Meneja wa Chelsea,Jose Mourinho anatazamia
kusajili mshambuliaji hatari zaidi ifikapo majira ya joto mara baada ya
kuweka wazi tatizo la ushambuliaji katika kikosi chake tangu arudi
Stamford Bridge mwaka jana.
Huku akiwa anahusishwa na kutaka kutumia fedha
nyingi kwaajili kumsajili mshambuliaji wa Atletico Madrid,Diego Costa
msimu huu na kumrudisha Fernando Torres katika klabu yake hiyo ya zamani
katika sehemu ya dili la kumpata nyota huyo.
Sare ya 0-0 dhidi ya Norwich siku ya Jumapili
ilidhihirisha tatizo hilo kwa Mourinho kufuatia timu yake kumiliki mpira
kwa kiwango kikubwa lakini ikashindwa kupata goli lolote mbele ya timu
inayohaha kutoshuka daraja.
Matokeo hayo yalikatisha matumaini ya Chelsea
katika kusaka taji la ligi kuu ya Uingereza msimu huu na Mourinho
anasema kuwa kupiga hatua hiyo atahitaji kupata aina ya mshambuliaji wa
kiwango cha hali ya juu sana.
Huku akisema,
Ukicheza dhidi ya timu zinazolinda kwa umakini zaidi bila ya kuwa na wasiwasi kuhusu kutoruhusu goli kuliko kucheza mpira,inahitaji kuwa na washambuliaji imara.
Mreno huyo anasisitiza kuwa,
Tuna wachezaji wazuri lakini hatuna aina ya washambuliaji ambao wanaweza kutumia nafasi chache ngumu,kufanya maamuzi sahihi,,kufungua nafasi na kuweza kufunga magoli.
Ndani ya michezo ya aina hii kitu pekee unachohitaji ni kufungua nafasi.Unapofungua nafasi,nafasi inafunguka na unaweza kushinda magoli zaidi.Hatukuweza kuwa na nguvu ya kufanya hivyo.
Mourinho akakiri kuwa,
Tunapaswa kujaribu kushinda kama timu,kuimarika kama timu lakini pia kuongeza mchezaji wa kushambulia ambaye anasifa bora zaidi na uwezo wa kufunga magoli ambayo yanaweza kuipandisha timu katika daraja tofauti kabisa.
0 comments:
Chapisha Maoni