Jeshi la Polisi mkoani Pwani limefanikiwa kumkamata Michael William maarufu (Michael dada), mkazi wa Kiluvya, wilayani Kisarawe anayetuhumiwa kuhusika na matukio ya ubakaji wa vikongwe mkoani Pwani.
Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa polisi mkoa wa Pwani Ulrich Matei alisema jeshi hilo lilikuwa likimsaka mtuhumiwa huyo kwa kipindi kirefu kutokana na kudaiwa kutenda makosa mbalimbali ya ubakaji wa vikongwe na wanawake na kutokomea kusikojulikana.
Alisema, William alitiwa mbaroni juzi baada ya kudaiwa kuhusika katika tukio la wizi wa mifugo lililotokea wiki mbili zilizopita huko Kiluvya.
Pia kamanda Matei amesema, mtuhumiwa huyo anadaiwa kuhusika katika matukio ya ubakaji zaidi ya 10 ambapo kabla ya kufanya vitendo hivyo alikuwa akiwatishia wahusika kwa mapanga.

0 comments:
Chapisha Maoni