Jumatatu, Mei 26, 2014

TATTOO MPYA YA RICK ROSS KIDEVUNI..AMEANDIKA RICH FOREVER

Unaweza kuwa na sehemu katika mwili wako ambayo ni chaguo lako kwaajili ya kuchorwa tattoo, mgongoni, mikononi, kifuani na hata usoni, sasa hii ya sasa ndio kali zaidi...
Msanii maarufu wa Marekani Rick Ross amechora tattoo- chini tu ya mdomo wake- inayosema 'Rich Forever' yaani 'Tajiri Milele'.
Sehemu hiyo ya uso wake ndio mahala pekee penye nafasi ya kuchora tattoo hiyo kutokana na eneo jingine la uso wake kuwa na ndevu zinazotunzwa vizuri.
Bila shaka kuona maneno hayo kila siku anapojitazama kwenye kioo itakuwa motisha ya kuhakikisha anakuwa tajiri milele.

0 comments:

Chapisha Maoni