HABARI KWA WAKATI KUTOKA HAPA

Tunakuhakikishia kupata habari zote zilizo muhimu kutoka ulimwenguni kote kwa wakati, unaweza kusubscribe mtandao wetu na ukawa unapokea habari zote katika email yako punde tu tuchapishapo machapisho yetu. Jiunge na mitandao yetu ya Facebook na Twitter kutupata kirahisi.

HABARI ZA MICHEZO

Sasa Fichuo tunakuhakikishia kupata taarifa zote za kimichezo kutoka viwanja mbalimbali duniani, lengo ni kuhakikisha hupitwi na lolote katika ulimwengu wa michezo.Jiunge na mitandao yetu ya Facebook na Twitter kutupata kirahisi.

TAARIFA ZA BURUDANI NA HABARI ZA WASANII

Unapenda masuala ya burudani? Ni jukumu letu kuhakikisha unazipata info zote za burudani na wasanii wanaokupa burudani, unapata video mpya, movie pamoja na muziki. Kaa karibu nasi.

KURASA ZA MAGAZETI KILA SIKU

Tunakupatia kila ambacho kinaandikwa katika magazeti ya Tanzania na nje ya Tanzania, usitie shaka ukishindwa kununua gazeti uipendalo, sogea karibu nasi na upate kila unachokihitaji.

MAHUSIANO

Fahamu mambo mengi katika ulimwengu wa mapenzi kwa kupitia dondoo, simulizi na visa mbalimbali kupitia Fichuo Online, Jiunge na mitandao yetu ya Facebook na Twitter kutupata kirahisi.

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo HABARI PICHA. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo HABARI PICHA. Onyesha machapisho yote

Ijumaa, Agosti 22, 2014

MAITI ILIYOZIKWA MIAKA 700 ILIYOPITA YAKUTWA HAIJAOZA, HABARI KAMILI NA PICHA 13 ZIKO HAPA

Maiti hiyo ikiwa imetolewa nje ya jeneza
Ama kweli ukistaajabu ya Musa, utayaona ya Firauni....Maiti ya mwanamke iliyozikwa miaka 700 iliyopita yagunduliwa China ikiwa haijaoza. Ipo katika hali nzuri kiasi kwamba bado ina nyusi. Inasemekana alihifadhiwa vizuri na inaonyesha alikuwa ni mtu kutoka katika familia ya ufalme. 
Maiti hiyo iligunduliwa na wafanyakazi wa barabara (wakandarasi) huko China mashariki walipopewa kazi ya kupanua barabara katika mji wa Taizhou, Mkoani wa Jiangsu. Wakandarasi hao walitakiwa kuchimba kwenda chini kiasi cha futi 6 ili kumaliza mwinuko uliokuwa katikati ya bara bara ndipo wakakutana kitu wasichotarajia kukikuta.
Walipokuwa wakichimba walikuta kitu kigumu  na baada ya kufanya utafiti wao kidogo ndipo waligundua kuwa kulikuwa kuna kaburi alilozikwa mtu na ndipo wakawaita wataalamu ili kuchunguza zaidi, baada ya hapo wakaamua kuweka wazi juu ya tukio hilo kuwa waligundua kwamba kaburi hilo lilikuwa na umri wa miaka 700. Tazama picha zaidi la sakata hilo hapa chini...
Mkandarasi akijaribu kuvunja zege lililozunguka sanduku lakini kabla hawajajua kuwa kuna maiti
Baada ya kuvunja sanduku hilo la zege
Wakihamaki baada ya kuona kitu ndani ya sanduku
Wakianza kufunua matambara yaliyo ndani ya sanduku yaliyozunguka maiti

Alhamisi, Agosti 14, 2014

UKIZIONA PICHA HIZI, HUTOMRUHUSU MPENZI WAKO AENDE CLUB USIKU PEKE YAKE


Mkesha kwaajili ya kusubiri sikukuu fulani ninavyoelewa mimi ni kwamba inatakiwa tukeshe tukiwa tunasali lakini hili liko tofauti kwa watu wa dunia hii wameigeuza mikesha hii kuwa usiku wa kufanya maovu hii inahuzunisha sana watu wanakunywa na kulewa bila kujali lililowaweka pale hebu angalia picha hizi ambazo mtandao huu umezipata kutokana na mkesha wa juzi tu hapa

Jumatano, Agosti 06, 2014

PICHA ZA UBAKAJI ZAZUA TAFRANI INDIA

Picha za wanamitindo zilizopigwa kwenye basi zikionyesha mwanamke akionekana kama anayebakwa na wanaume, zimezua hisia kali kwenye mitandao ya kijamii nchini India. Watu wengi wamesema kuwa picha hizo zinaonekena kusifu kitendo cha ubakaji kilichomkuta mwanafunzi mmoja mjini Delhi kwenye basi mwaka 2012.

