Baada ya kutoonekana katika pozi za kimahaba kwa muda mrefu, kwa mara ya
kwanza, staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe ‘Gambe’
amenaswa ‘live’ na mwanaume anayedaiwa kuwa ni mume wa mtu.
Kwa muda mrefu Wolper amekuwa makini na picha
zake za kimahaba tangu alipokuwa akitoka kimapenzi na mfanyabiashara
maarufu jijini Dar, Abdallah Mtoro ‘Dallas’.
Awali, chanzo makini
kilipenyeza habari kuwa kuna mawasiliano yamenaswa ‘kimafia’ ambayo
yalitoka kwa Wolper kwenda kwa rafiki yake yakionesha anabanjuka na
mwanaume huyo wa mtu aliyejulikana kwa jina moja la Gee.
Chanzo hicho
kilikwenda mbali zaidi kwa kudai kwamba licha ya kuwa ni mume wa mtu,
mwanaume huyo ni bwana wa rafiki yake kutokana na mawasiliano hayo
yalivyosomeka.
Mashabiki kila siku huwa wanamtetea Wolper na skendo zake, sasa nakutumia picha pamoja na ‘chating’ zake alizokuwa akichati na shoga yake kuhusiana na jamaa huyo
kilisema chanzo hicho.
Baada ya habari hizo alitafutwa Wolper na akajieleza kama ifuatavyo:
Kiukweli kabisa bila ya hata kupepesa macho hizo picha ni zangu na zimepigwa kwa kutumia simu yangu tangu mwaka juzi lakini kuhusiana na hizo chating siyo zangu hata wewe unaweza kuwa shahidi kwani mara nyingi huwa tunachati na unajua vizuri ‘floo’ yangu katika kuandika SMS.
Hii ni mara ya pili kwa Wolper kutuhumiwa
kukwapua bwana wa rafiki yake. Hivi karibuni mshiriki wa Miss Tanzania
2012, Husna Maulid alilalamika kuwa Wolper kamchukulia bwana’ke
aliyemtaja kwa jina moja la Rajab, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo.
Si Wolper pekee, ‘trendi’ inaonesha kuwa mastaa wengi wa kike hasa wa
filamu wamefanya ishu ya kuporana wanaume kuwa sehemu ya utamaduni
katika tasnia hiyo bila kujua wanajiondolea heshima mbele ya jamii.
0 comments:
Chapisha Maoni