Brunei wametangaza utumiaji wa sheria mpya kwa raia laki nne na elfu
16 wa nchi hiyo ndogo yenye utajiri mkubwa wa mafuta ambayo imekua
ikiongozwa na Hassanal Bolkiah kwa takriban karibu ya nusu karne hivi
sasa.
Bolkiah ameanzisha kanuni mpya ya adhabu ambazo zitafanyika kulingana
na mwenendo wa dini ya kiislam akisema adhabu hizi ni njia ya kufuata
maamrisho ya mwenyezi Mungu ili kulinda falme yake na ushawishi unaotoka
nchi za nje ambapo mara nyingi wamekua wakishawishika kupitia mitandao
ya kijamii.
Anasema
Allah ni mkarimu na kwa sababu ya ukarimu wake ametengeneza sheria kwa ajili yetu ili tuzitumie kupata haki katika nchi yetu, hatujawahi kuchukulia wengi vibaya na wala hatuwategemei wao kukubaliana na sisi lakini ni vizuri wakatuheshimu kama tunavyowaheshimu
Adhabu zinazohusika ni pamoja na kupigwa mawe mpaka kifo, kupigwa
mijeledi (floggings) na kukatwa viungo vya mwili kama miguu kwa makosa
kama ya uhusiano wa jinsia moja, wizi, mimba za nje ya ndoa, unywaji
pombe, kukosa kwa sala za Ijumaa, kukufuru (makosa ya lugha),ulawiti n.k
na adhabu zinaweza kupungua ama kufutwa kwa wale walio chini ya miaka
18.
Kwa sheria hizi za sasa ubatizo makanisani utashindikana kufanyika kulingana na sheria hizi mpya nchini humo ambapo tayari
tume ya kimataifa ya wanasheria (ICJ) imesema sheria hizo hazitalingana na makubaliano ya sheria za kimataifa na mkuu wa tume ya haki za binaadamu UN amesema anapingana na sheria hizo.
tume ya kimataifa ya wanasheria (ICJ) imesema sheria hizo hazitalingana na makubaliano ya sheria za kimataifa na mkuu wa tume ya haki za binaadamu UN amesema anapingana na sheria hizo.
0 comments:
Chapisha Maoni