Jumatano, Oktoba 29, 2014

MCHEZAJI WA SOKA ANG'ATWA NA MBWA UWANJANI


Mchezaji wa klabu ya Sao Paulo ya nchini Brazil, mwishoni mwa juma lililopita alilazimika kutumia muda wake akiwa uwanjani kwa kumuondoa mbwa aliyekua ameingia sehemu ya kuchezea wakati wa mchezo wa ligi nchini Brazil ulipokuwa ukiendelea.
Mandai alijitolea kumtoa mbwa huyo katika sehemu ya kuchezea kwa kumbeba na kisha kukimbia nae mpaka nje, ila kwa bahati mbaya aling’atwa kidoleni lakini haikuwa kwa kiasi kikubwa.
Muda mchache baadae baada ya kufanya hivyo Mandai alifanikiwa kuifungia Sao Paolo bao la ushindi na mashabiki wengi waliamini huenda mafanikio hayo yalikuja kwa baraka za mbwa aliyembeba na kumpeleka nje ya sehemu ya kucheza.

0 comments:

Chapisha Maoni