Mwanafunzi huyo ambaye aliga baadaye, alibakwa na genge la wanaume. Picha za mpiga picha Raj Shetye ambaye alipiga picha hizo, zinaonyesha mwanamke akioenekana kupigania maisha yake akiwa amezuiliwa na wanaume wawili kwenye kiti cha basi.
Ni kitendo ambacho kinaleta hisia kali kwa watu wengi na kumbukumbu za unyama uliotendewa msichana wa shule kwenye basi hadi akafa. Watu wengi kwenye mitandao ya kijamii wanasema picha hizo ni za kukera na zinatisha .
Bwana Shetye hata hivyo amejitetea akisema picha hizo ni za kuonyesha tu hali inayowakumba wanawawake wengi nchini huo wala sio kuonyesha ubakaji. Hata hivyo picha hizo ziliondolewa kwenye mtandao huo wa Behance baada ya hisia kali kutoka kwa watumiaji waTwitter na Facebook.

Ubakaji wa msichana huyo aliyekuwa na umri wa miaka 23 ulisababisha maandamano makubwa nchini humo na hata kulazimisha maafisa wakuu kuweka mikakati mipya ya kukabiliana na ubakaji
BBC ilijaribu kumtafuta Bwana Shetye aweze kujieleza kuhusu picha hizo ingawa hatukufanikiwa badli vyombo vya habari vilimnukuu akisema hakua na nia ya kuleta kumbukumbu mbaya kuhusu kitendo cha ubakaji kilichozua hasira kote nchini India.

Jumatano, Julai 30, 2014

KATI YA BARABARA HATARI ZAIDI DUNIANI

Kuna maeneo mengi hatari duniani kwa madereva watumiapo vyombo vya moto, lakini leo katika Fichuo Tz Blog nataka uifahamu barabara iitwayo Atlantic Ocean Road iliyo Norway ni barabara yenye umbali wa kilomita 8.3 ambayo inatajwa kuwa mojawapo ya barabara hatari kutumiwa na madereva duniani!

Jumatano, Juni 25, 2014

SIMU ZILIVYOTUMIKA JANA BUNGENI DODOMA BAADA YA UMEME KUZIMA

Sakata la umeme kukatika nchi nzima kwa mikoa inayohudumiwa na GRIDI ya Taifa! Wabunge wakisoma kwa kutumia mwanga wa tochi za simu ndani ya Bunge jana mara baada ya umeme kuzima katika ukumbi huo wakati walipokuwa wakipiga kura kupitisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2014/15.

Jumamosi, Juni 14, 2014

KIUMBE CHA AJABU CHAKUTWA KATIKA SOKO LILILOUNGUA DAR ES SALAAM

Najua wewe ni mfuatiliaji mzuri wa habari hasa za hapa nyumbani Tanzania, na ninauhakika kuwa ulipata habari na picha juu ya kuungua mabanda ya wamachinga katika soko la Karume jijini Dar es Salaam au ulishuhudia live kama ulifanikiwa kufika katika eneo la tukio.
Sasa kufuatia lile tukio, ni kwamba kuna kiumbe cha ajabu kimekutwa katika sehemu iliyoteketea kwa moto na mpaka sasa bado haijafahamika kuwa ni kiumbe gani, wapo wanaodai kuwa ni paka, wengine wana sema kuwa ni mtu na maoni mengine mengi sana, hebu tazama kwa muda wako kama utaweza kutambua kiumbe hiki>>>

Jumatano, Juni 11, 2014

BREAKING NEWS: MABANDA YA WAMACHINGA SOKO LA KARUME YANAWAKA MOTO USIKU HUU, PICHA NNE ZA TUKIO ZIKO HAPA

Mabanda ya wamachinga eneo la Soko Karume yanaungua na moto. Habari zaidi zitafuata. Moto bado ni mkali, unazidii kusambaa na sasa unaelekea Breweries. Usipothibitiwa Mapema utaleta athari kubwa sana.
Hali bado ni tete, Fire walifika katika eneo la tukio na sasa wanaondoka bada ya kukubali kushindwa, hakuna wanachoweza kuokoa.
Nguzo za umeme zinaungua pia.
Kuna umati wa watu mkubwa, baadhi wanalia kwa uchungu wakiwa wamejishika kwa kukata tamaa.

HILI NDIO KABURI LILILOVUNJA REKODI YA DUNIA


Sasa uachane na stori zote za watu maarufu na wasio maarufu, matajiri na masikini waliokufa na kuzikwa ndani ya majeneza mazuri na yaliyo na thamani kubwa, hayo tulikwisha yazoea kitambo sana, kiboko cha yaote mtu aliyezikwa katika kaburi lililotengenezwa kama chumba cha kulala kilicho na samani tofauti za thamani kubwa sana kama vile flat screen, dreassing table, kitanda na vitu vingine vingi mpaka mvinyo, perfumes na vingine vingi, hii ndio top katika dunia hii, angalia picha zaidi  za tukio hilo...

