Wenyeji wa fainali za kombe la dunia za mwaka 2018, Urusi wameianika
hadharani nembo ambayo itakuwa utambulisho wa fainali hizo ambazo kwa
mara ya mwisho ziliunguruma huko nchini Brazil miezi minne iliyopita.
Urusi ambao ni wenyeji wa fainali zijazo za kombe la dunia wameianika
hadharani nembo hiyo katika sehemu mbali mbali na tayari imeonekana
kukubaliwa na wengi.
Ubunifu wa kuchorwa kwa nembo hiyo umefanywa na magwiji wa Sanaa
nchini Urusi na usiku wa kuamkia hii leo ilionekana katika moja ya jengo
kubwa la Bolshoi Theatre huko mjini Moscow.
Nchi ya Urusi ilishinda kuwa mwenyeji wa fainali za kombe la dunia za
mwaka 2018, baada ya kuzibwaga nchi za Uingereza, Hispania-Ureno,
Uholanzi pamoja na Ubelgiji katika kinyang’anyiro cha kupigiwa kura na
wajumbe wa FIFA kilichofanyika mwaka 2010 huko mjini Zurich nchini.
0 comments:
Chapisha Maoni