Picha za wanamitindo zilizopigwa kwenye basi
zikionyesha mwanamke akionekana kama anayebakwa na wanaume, zimezua
hisia kali kwenye mitandao ya kijamii nchini India. Watu wengi wamesema kuwa picha hizo zinaonekena
kusifu kitendo cha ubakaji kilichomkuta mwanafunzi mmoja mjini Delhi
kwenye basi mwaka 2012.
Mwanafunzi huyo ambaye aliga baadaye, alibakwa na genge la wanaume. Picha za mpiga picha Raj Shetye ambaye alipiga
picha hizo, zinaonyesha mwanamke akioenekana kupigania maisha yake akiwa
amezuiliwa na wanaume wawili kwenye kiti cha basi.
Ni kitendo ambacho kinaleta hisia kali kwa watu
wengi na kumbukumbu za unyama uliotendewa msichana wa shule kwenye basi
hadi akafa. Watu wengi kwenye mitandao ya kijamii wanasema picha hizo ni za kukera na zinatisha .
Bwana Shetye hata hivyo amejitetea akisema picha
hizo ni za kuonyesha tu hali inayowakumba wanawawake wengi nchini huo
wala sio kuonyesha ubakaji. Hata hivyo picha hizo ziliondolewa kwenye mtandao huo wa Behance baada ya hisia kali kutoka kwa watumiaji waTwitter na Facebook.
Ubakaji wa msichana huyo aliyekuwa na umri wa
miaka 23 ulisababisha maandamano makubwa nchini humo na hata kulazimisha
maafisa wakuu kuweka mikakati mipya ya kukabiliana na ubakaji
BBC ilijaribu kumtafuta Bwana Shetye aweze
kujieleza kuhusu picha hizo ingawa hatukufanikiwa badli vyombo vya
habari vilimnukuu akisema hakua na nia ya kuleta kumbukumbu mbaya kuhusu
kitendo cha ubakaji kilichozua hasira kote nchini India.
0 comments:
Chapisha Maoni