Alhamisi, Juni 05, 2014

MPENZI WA YOUNG KILLER 'MRS SUPERSTAR' AACHIA PICHA TATA

Mrembo ambaye amekuwa katika headlines tofauti katika social networks na media mbalimbali baada ya kubadili noti za Tsh. 10,000 kuwa shuka, na mpenzi wa staa wa muziki wa hip hop Tanzania Young Killer aitwaye Halimaty ameingia katika scandal mpya baada ya kupost picha katika pozi tofauti na nguo zinazoacha maungo yake ya siri hadharani
'Mrs. Superstar' huyo amepiga picha hizo akiwa katika sweeming pool, unaweza kuziona hapa

Jumatatu, Juni 02, 2014

MWILI WA MTOTO WA BOX 'NASRA RASHID' UMEWASILI MOROGORO, HUZUNI YATANDA...WAANDISHI WA HABARI WAFURIKA

Mwili wa Nasra ukipelekwa mochwari kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.
Mwili wa mtoto Nasra Rashid ukiwasili katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro
Wanahabari wakichukua matukio wakati mwili wa mtoto Nasra ukiwasili katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.
Mwili wa mtoto Nasra ukiwa mochwari.
Waombolezaji wakiangua kilio baada ya mwili wa marehemu Nasra Rashid (4) kuwasili mkoani Morogoro.

Jumatano, Mei 28, 2014

MMILIKI WA TIMU YA MANCHESTER UNITED AMEFARIKI DUNIA! TAZAMA PIA MALI ZAKE ZA THAMANI ALIZOZIACHA

MMILIKI wa timu ya Manchester United, Malcolm Glazer, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 85. Amefariki akiwa nyumbani kwake Marekani.
Glazer aliinunua klabu hiyo mwaka 2005 kwa pauni milioni 790 sawa na shilingi trioni 2.2 na akashuhudia timu hiyo ikipata mafanikio kadhaa ikiwemo kutwaa Kombe la Klabu Bingwa Ulaya na ya Ligi Kuu ya England.

SHETANI YUKO KAZINI! MWANAMUZIKI WA INJILI AACHIA PICHA YA UCHI

Sasa nimeamini Shetani ana nguvu kubwa na roho ya ushawishi kuliko kiumbe kingine chochote cha duniani...kweli yuko kazini! Hivi unapata taswira gani unaposikia kuwa eti Rose Muhando au Bahati Bukuku anapiga picha za uchi? Ni kweli inashtua sana, na hii imetokea huko Nigeria ambaho mwanamuziki wa muziki wa dini Maheeda amedhihirisha kukamatwa hasa na pepo mchafu baada ya kuendelea kufyatua picha za uchi kila uchao!!!!!!!!!!!!

Jumatatu, Mei 26, 2014

TATTOO MPYA YA RICK ROSS KIDEVUNI..AMEANDIKA RICH FOREVER

Unaweza kuwa na sehemu katika mwili wako ambayo ni chaguo lako kwaajili ya kuchorwa tattoo, mgongoni, mikononi, kifuani na hata usoni, sasa hii ya sasa ndio kali zaidi...
Msanii maarufu wa Marekani Rick Ross amechora tattoo- chini tu ya mdomo wake- inayosema 'Rich Forever' yaani 'Tajiri Milele'.
Sehemu hiyo ya uso wake ndio mahala pekee penye nafasi ya kuchora tattoo hiyo kutokana na eneo jingine la uso wake kuwa na ndevu zinazotunzwa vizuri.
Bila shaka kuona maneno hayo kila siku anapojitazama kwenye kioo itakuwa motisha ya kuhakikisha anakuwa tajiri milele.

Alhamisi, Mei 22, 2014

FAHAMU MITINDO MITANO YA NYWELE ILIYOKUWA GUMZO ZAIDI VIWANJANI

Balloteli is an Italian international, who is currently playing for AC Milan. Apart from being classified among world class bad boys in football, Mario Balloteli is also known for his funny and crazy haircut.
Giovanni is an Argentina international footballer who plays for his home club Liver Plate, His hairstyle surprises everyone because of its uniqueness and the way he takes care of it.
Kidiaba is a Congolese goalkeeper who plays for his home club T.P MAZEMBE and the Congolese National team. His haircut and goal celebration have been very famous in the 2008 Africa Cup of Nations.
Also known as El Fenomeno, Ronaldo is a retired Brazilian footballer who is considered as a legend in the national team and his former clubs like Real Madrid and AC Milan. His haircut has been famous in the 2002 World Cup.
Taribo West is a retired Nigerian international; he played in different European clubs like inter Milan and AC Milan. His hairstyle is the most remembered in football history.