Uongozi wa klabu ya Young Africans leo umefanya mkutano na waandishi
wa habari juu na kusema kilichofanywa na waandaji wa michuano ya Kombe
la Vilabu Bingwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kuiondoa
timu isishiriki ni cha kushangaza sana na kinadidimiza soka kwa ujumla.
Katibu Mkuu wa Young Africans Bw Beno Njovu amesema walipata barua ya
mwaliko wa kushiriki mashindano tarehe 25/7/2014 na kudhibitisha
kushiriki michuano hiyo kwa kuandika barua iliyokwenda TFF na kisha wao
kuiwasilisha kwa CECAFA.
Baada ya kudhibitisha kushiriki michuano hiyo tuliambiwa na CECAFA tutume orodha ya wachezaji na viongozi ambao watasafiri kuelekea nchini Rwanda kwenye michuano hiyo ili waweze kuandaa tiketi za ndege na sehemu ya malazi kitu ambacho tulitimiza
alisema Beno.
Lakini
katika hali ya kushangaza jana tulipokea barua kutoka TFF ikisema
CECAFA imetuondoa kwenye mashindano hayo kwa kushindwa kukidhi vigezo na
kuiteua timu ya Azam kuchukua nafasi yetu "aliongeza Beno."
Kanuni
za CECAFA zipo wazi kuwa wachezaji wanaopaswa kushiriki michuano hiyo
ni lazima wawe na leseni za kucheza mpira kutoka kwa chama husika, jambo
ambalo ambalo orodha tuliyowapelekea wachezaji wote wataichezea Yanga
msimu huu wa 2014/2015.
Kocha Marcio Maximo alianza maandalizi ya
kikosi ambacho kingekwenda kushiriki michuano hiyo ambayo ilipaswa
kuanza ijumaa tarehe 8/8/2014 kwa Yanga kufungua dimba la wenyeji timu
ya Rayon FC .
Kikosi ambacho kocha mkuu alikichagua kwenda kwenye
michuano ya Kagame kilikua na jumla ya wachezaji 20, 15 wakiwa kutoka
timu ya kikosi cha wakubwa na wachezaji watano wakitoka kikosi cha pili
U20 chini ya kocha Leonado Neiva ambaye amekua na wachezaji hao kwa
takribani mwezi mmoja.
Lakini walichokiamua CECAFA ni kuiondoa
klabu ya Yanga na kuipa nafasi timu nyingine kwa kusema kikosi
kilichopelekwa hawakubaliani nacho na hata kocha mkuu Marcio Maximo
haendi, hao ndo tulipojua ya kuwa wanataka majina ya watu na sio timu.
Zifuatazo ni sababu za Kiufundi ambazo Yanga ilizipelekea CECAFA kuhusu kikosi hicho kutojumuisha wachezaji wa timu za Taifa.
a)
Ripoti ya kocha aliyeondoka Yanga msimu uliopita Hans ilitoa maelekezo
ya kupunguza wachezaji tisa (9) na wachezaji wawili kujiunga na klabu ya
Azam hivyo kufanya kikosi kupungua wachezaji 11 kutoka katika idadi ya
wachezaji 30 wa msimu uliopita.
b) Wachezaji 10 wa Yanga wamekuwa
na majukumu ya timu za Taifa za Tanzania (Taifa Stars), Rwanda na Uganda
tangu Aprili 19, 2014 mpaka mwanzoni mwa Agosti, takribani miezi mitatu
wamekuwa kambini bila kupata muda wa kupumzika.
c) Benchi la
Ufundi la Yanga ni jipya kuanzia kocha mkuu Maximo na wasaidizi wake
watatu Leonardo Neiva, Salavatory Edwarda na Shadrack Nsajigwa hivyo
wanahitaji muda wa kuwajua wachezaji waliokuwa kwenye timu ya Taifa ndo
maana hawakuwajumuisha kwenye kikosi cha kwenda Kigali Rwanda.
d)
Baadhi ya wachezaji wanahitaji Vibali vya kufanyia kazi nchini,
uhamisho wa Kimataifa (ITC) ili waweza kushiriki michuano ya Kagame, na
moja ya kanuni za CECAFA mchezaji anayeshiriki mashindano hayo ni lazima
awe na leseni ya kucheza mpira kwa ligi ya ndani.
e)
Katika wachezaji 20 waliochaguliwa kushiriki michuano ya Kagame,
wachezaji 6 wamepandishwa moja moja katika kikosi cha wakubwa msimu huu
hivyo kufanya idadi ya wachezaji wa U20 kuwa watano tu.
f)
Wachezaji walikokuwa kambini Taifa Stars kwa takribani miezi mitatu
bila ya kupumzika, daktari alipendekeza wapate japo siku kumi na nne
(14) za kupumzika ili miili yao iweze kupoa na kuanza upya tena
maandalizi ya msimu mpya.
g) Yangga tunaamini hakuna mtu
yoyote zaidi ya Kocha Mkuu anayeweza kutupangia kikosi cha kwanza,
sababu yeye ndio anayekaa na wachezaji mda wote na kujua ubora wa
wachezaji wake.
0 comments:
Chapisha Maoni