye kuingia na gari akitokea mafichoni anakoishi kwa
sasa.
Kwa mujibu wa chanzo, siku ya tukio
ilikuwa saa 9.15 alasiri ambapo Flora aliingia nyumbani kwake na
kufunguliwa geti kubwa kisha kuingiza gari ndani na geti kufungwa tena.
Flora aliingia na gari akitokea hotelini anakoishi kwa sasa. Alikuwa ameshaingia na geti likafungwa. Ghafla, watu wakafika na kugonga geti hilo kwa nguvu huku wakisema watalibomoa geti kama wenyeji hao hawatafungua
kilisema chanzo.
Chanzo kikazidi kudai kwamba, ilibidi Flora apige simu polisi ili wafike kumuokoa yeye na familia yake.
Polisi wawili walifika haraka sana wakiwa na bunduki na kukuta wale watu wamekimbia maana walimsikia Flora akiongea na polisi kuomba msaada.
Lakini polisi wenyewe ilibidi watumie nguvu kubwa kugonga geti na kujitambulisha ndipo akatokea Flora na kuchungulia nje kupitia dirisha dogo. Alipowaona polisi akafungua mlango
kilisema chanzo hicho.
Akihojiwa na polisi hao, Flora alisema watu hao walikimbia na hakuwajua kwa sura wala hawakujitambulisha ni akina nani.
Akihojiwa na polisi hao, Flora alisema watu hao walikimbia na hakuwajua kwa sura wala hawakujitambulisha ni akina nani.
Alizungumza baada ya tukio, Flora alisema:
Unajua kwa sasa nina hofu sana na nilihisi wale watu walikuwa wakinifuatilia kwa karibu kila sehemu, sasa naogopa kuendelea kuishi hapa, wanaweza kurudi na sijui lengo lao.
Hata hivyo, baada ya askari hao kuondoka katika eneo hilo, Flora naye
aliingia kwenye gari lake akiwa na mdogo wake na kuondoka.
Mume wa Flora, Mbasha naye yupo mafichoni baada ya kudaiwa kumbaka binti wa miaka 17 ndani ya nyumba yao huku utata ukitawala kuhusu ukweli wa tukio hilo ambalo limeigawa jamii.
Mume wa Flora, Mbasha naye yupo mafichoni baada ya kudaiwa kumbaka binti wa miaka 17 ndani ya nyumba yao huku utata ukitawala kuhusu ukweli wa tukio hilo ambalo limeigawa jamii.
0 comments:
Chapisha Maoni