Jumamosi, Juni 14, 2014

FIFA 2014 BRAZIL: UHOLANZI 5-1 UHISPANIA

Mabingwa watetezi wa kombe la dunia Uhispania wameambulia kichapo cha mabao 5-1 mikononi mwa timu walioishinda katika fainali ya kombe la dunia huko Afrika Kusini miaka minne iliyopita.
Kabla ya leo Uhispania ilikuwa haijashindwa katika dakika 476 ya mechi za kombe la dunia.
Mabao hayo ni zaidi ya mabao yote waliofungwa katika mchuano wa Euro na kombe la dunia la mwaka wa 2010 huko Afrika Kusini.
Uholanzi ilitoka nyuma baada ya Xavi Alonso kuiweka Uhispania mbele kwa mkwaju wa penalti baada ya Diego Costa kuangushwa katika eneo la hatari.
Hata hivyo Robin van Persie aliisawazishia Uholanzi kwa mkwaju wa kipekee wa kichwa dakika moja tu kabla kipindi cha kwanza hakijakamilika.
Casillas alisababisha bao la Nne
Na hapo ndipo mkoko ulialika maua .
Mabingwa hao wa dunia hawakuwa na majibu ya wimbi baada ya wimbi ya mashambulizi kutoka Uholanzi Arjen Robben Robin van Persie na Wesley Sneijder waliposhirikiana kwa karibu na juhudi zao zikazaa matunda .
Arjen Robben aliiweka Uholanzi mbele kunako dakika ya 53.
Hata hivyo masihara ya kipa Iker Cassillas yalipelekea RVP kufunga bao lake la pili na hivyo kumhakikishia kocha Van gal alama tatu muhimu katika mechi yao ya kwanza ya kundi lao.
Robben kwa upande wake aliidhalilisha safu ya ulinzi ya Uhispania na kufuma bao lake la pili na la tano kwa kocha Van Gaal.
Kufuatia kichapo hicho Mabingwa hao watetezi walishuka hadi nafasi ya mwisho kwenye kundi B wakiwa wametinga idadi kubwa ya mabao ikilinganishwa na Australia na Chile .

0 comments:

Chapisha Maoni